Kauli hii ya JK kwa mawaziri wezi sijaielewa?

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,115
Jana wakati anatangaza baraza jipya Rais kikwete alinihuzunisha sana!
Katika kuonyesha hakuna kitakachofuata kwa wapendwa wezi alisema hv;
Mnawajibishwa kisiasa hata kama hamjatenda nyie ! Sasa tunaenda kwa waliosababisha mfike hapa!
Je wanajamvi kwa kauli hii mnategemea lolote zaid ya kuwapa ulaji sehem zingine?
 
Hii ni bongo bana,umeshawahi ona wapi binadamu hana kichwa lakin anatembea cha kùshangaza ni kiongozi tena wa juu kabisa,hayo maajabu yanapatikana tz pekee
 
Jana wakati anatangaza baraza jipya Rais kikwete alinihuzunisha sana!
Katika kuonyesha hakuna kitakachofuata kwa wapendwa wezi alisema hv;
Mnawajibishwa kisiasa hata kama hamjatenda nyie ! Sasa tunaenda kwa waliosababisha mfike hapa!
Je wanajamvi kwa kauli hii mnategemea lolote zaid ya kuwapa ulaji sehem zingine?

..tafuta mtu akueleweshe mkuu,hiyo ni awamu ya kwanza
 
Anachomaanisha ni kwamba kweli Nundu na kina Mkullo hawajakosea wao. Lakini basi tuu mmepiga kelele nifanyeje sasa!
 
Father kauli ya JK iko wazi, wenye vyeo ni wanamtandao, wapwa zake, maswahiba na mabibi zake hivyo aliogopa kuondolewa Ikulu akawaengua na hii ni kwa muda tu, kwa udhaifu wake hapo ndo kamaliza maana watendaji wa mashirika na wakurugenzi wa mawizara ndo wanaomtajirisha Rizwan, hana zaidi JK na Rizwan ni compuni moja.
 
'Mnawajibishwa kisiasa hata kama hamjatenda nyie ! Sasa tunaenda kwa waliosababisha mfike hapa'!

Colleagues,

Maneno ya mh hapo (in quotes) yana maana nyingi kwa Wa-Tanzania. We deeply need to think about it. Ni wazavyo mimi (and likely to be true) ni:
1) Kwa utashi, uwezo na akili ya mh hakupenda kufanya hivyo (kuwawajibisha wezi). Hii ni kwa sababu hata watuhumiwa wengine kama hao (refer mjadala wa bunge lililopita kuhusu Katibu wa wizara ya nishati na madini, Mkurugenzi-TRA... mh hakuchukua hatua zinazostahili. 2) naungana na mtoa mada hapo juu kuwa hakuna hatua nyingine zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya waliowajibishwa zaidi ya kuwatafutia nafasi nyingine za uraji serikalini. Hii ni mbaya sana (baada ya ukwapuzi wa mamilioni ya walipa kodi-mtu anawajishwa kisiasa and that is all!). Kwa nini mh hafikiri jinsi ya kurudisha fadha hizo za watanzania? Kwanini kauli yake hiyo ije sasa na sikabla ya hapo? Hakujua kuwa mhusika yeyote (regardless his/her expertism in the ministry) anapaswa kuchuliwa hatua sitahiki endapo kuna tuhuma za wizi ktk wizara husika?.

My Take: Yamkini kwa hasira hiyo linalofuata ni ulipizaji visasi. Kurudishwa kwa fedha zote zilizoibwa itapendeza zaidi (I advise Mh. to do so otherwise hata hawa walioingia wanaweza kurudia makosa hayo hayo (maana kuwajibishwa kisiasa ni faida( fedha zote zinabaki kwa mhajibishwaji)
 
Mheshimiwa balozi massinda huko uliko canada jiandae tu kurudi Bongo au kuhamishiwa Burundi nk. Mheshimiwa Ngeleja yuko njiani kuja kuchukua ubalozi. hii ni kwa uhusiano wake mzuri na makampuni ya madini yenye asili yake Canada, Australia nk. Mheshimiwa Ngeleja hakufanya lolote baya pale wizarani kwake. Amewajibishwa tu kisiasa!!!!
 
Jana wakati anatangaza baraza jipya Rais kikwete alinihuzunisha sana!
Katika kuonyesha hakuna kitakachofuata kwa wapendwa wezi alisema hv;
Mnawajibishwa kisiasa hata kama hamjatenda nyie ! Sasa tunaenda kwa waliosababisha mfike hapa!
Je wanajamvi kwa kauli hii mnategemea lolote zaid ya kuwapa ulaji sehem zingine?
Duuh ulikuwa unatarajia kitu tofauti na hicho..............:rain::blah::msela::peace:
 
Back
Top Bottom