Kauli hii ya ccm imekwenda wapi??......!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli hii ya ccm imekwenda wapi??......!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Sep 18, 2010.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Katika kipindi hiki ambacho nchi yetu inaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na madiwani ni wazi kwamba masikio,macho na mawazo mengi ya watanzania yameelekezwa kwa wagombea hasa katika kunadi sera zao na za ilani ya vyama vyao ili waweze kuchagua kwa usahihi viongozi wa aina gani ambao wanapaswa kuilekeza nchi yetu katika ile bahari isiyo na mawimbi na maji yake daima ni matulivu yaliyojaa samaki wakubwa na wadogo walio katika hadhi ya aina moja na si kama ilivyo katika mapapa na manyanguni ambao mara nyingi ukubwa wao unawafanya kuwaonea na kuwatafuna wale wadogo, nchi ambayo ni zaidi ya ile imwagayo maziwa na asali.

  Itakumbukwa wazi kwamba katika kampeni zile za mwaka 2005, vyama hivi ambavyo kwa mara nyingine tena vinajitokeza hadharani kunadi sera zao ambazo wanadhani kuwa kwa namna moja au nyingine basi zinakidhi mahitaji ya watanzania, ni kipindi hicho CCM kwamba ilimteua kwa mara ya kwanza mgombea uraisi Jakaya Mrisho Kikwete aendeshe gurudumu hili la taifa kwa kupewa ahadi kemkem ikiongozwa na kauli mbiu yake isemayo KASI MPYA, NGUVU MPYA, ARI MPYA...huku akienda mbali zaidi kuahidi MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.....

  Na kuanzia hapa ndipo nionapopata mashaka yaliyoyajaa huzuni moyoni na kusema kwamba hawa CCM ni MAVUVUZELA yanayounguruma ndani ya mtungi yakidhani makelele yake yanaathiri na kuwanyima usingiziwatengenezaji. Hivi majuzi tulimsikia Kampeni meneja wa CCM Abduraham Kinana akisema mbele ya wahandishi wa habari kwamba wamekaa na wataalam wao ndani ya chama kama si serikali wakaichambua HOJA ya CHADEMA ya gharama za kusomesha na gharama za matibabu bure, kwamba kwa hili CHADEMA ni feki, kuwarubuni wananchi na halitekelezeki, wakaenda mbali zaidi wakasema hili swala litaimeza bajet nzima ya nchi yetu.

  Hali hii ni sawa na kusema kuwa utapaka vipi makapeni kwenye shati la mwenzako kwa kujua kuwa unamchafua bila kuzingatia upande wa pili kwamba yawezekana ukawa unalipendezesha? Kama nyie mlikuja na kampeni za MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA (kauli ambayo leo hii ni sumu kwa kiongozi yeyote wa CCM kuitamka hadharani), je mlikaa vikao vyenu mkatathmini kwamba maisha bora yatakuja kwa kila mtanzania ndani ya miaka mitano? Je hayo maisha bora ndio kwa viongozi na kina mama salma kutembea na maV-8? Hayo maisha bora ndio haya ambayo mzee alitamka kwamba ni mikusanyiko na mirundikano ya magari mabarabarani? Je haya ndio maisha bora ya watanzania kuokota na kubeba mifuko mikubwa iliyojaa makopo na vyuma chakavu? Ndio maisha haya ambayo vijana wengi wamejiajiri mtaani kwa kuuza sumu ya panya,mende,kunguni nk?. Naomba mtuambie kwanini hii kauli ya maisha bora kwa kila mtanzania hamuitumii sasa katika makampeni yenu?
  Nimesikitishwa zaidi pale ambapo CCM iliahidi ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania na ndio iliyowafikisha ikulu huku wakijua wazi kuwa hawawezi kuyaweka haya kwa unyumbuaji halisi, sasa inakuwaje hawa CCM wakasema kwamba CHADEMA HAWAWEZI KUGHARAMIA ELIMU NA MATIBABU BURE wakati tayari wameshaainisha ni kwa namna gani wataiwezesha hii kitu, je na hao CUF walioahidi elimu bure, kuongeza mishahara kwa wafanyakazi na kulipwa kila baada ya wiki mbili na MAALI SEIF kule Zanzibar ni kusema uzushi pia? Hivi inaingia akilini kwa watu wenye akili zao kurubuniwa kwa hili huku bara na Zanzibar?Je hii hamuoni kwamba CCM ni zaidi ya mavuvuzela kwa kupiga makelele ilani za wenzenu wakati zenu hazitekelezeki hata tuwape miaka mia?
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sema baba/bibi semaaaaaaaaaaaaaaa labda utaaminiwa wewe.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Akili mgando wakaamua kuongeza zaidi..zaidi..zaidi
   
 4. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Hawawezi kuitamka tena kwani wanaujua ukweli, maisha bora kwa wateule wachache na familia ya JK na si kila mtanzania!
   
 5. r

  rimbocho Member

  #5
  Sep 18, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo kauli haijathibitika kama inaukweli, kwani watanzania sasa hawadanganyiki.
  Mama Salma ndio attengenezewa uwanja wa ndege wa kisasa kule Mbeya na kwingine alikoahidi mumewe au kuna mtanzania gani anayeruka angani zaidi yake? wakati akishika chaki aliota kuruka angani? sasa hivi si ameshapata hayo maisha bora aliyo ahidiwa na mumewe? kwani umesahau uraisi ni wa familia- pia maisha bora ni kwa familia
  Raisi wa Tanzania= Raisi wa familia
   
 6. D

  Dopas JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Asante.
   
 7. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hakuna kulala mpaka kieleweke
   
 8. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hawa CCM wanajua tu kuchakachua Ilani ya Chadema kwamba Darasa la Kwanza hadi form six free HAIWEZEKANI... Mbona Prof Lipumba kaenda Mbali zaidi na kusema itakuwa free mpaka university... mbona yeye haulizwi...

  ukiona vyama viwili vinasema kwamba inawezekana kusomesha watoto darasa la kwanza walau mpaka form six free.. ujue ni jambo linalowezekana na CCM hawajatoa takwimu kutuonesha kwamba ni kivipi haliwezekani... naomba ccm waamuzile basi Prof Lipumba achanganue maana sijasikia wakimkana...
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,671
  Likes Received: 21,902
  Trophy Points: 280
  CCM is a walking corpse!
   
 10. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Mnayosema ni kweli kabisa CCM wameishiwa hoja, na ni dhahiri nchi imewashinda, hofu yangu ni kuwa hawa jamaa ni hodari wa wizi wa kura kutokana na mfumo uliopo unavyowawezesha kufanya hujuma zao kama vile Tume ya uchaguzi inayowajibika kwa rais ambaye nae ni mgombea, hivi jamani tufanyeje? Mi naumia sana moyo kwa sababu najua wanaiba kura zetu.
   
Loading...