Katuni ya Mwanahalisi na Hatima ya Magazeti Yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katuni ya Mwanahalisi na Hatima ya Magazeti Yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GreatConqueror, Jun 8, 2009.

 1. GreatConqueror

  GreatConqueror Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jumatano iliyopita tarehe 3 June nilinunua kama kawaida yangu gazeti la Mwanahalisi nilichokutana nacho kwenye page ya Katuni sikuamini macho yangu manake nilihisi labda ze utamu wameanzisha gazeti na nimelinunua bila kujitambua. Kwa kweli katuni ile mimi binafsi sikuilewa mantiki ya kuwekwa kwenye gazeti linaloheshimika kama hilo.

  Hivi mchora katuni huyu na mhariri wake hawakuwa na njia mbadala ya kuonyeshwa kukerwa na safari za nje za Rais zaidi ya kumdhalilisha kiasi hiki? Hebu fikiria unasoma gazeti then mtoto anakuuliza hii katuni ina maana gani na huyo aliyechorwa kabeba nini? (nguo za aibu kweli kweli!!).

  Jumanne June 2 katika gazeti la Sauti Huru ilitoka makala yenye kichwa "TUMSILIKILIZE MWAKYEMBE KISHA TUMPUUZE". Ndani ya hiyo makala kulikuwa na paragraph inayodai

  "Kwa nini Mwakyembe anataka kutufanya watu wote WAPUMBAVU?
  Yaani kulala Ifunda ndio iwe sababu ya kutokulala kwenye gari?
  Hii ni aina fulani ya UTAAHIRA".

  Huyu mwandishi naye na mhariri wake hawakuwa na njia mbadala ya kuonyesha "HASIRA" zao kwa tamko la Mwakyembe kuhusu ajali yake? Tunajua kuna baadhi ya magazeti yameanzishwa ili kupambana na watu fulani, lakini tunaomba ziwe zinatumika lugha za staha kwani magazeti husomwa na watu wa rika zote!

  Wanahabari mnatupeleka wapi?

  Naomba kutoa hoja  [​IMG][​IMG]
   

  Attached Files:

 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuhusu hiyo katuni mimi sijaona ubaya wake... labda tufafanulie zaidi. Ni hizo nguo za ndania au??
   
 3. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa upande wangu naona jamaa alikuwa sawa kabisa,maana amefananisha safari ya vasco da ***** kuwa ni safari ambayo haina manufaa kwa taifa,duh! weli prezida wetu watu wamemchoka,kumbe alikwenda kumnunulia wife kufuli na S***a mweh!
  mkuu asante sana kwa picha hii maana umenivunja mbavu.
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Lazima tuelewe kuwa kadiri tunavyoendelea, na kukuza demokrasia, uhuru wa kujieleza nao pia unakua.Uhuru wa kujieleza unaendana na ustaarabu.Mwingine anaweza kufikiri ustaarabu ni kutomchora rais vibaya, kwa kuendeleza kile Jaji Warioba alichokiita "rais ni alama ya taifa".Lakini wengine tutapinga vikali na kusema watu wana uhuru wa kujieleza, ikiwa ni pamoja na kutoa maoni yaliyo tofauti na ya wengine -pamoja na kumkaragosi rais- ilimradi tu hawavunji sheria.

  Rais ni mtu na anaishi katika jamii yetu, hivyo anaweza kukosea.Anapokosea, waandishi wa habari pamoja na wachora katuni wana wajibu wa kuifikishia jamii ujumbe kuhusu maoni yao.Kilichofanyika hapa ni kuwakilisha maoni ya baadhi ya watanzania kuhusu safari za Kikwete.Inawezekana maoni haya yako sawa au hayako sawa, haisumbui kama yako sawa au hayako sawa ilmuradi hayajavunja sheria, kinachosumbua ni kuona kuna watu hawataki maoni yaliyo tofauti na yao yachapishwe.

  Kwangu mimi, ukiachilia mbali maudhui ya kikatuni -kwamba kiko sawa au si sawa- kikatuni hiki kamwe hakimvunjii heshima rais, bali kinamuongezea heshima na kumfanya aonekane bingwa wa demokrasia ambaye anaweza kufungia gazeti kwa sababu nyingi tu lakini hajachagua kufanya hivyo kwa kuelewa umuhimu wa demokrasia na uhuru wa kujieleza.
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mimi binafsi sikuona ubaya wowote kwenye ile cartoon ya Mwanahalisi; kwa uelewa wangu cartoon ile ilikuwa na ujumbe kuwa safari za muungwana hazina tija kwa wadanganyika ila pengine kwa familia yake!! Sikuona kitu chochote cha kulidhalisha gazeti la Mwanahalisi. Ulikuwa ujumbe sawia!
   
Loading...