Katuni katika historia na heshima ya wachora katuni

Isack inno B

Member
Oct 28, 2012
97
51
Na

Dr. Christopher Cyrilo
Utamaduni wa kuweka picha ya mtu kwenye pesa za noti au sarafu umekuwapo tangu kale. Historia inaonesha kuwa mtawala wa zamani wa dola la Rumi, aliyekuwa pia jemedari imara wa vita, mwanasiasa nguli na muhamasishaji haswa, Gaius Julius Caesar, ndiye binadamu wa kwanza aliyepata heshima ya picha yake kuwekwa kwenye sarafu ya dola la Rumi. Unaweza kustaajabu kwamba, sarafu hiyo ya Rumi ya kale, iliitwa "Shilling". Caesar, pamoja na sifa nzuri, pia alikuwa na sifa hasi. Alikuwa dikteta. Pengine tabia ya uonevu na ukatili ndio vilipelekea kuuawa mikononi mwa kundi la uasi liloongozwa na Gaius Cassius Longinus, Marcus Junius Brutus na Decimus Junius Brutus. Historia haitambui hasa nani aliyemuua Caesar kati ya hao watatu.
Baada ya kifo chake, Caesar alitawazwa kuwa Mungu wa nguvu (God of strength) na kuweka rekodi ya Mrumi wa kwanza kupata cheo hiko cha Umungu. Pia, kwa heshima yake, mwezi wa Quintilis ulibadilishwa jina na kuitwa kwa jina lake la kati la Julius au July (mwezi wa saba) kama tunavyouita leo. Jina lake la mwisho la Caesar (kaisari) lilitumiwa kama cheo kwa watawala wengine waliofuata; wakaitwa makaisari. Na kama ilivyo katika mambo mengi ya Rumi, mabaki ya historia ya dola hilo yameendelea kugandamana na tamaduni zetu za kileo, aghalabu katika mambo mengi.
Moja kubwa kati ya mabaki ya historia ya Rumi ni kuweka picha za wakuu wa mataifa kwenye noti au sarafu za fedha. Hata hivyo, yupo mtu aliyevunja kanuni hiyo, si kwa hiari yake bali kwa upendeleo maalum; naye ni Benjamin Franklin.
Ukitazama noti ya dola mia moja ya marekani (USD 100) utaiona sura ya hekima ya Benjamin Franklin katikati ya noti hiyo maarufu kuliko zote duniani. Kumbe pamoja na utamaduni uliodumu tangu miaka 40-50 kabla ya kristu wa kuweka picha za wakuu wa dola kwenye sarafu au noti, lakini leo sarafu maarufu kuliko zote ulimwenguni ina picha ya mtu ambaye hakuwahi kuwa mkuu wa dola. Benjamin Franklin hakuwahi kuwa mkuu wa dola la Marekani. Kwa uchache tu, alikuwa mwandishi, mwanasayansi, mwanasiasa, mwanamapinduzi, mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, Mwanadiplomasia, Mwandishi, tajiri na mmiliki wa jarida la Pennsylvania; Jarida alilotumia kuchapisha katuni za kuhamaisisha mapambano dhidi ya ukoloni wa kiingereza huko Amerika ya Kaskazini.

JOIN OR DIE
Inaaminika kwamba katuni ya kwanza kuchapishwa kwenye jarida, ni katuni iliyopewa jina Join or die (jiunge au ufe) iliyochorwa na Benjamin Franklin. Katuni hiyo ilionesha nyoka aliyekatwa vipande vipande, huku vipande hivyo vikipewa majina ya baadhi ya majimbo yaliokuwa chini ya ukoloni. Taswira ya nyoka alaiyekatwa vipande iliakisi imani za kimila za watu wa huko marekani. Ni imani ileile iliyozagaa hadi Africa, kwamba eti Nyoka aliyekatwa vipande anaweza kujiunga kabla jua alijazama na kuendelea kuishi. Kwa hiyo, Benjamin aliweka ujumbe huo, kuonesha kwamba jamii ya wamarekani imevunjwa vunjwa na hivyo inawapasa kuungana mapema kabla hawajakufa kabisa. Katuni hiyo na nyingine zilichangia sana kuhamasisha vita dhidi ya ukoloni wa kiingereza. Benjamin, alitunia jarida lake la Pennsylvania gazette kuchapisha makala na katuni za kuudhi wakoloni, na wakati mwingine kueneza propaganda dhidi ya ukoloni.
Kwa hivyo pamoja na mambo mengi makubwa aliyofanga Benjamin, mojawapo ni kutumia katuni katika kuleta uhuru wa wamarekani, na kwa heshima yake, picha yake inapamba sarafu maarufu kuliko zote duniani. Sarafu hiyo ya Dola 100 pia hutambulika kwa 'nick name' ya "The Benjamin" au "The Franklin". Anatajwa kuwa moja ya waanzilishi wa Taifa la Marekeni, na yeye ndiye aliyetia saini azimio la uhuru (declaration of Independence) wa marekani. Pia alishiriki kikamilifu katika kuunda katiba ya Marekani akishirikiana na akina George Washington, Baba wa Taifa la Marekani. Kuna msemo wa utani huko marekani, unaosema "Benjamin ndiye Rais pekee wa Marekani ambaye hakuwahi kuwa Rais wa marekani".

Katuni zenye mfano wa mtu.

Kwanza, unapoita kitu katuni au kikaragosi maana yake sio kitu halisi. Ni maelezo ya picha na maandishi ambayo kila mtu anaweza kutafsiri anavyoona yeye. Katuni kamwe haioneshi sura ya mtu. Hakuna mtu anayefanana na katuni duniani, au ikitokea basi sio jambo la kawaida. Inaruhusiwa kuhisi kuwa 'huyu aliyechorwa ni mimi' lakini kuonesha hisia hizo waziwazi, ni upungufu wa akili. Kujifananisha na katuni ni kumkosoa Mungu akiyekuumba. Ndio maana hakuna sheria itakayomtia hatiani mchora katuni.

Tanzania, kama zilivyo nchi nyingi za kidemokrasia ni nchi ambayo misuguano ya kimawazo haitaisha, ali mradi tuna uhuru wa kufikiri na kusema. Katika uhuru huo, haitarajiwi hata kidogo tukafikiri sawa. Na jamii ambayo kila mtu anafikiri kama mwingine ni jamii isiyofikiri.
Katuni ni moja ya njia bora ya kuanika fikra zetu. Ziwe fikra kinzani, au fikra za kuunga mkono, au fikra zisizo na mlengo wowote, ali maradi ziwe fikra huru. Itakuwa bahati mbaya sana kupeleka nyaraka za vikatuni mbele ya vyombo vya sheria.

Itoshe kukubaliana kwamba, Hata kama itatafsiriwa kwa namna gani, katuni kamwe haiwezi kuwa kitu halisi. Wala haiwezi kukusanywa kama ushahidi (evidence) wa kumtia mtu hatiani. Labda tu, utamaduni wa watu wasiojulikana uendelee. Lakini katika dunia ya wafikirifu, sio kitu cha kuhangaika nacho.
Hata hivyo, katuni zina ujumbe maridhawa, na matokeo yake makubwa yameonekana katika historia mbalimbali tena katika mataifa makubwa. Kwa hiyo, nichukue nafasi hii kiwatia moyo wachora katuni wote, bila kujali itikadi zao. Hakuna hatia katika kuchora katuni, bali kuna matokeo makubwa kupitia katuni. Jamii inafurahi, inajifunza, inakumbuka, inahamasika na kujitambua.
Tuendelee kuwachora, kama Benjamin alivyowachora. Pengine Marekani ingechelewa kupata uhuru kama sio katuni za Banjamin. Tuwachore tu! sio sura zao, sio maumbile yao, sio macho yao, sio vichwa vyao, sio matumbo yao, ila tuwachore. Werevu watajifunza, wengine watapaniki; wendawazimu.
 

Attachments

  • 26169155_1726248287440401_6579225024914050684_n.jpg
    26169155_1726248287440401_6579225024914050684_n.jpg
    28.3 KB · Views: 74
Iyo Picha ya join or die mbona kama nahisi jambo ivii...

Kwenye series ya sleep hollow kuna kipande wameonyesha na kwa ujumla ilihusiana na mambo ya freemason
 
"katuni kamwe haioneshi sura ya mtu";


ila hapa kwetu kuna mchora katuni akimchora jamaa fulani inakuwa sio tena katuni, ni sura harisi ya jamaa.
 
Nakusahihisha tu Gaius Julius Caesar hakuwa dikteta wa mabavu kipindi chao dikteta ulikua unapewa kwa kipindi fulani ndani ya uongozi wako!..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom