mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,610
- 1,601
Idhaa ya habar ya ujerumani DW imepost hii katuni ya Rais wetu John Pombe Magufuli kama nae anajipu kichwani.
Watanzania tunatakiwa tuungane kwa nguvu ili kupinga hizi hujuma zinazofanywa na watu tofauti kama hawa wanazofanya kwa Rais wetu ambae ameonesha nia ya kulikomboa hili taifa lililoharibiwa vibaya na wahuni.
Inasemekana na inasikitisha kusikia aliechora hii katuni ni mtanzania anaeitwa Gado aliyefukuzwa kazi Nation Media ya Kenya ndio anaetumiwa na vyombo vya magharibi kama DW ya ujerumani.
Na ikumbukwe kuwa ujerumani alikuwa anaunga mkono upinzani kwenye uchaguzi wa 2015.
Naomba watanzania tuungane pamoja kupinga vitu kama hivi vinavyomdhalilisha Rais wetu alieonesha nia ya kuwasaidia nchi yake.
Naomba TCRA mchunguze mambo kama haya na muangalie Sheria za Uhuru wa mitandao zinasemaje kwenye mambo kama haya ili wahusika wawajibishwe kwa hujuma na matusi kama haya kwa Watanzania.