Katoro Na Tunduma, Saa 12 Asubuhi Ugali na Nyama Choma Inakua Tayari Kwingine huko Vipi?

Njia nyingi kubwa za malori kwenye miji mikubwa huu utaratibu mboona kawaida sana,last week nilipiga ugali pale singapore(singida) asubuhi..

Njia ya Dar, Lindi, Mnazi mmoja, masasi, kwenda tunduru kupita kilimasere, hadi namtumbo, songea hadi mbinga hawana huo utaratibu kabisa utanusanusa nangulukuru kwingine usishangae ukakuta giza tupu
 
Jmosi hii nilikula ugali nyama choma na kichuri hapa Banana dsm. Maeneo ya Gmboto, kitunda na ukanda huo kwa dsm ugali nyama choma na kichuri ni mapema asbh kabisa. Sababu wakurya wengi wanaishi maeneo hayo
 
Mbwembwe tuu. Mtu unakaa kwenye kiti umening'iniza poumbou mkono huko usukani kila baada ya kilomita 10 unasimama kwa mama ntlie kula na kupiga umbea na madereva wenzako iyo unaita kazi? Kuna wanaume wako kazini shambani na migodini hawaendekezi msosi na kulakula hovyo hovyo ni kazi kwenda mbele.
Dogo nitumie namba yako PM nikutumie muamala wa supu, naona unastress sana
 
Dogo nitumie namba yako PM nikutumie muamala wa supu, naona unastress sana

Achana nae anasema madreva sio kazi nzito hajui hapa kuna Baba zake walianza kukokota Fiat 682 , hapo hakuna maji ya dasani au kilimanjaro ni mwendo wa vidumu tu maji ya kunywa hayo hayo yanatiwa kwenye radiator, ukikaribia kijijini ile poooopoooopoooo hadi mwenyekiti wa kijiji anasogea barabarani kukupungia mkono, hapo unasugua kiganja kwenye gearlever hadi kinawasha inabidi uchukue shati liwe kama gloves ndio upige gia hapo miaka kadhaa nyuma umetoka kugonga bedford na injection ya bluu, mvua yako, jua lako , anadhani watu wote walianza kurndesha auto gear truck tena wakiwa wamechomekea, msamehe bure.
 
Back
Top Bottom