Katikati ya tanzania inadharaulika

Original Pastor

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
1,274
50
Siku moja nilikuwa nasafiri kwenda Singida sasa nikapita kijiji kimoja abiria mwenzangu nilikuwa nimekaa nae akaniuonyesha katikati ya Tanzania Kule Dodoma na nikapaona ila mazingira DU! yanachekesha sana kwani hiyo mark iliwekwa enzi za utumwa na ni mark kama "inch "16" tu yaani inashangaza tena kustaajabisha kwani nasikia hata mkuu wa nchi mstaafu aliwahi kwenda pale kukaa barabarani na kupiga picha (kama wadau wanayo iwekeni tumjadili) kwani ilitakiwa kujengwe Bonge la Mnara wa kuonyesha kweli ni Centa ya Tanzania kuliko kukaa hivi tena utakuta wabunge wengi hawajua au wanafanya kusudi pamoja na waziri wao wanafanya makusudi kwani hata kamati ya bunge kuhusu mambo ya mazingira wapo kimya.Je mkuu wa wilaya? Mkuu wa Mkoa? eti sisi abiria ndio tuone.Tena narudi kutoka Singida mtu mmoja akaniambia Hembu ona katikati ya Tanzania tunapadharau kwani panahitaji changamoto ili tuweke mnara. nikasema Du! kumbe kuna watu wanaongea lakini hawajui pa kuongelea kwani mtu anasema mimi nimeshafika mpaka pale ukipanda juu utaona kweli ni tanzania. akaniomba kama naweza kuzungumza sehemu nyingine niende lakini mimi nikamwambia kuna web inaitwa jamiiforums wewe nenda kafungue uelezee kuna wadau watachangia mada hii sasa nimeona jamaa si muelewa sana wa computer nimeona mimi niwafikishie wadau wenzangu ili nanyi muweze kuelewa nini au kitu gani Tanzania kinaendelea kwani kuna mabo mengi yamesahaulika. kwa mfano Zanzibar wao wanarekebisha mambo yote ya kale ndio maana wazungu wanakwenda kuangalia na sisi kwa hili pia wazungu wangeenda kuangalia pato la Taifa lingekuwa hata sisi Wadanganyika tungekuwa updated kuliko ukimya.mfano mtoto wako au wangu atajua Tanzania katikati ni wapi?
 
Elezea vizuri watu waelewe ili wachangie; unajaribu kusema nini?
 
ndugu unataka kuzungumzia nini hasa sababu umejikanyaga sana lakini kwa kukusaidia kuna changamoto nyingi zinazo wakabili watanzania kwa sasa hili la katitati ya Tanzania nakuomba ukalijadili kwenye vikao vya kahawa jioni hapa umepotea
 
ok msijali hii ni changamoto tu kwani na maanisha hii sehemu ingekuwa vyema serikali ingejenga hata mnara ili ionyeshe maana ndio makumbusho hayo ili mimi wewe tuvutiwe kwenda hata hapo centa. haya ni makumbusho yaliosahaulika ambayo katika vitabu vya wakoloni waliandika sana na iliweka mark hiyo ni mreno wa kwanza mwaka 1847 je kwanini yawe kimya???
 
angalia hata barabara zinajengwa huku huku pwani tu. mimi sijatoka western africa, maeneo nitokayo hayana shida kabisa ya usafiri. lakini huwa nashindwa kuelewa, kwanini western tz na maeneo ya north west yanadharaulika? Kigoma, central tz(singida,shinyanga etc), kagera,rukwa nk. pamoja na kusini. kama sio tz vile, cha ajabu, hata bajeti hutungwa kuwabagua watu wa huko. pamoja na kwamba maeneo yao yana resources nyingi ambazo kama tungekuwa makini kuweka pesa nyingi kwenye infrastructures huko, tungepiga hatua kuvuna utajiri wa huko. barabara mbovu pamoja na kwamba zingine zinapakana na nchi jirani ambao wangekuwa wateja wetu, reli ndo tumeuza kwa wahindi. bandari ya mtwara ingekuwa bomba, lakini wizi mtupu. nashindwa nisemeje kwakweli.
 
Back
Top Bottom