"Katika Utawala Wangu..."

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Guys... Who is legal advisor wa Rais Magufuli? Au advisor wa namna yeyote ile?

Hii ziara ya Pwani yametokea matamko ya Rais ya kusema "katika utawala wangu" but kwangu naona hakuna jitihada kuweka mfumo, kanuni Na Sheria Imara zinazoeleweka ili uwajibikaji uwe ni kitu Na tunu ya kawaida si mfumo w utegemezi wa kiongozi mkuu wa nchi au hamasa yake kuongoza Na "kunyoosha" Taifa!

JPM alipokujaa alishangaa kukuta madudu na machafu kupindukia, sababu yawezekana sana kuwa JK naye alisema "katika utawala wangu" akajifanyia mambo Na maamuzi mengi ambayo Magufuli anayashangaa.

Labda naye Kikwete alikuta aliyoyarithi ambayo yalifanywa kwa mantiki ya "katika utawala wangu.." iwe ni Serikalini au hata katika Chama.

Leo Magufuli anaongoza nchi na kufanya kila kitu kwa kigezo cha "katika utawala wangu"

Kesho akiondoka Magufuli, atakayekuja naye atasema "katika utawala wangu" na kubadilisha Yale yaliyofanya "katika utawala wangu" wa Magufuli !

Now nikiangalia kwa nini kuna non-responsive kutoka taasisi, mashirika, Serikali, watendaji Na hata wananchi, jibu lake ni kila mtu anajua "katika utawala wangu" utapita Na kuna expiry date Na si mfumo unaoeleweka kisheria... Wanapuuzia wanajua wakisema "ametukuta, ataondoka, atatuacha"!

Nchi imekuwa ikiendeshwa au kuongozwa na maamuzi kufanywa kwa dhana na fikra za "katika utawala wangu.." kuanzia Rais mpaka Mkuu wa Wilaya au hata mwenyekiti wa kijiji kupuuzia kabisa mipaka ya kisheria, mamlaka,kanuni hata katiba.

Zaidi, dhana hii ya "Katika utawala wangu.." si kwamba imekwamisha maendeleo ya jamii na Taifa, lakini hata imepunguza uwajibikaji wa kweli, kujenga kiburi nauungwana wa kukiri makosa, kujikosoa au kujisahihisha kunakosekana.

Mfano inawezekana DC wa Hai juzi akivunjavunja shamba la Mbowe alitumia kigezo hicho cha "katika utawala wangu.." au leo Mkuu wa TRA Arusha anaposema ukikutwa huna risiti fainielfu thelathini, naye anatumia nguvu ya "katika utawala wangu".

Keshoanapokuja mtendaji au kiongozi mwingine naye akasema "katika utawala wangu" (mfano mzuri ni Nape na Mwakyembe wizara ya habari) naye akaamua kusema anabadilisha na kufuta kila kilichofanywa na aliyemtangulia kwa kuwa "katika utawala wangu" haoni manufaa.

Kuna tofauti ya kufanya mambo "katika utawala wangu" kama mambo hayo hayahusu kanuni, sheria, taratibu, katiba au maamuzi yenye impact kubwa kwa jamii na Serikali.

Ni haki kusema "katika utawala wangu" uvivu,uzembe, ubabaishaji, uchelewaji, umangimeza, uhujumu nu mwiko na kamwe hautavumiliwa. Lakini kuna haja ya kuweka na kurejea misingi iliyopo na kuhoji kwa nini utovu wa nidhamu upo na au unaongezeka!

Leo Rais Magufuli kawasema Brela mpaka kutoa tamko (presidential executive order) verbally kuwa wenye nia ya kuanzisha viwanda au biashara wasisubiri Brela, waanze mchakato maana Brela wanajivutavuta na kupunguza kasi ya maendeleo na azma ya viwanda ya awamu ya tano. Najiuliza je kwa nini Brela leo ni miezi 20 tangu awamu ya Tano iingie madarakani bado inajivutavuta na kuwa na umangimeza au ukiritimba ambao unakwamisha ufanisi? je hawana kanuni za uwajibikaji? au usimamizi wa kanuni za uwajibikaji na majukumu zina mapengo na mianya ya uzembe, uhujumu au hata kulea rushwa na kero?

Je yawezekana huko Brela hakuna hizi kanuni kwa kuwa kila mkubwa wa sehemu anafanya mambo ya "katika utawala wangu" na kujiamulia mambo na wafanyakazi wa chini kwa kukosa mfumo unaoeleweka na kushuhudia kwao wakubwa wakifanya mambo kwa itikadi ya "katika utawala wangu" basi wanajijengea kiburi cha "alitukuta, atapita, atatuacha hapahapa"?

May be tukiongelea mambo kwa mtazamo huu, ubishi na ushabiki unaopinga kujengwa kwa mfumo huru Imara kuanzia Katiba, Sheria na Kanuni hata uwajibikaji wake utaangalia mambo kiuhalisia Na si kushangilia current happenings ambazo "baada ya utawala wangu" tutarudi kule kule au atakuja mwingine na mtazamo wake na kusema "katika utawala wangu"?
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,179
2,000
Mkuu Rev

Niliwahi kushangaa India ilipokaa zaidi ya miezi mitatu bila Waziri mkuu
Uingereza ilikaa wiki tatu bila ya Waziri mkuu

Na mifano ipo mingi ya namna hiyo.
Nilichokibaini watawala wana na sera kwa wakati uliopo , miongozo ya Taifa haibadiliki.

Hii inaonyesha uwepo wa taasisi ambazo hufanya kazi bila kujali nani yupo madarakani

Katika nchi yetu hakuna miongozo ya namna hiyo. Tukianza na katiba ambayo nguvu yake kama chombo cha kusimamia thamani na mwongozo wa nchi haionekani.

Katiba inatumika watawala watakapohitaji kutekeleza matakwa yao na si vinginavyo

Ni kwa mtazamo huo neno 'utawala wangu' lina maana, kwamba, kipindi fulani Taifa linazimika kufuata maelekezo ya watu walioko madarakani na si utaratibu uliopo

Hoja hii inashadidiwa na kauli ya kiongozi mmoja aliyenukuliwa akisema ' ....nchi itayumba ni watu hatari sana'' .

Tunakumbuka Waziri mkuu alipojiuzulu Rais alisema ' Nchi imeyumba kwa tukio hilo''

Kwamba, nchi inayumba kwa mtu kujiuzulu ni dalili nchi inaongozwa na mtu na si taasisi. Haiwezekani nchi yenye taasisi kamili ikayumba kwa mtu mmoja kutokuwepo

Nikiangalia nchi kama Japan, katika kipindi cha miaka 10 wamekuwa na mawaziri wakuu ambao ndio viongozi wa serikali na nchi zaidi ya 5.

Hili linawezekana kwasababu mifumo inafanya kazi na watumishi huitumikia

Taasisi kama BRELA ni mfano mzuri wa hoja. Haiwezekani kuwalaumu kwa kujivuta vuta ikiwa inasimamiwa na serikali. Je, aliyeshindwa ni Brela au serikali ?

Mfumo tunaosema ni mbaya ni huu wa exec order, kwasababu baada ya muda Rais ana majukumu mengine na azma ya viwanda haitafanikiwa.

Kutofanikiwa ni kwasababu Brela watafanya kazi kwa woga na si ubunifu 'innovations'

Kinachotakiwa ni kuimarisha taasisi zifanye kazi kwa kufuata miongozo iliyopo
Yanapotokea mabadiliko ya viongozi taasisi zinasimama zenyewe imara

Kazi ya serikali nikusimamia taasisi zifanye 'delivery' kutokana na sera zilizopo

Sera kama ya viwanda ni kubwa inahitaji maandalizi, kuwalaumu ni kuwatwisha mzigo

Miaka miwili iliyopita tulikuwa na sera ya kilimo kwanza.
Brela walikuwa katika mtazamo huo, ghafla imekuja ya viwanda hawajui waanzie wapi

Hatuwezi kuwa na taasisi imara ikiwa zipo chini ya uongozi unaopaswa kuzisimamia

Jambo hili linazotesha sana ubunifu kwa taasisi kusubiri maelekezo na si kutenda

Ili kuziimarisha ni lazima tubadili mfumo mzima kwa kuangalia upya miongozo yetu

Kuzifumua taasisi kunakwenda sambamba na mabadiliko makubwa ya katiba ili kuziondoa katika mikono ya watu na kuzipa uhuru zikiwajibika kwa taasisi nyingine za juu
 

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,262
2,000
Nguruvi3 na rev kishoka kibaya zaidi miongoni mwa hawa viongozi wetu ni kwamba hawana common understanding.

Yaani hata wakiwa kwenye madaraka mamoja Bado kauli zao zinakinzana tu. Kukiwa na sera basi itakuwa ni ya wizara fulan ama kundi fulan na sio ya nchi mzima jambo ambalo linatishia utayari wetu katika kuleta maendeleo ya dhati

Sent from my Royale A1 using JamiiForums mobile app
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,940
2,000
Guys... Who is legal advisor wa Rais Magufuli? Au advisor wa namna yeyote ile?

Hii ziara ya Pwani yametokea matamko ya Rais ya kusema "katika utawala wangu" but kwangu naona hakuna jitihada kuweka mfumo, kanuni Na Sheria Imara zinazoeleweka ili uwajibikaji uwe ni kitu Na tunu ya kawaida si mfumo w utegemezi wa kiongozi mkuu wa nchi au hamasa yake kuongoza Na "kunyoosha" Taifa!

..."?

Mbona hivi vitu vya kawaida, hata mamtoni mambo mengine huenda kutegemea na nani kachaguliwa. Sasa Mayu unataka Mhe. Magu aende kama automaton kufuata maelekezo aliyoyakuta? Na ni nani basi atakeyekuwa na mamlaka ya kuaandaa hayo maelekezo ya kufuatwa na kila mtu ataekuwa Mhe. Rais?
 

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,262
2,000
Unajua katika vitu vinvyoshangaza ni hili swala la sisi kuendelea kukaa kimya tu pasi kunyanyua sauti zetu kinyume cha haya.

Wachache wanaojitahd kupaza sauti wanazimishwa na wakuu.

Kimenishangaza sana baada ya hata Lissu kulisema hili kwa sauti akakamatwa hakuna mwngine aliyejaribu zaidi ya mawakili tuu hao 20 waliojitokeza. Hakuna mwananchi ama kundi Fulani liki paza sauti. Sote tumekua waoga.

Lakin kwa kukaa kimya hivi ndio haya yanaendelea Leo atapanua uwanja tabora lkn alipoenda Kilimanjaro Kia hakuiona wakati ndio uwanja wa ndege wa kimataifa ambao unapokea ndege za kimataifa. What if akiupanua huu uwanja na ule wa arusha je??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
Mbona hivi vitu vya kawaida, hata mamtoni mambo mengine huenda kutegemea na nani kachaguliwa. Sasa Mayu unataka Mhe. Magu aende kama automaton kufuata maelekezo aliyoyakuta? Na ni nani basi atakeyekuwa na mamlaka ya kuaandaa hayo maelekezo ya kufuatwa na kila mtu ataekuwa Mhe. Rais?
I know you know better than this Mayu... Rais anakujaku-fit in what is already a national plan na kuna checks and balances za kutosha ambazo zinamlazimisha mgombea yeyote afanye refinment ya agenda na vision to the unified national plan navision.

Tanzania hakuna National Economic Planna vision ambayo ni huru bila kuwa na mikono na matakwa ya CCM.

Angalia how Katiba inasema nchi ni ya Kijamaa na misingi ni ya kijamaa. Then tunasema ttuna vyama vingi na chama Tawala kinapiga vita sera za kiuchumi za wengine, huku yenyewe kupitia safu za uongozi wake zinatumia na kuamini ubepari uchwara na kukimbilia kutumia hazina ya nchi kujijengea himaya zao za kiuchumi kwa kutumia dola kujihakikishia uhai.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom