Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,653
Maendeleo ya binadamu yamepiga hatua sana pale binadamu walipoamua kuishi pamoja.
Tatizo moja la kimsingi kabisa lililopelekea binadamu kuwa na serikali ni changamoto ambazo binadamu alikuwa anakumbana nazo. Kiu ya binadamu kubadilika na kutawala mazingira yake. Kwa jamii yeyote ile ingekuwa vigumu kupiga hatua ya kimaendeleo bila uongozi.
Kwahiyo binadamu walihitaji kiongozi ambaye angewaongoza kuwaonyesha nini cha kufanya na ni wakati gani. Ambaye angeleta order katika jamii na ku organize watu ili wajiletee maendeleo yao wenyewe.
Fukuto hili ndani ya binadamu la kuleta maendeleo, la kumbadilisha mtu kutoka katika uasili wake alioumbwa nao kuja katika High level of spiritual and intellectual capability. Binadamu tunayemuona sasa sio wa miaka elfu kumi iliyopita. Nguvu yake na uwezo wake umekuwa mkubwa mno. Kwa miaka mingi imekuwa ikiaminiwa kiongozi ndiye mshika ''maono'' ndiye anayejua Taifa lielekee wapi. Siongelei viongozi tulionao. Naongelea viongozi ambao intellectual capacity and moral insights zao ni za juu. Viongozi waleta mabadiliko.
Katika Taifa mabadiliko haya lazima yaanzishwe, this moral courage to transform our country to the better end.
Ni lazima tukumbuke wakati tukikimbizana na kuwa na utajiri wa mali. Tusisahau utajiri wa kiroho na utajiri wa kiakili. Tunahitaji vitu hivi viwili ni muhimu. Hatuwezi kusema sisi ni Taifa lilo endelea bila kuwa na ''morals'' na kuwa na raia wenye uwezo wa ku discern btn wrong and right na kufuata kilicho sahihi kwa nguvu zote.
Tunahitaji kuundwa harmonius society. Watu wetu wakiwa na afya nzuri ya kiakili na kiroho na wenye furaha. Kwahiyo ni lazima tuunde taifa lenye watu wenye furaha na kuridhika. Hii haitofanikiwa bila uongozi wa Haki. Hatutaweza kujenga Taifa hili katika mantiki ya kukandamizana na Taifa hili likaendelea kuwepo.
Uzuri wa Taifa lolote lile hujengwa na watu. Roho ya Taifa hili lazima ijengwe. Kama nilivyosema mahusiano yetu ni muhimu sana katika ujenzi wa Taifa hili. Hii ni kweli hata katika familia. Baba aliyejenga familia yake katika upendo na amani na ushirikiano ataipenda familia yake na kufurahia kuwepo nyumbani kwake na watoto watafurahia nyumba hiyo.
Swali la kujiuliza kwanini watu wana kuto kuridhika na kulalamika? Kutoweka kwa nguvu ya pamoja katika ujenzi wa Taifa hili chanzo chake ni nini? kutoweka kwa uzalendo ni nini chanzo chake? Katika maswali yote haya raia hawawezi kuwa ni Tatizo. Kuvunjika kwa familia huwezi kumlaumu mtoto kwa namna yeyote ile. Kiongozi imara huweka Taifa lake katika umoja. Huingiza msukumo kwa watu wake, Msukumo huu kutoka ndani kabisa ya raia wa Taifa lake kulisongesha Taifa mbele.
Katika tafakuri yangu nimegundua kuna serikali ya kibwanyenye Sio lazima iingie madarakani kwa kupindua hata serikali iliyoingia madarakani kwa kupindua inaweza kuwa bora kuliko ili iliyoingia kwa kuchaguliwa. Inaweza kuingia madarakani kwa ulaghai na uongo lakini ndani ya moyo wao kukawa hakuna nia ya dhati ya kuhudumia wananchi.
Serikali ya namna hii hupenda raha na wala haiwafikirii wananchi hata ikifanya jambo haifanyi kwa dhamira ya dhati ya moyo bali kutaka kuendelea kubaki madarakani, haiguswi na matatizo ya wananchi. Serikali ya namna hii huangalia mali na anasa. Haijengi kitu chochote katika ukamilifu wake kila kitu hujenga juu juu ili waje kuonyesha tumewafanyia hiki na hiki ili wapate kupata kura. Ni serikali ya kikandamizaji. Wananchi hawana uhuru wa dhati kutokana na njaa na magonjwa. majeshi ya ulinzi na yale ya polisi yanakuwa hayako kwaajili ya ku serve wananchi bali kuikundi kidogo cha watu serikalini.
Majeshi ya polisi ambayo yangetakiwa yawe huru kutumikia wananchi na sheria za nchi hutumiwa kukandamiza democrasia kwa maslahi ya serikali. Kwahiyo tutadanganyana kama tukisema tukichagua tu ndio tutakuwa Taifa la kidemocrasia bila ya kuondoa hizi elementi za serikali ya kibwanyenye na kuweka serikali huru inayotumikia raia kwa faida ya wote.
Hatuwezi kuendelea kuwa na viongozi wanaoamua wanavyotaka na wasiotumia maliasili ya nchi hii visivyo. Maliasili ya nchi hii lazima inufaishe watu wote. Na kodi za nchi hii lazima zitumiwe ipasavyo. Ni lazima tuunde Taifa ambalo viongozi wana heshimu mali za umma. Viongozi wanao tambua kwamba cheo ni dhamana.
Kwamba hakuna yeyote ambaye atakaye kuwa juu ya sheria. Bila mambo haya hatutaleta Order na maendeleo katika Taifa hili. Viongozi lazima wajue wao ni watumishi tu wa watu na wasinyanyue pembe zao. Serikali lazima iwe subjected to the people.
Watu lazima wawe na mamlaka dhidi ya serikali yao. Wana haki ya kimsingi ya kuiwajibisha serikali yao. Lazima serikali iheshimu raia, hili ni lazima lijengeke. Ni lazima tutengeneze nchi ambayo viongozi na wananchi ni kitu kimoja. Nchi yetu haiwezi kuendelea kuwa na serikali yenye mfumo wa kibwanyenye, watu wakiitumikia serikali badala ya serikali kuwatumikia wao. Ukandamizaji lazima uishe haraka sana. Wizi lazima uishe. Kuibia wananchi ni dhambi na ni usaliti.
Ni wakati sasa kwa nchi yetu kurudi katika dira. Ni wakati kwa nchi yetu kuona baadae yake. Ni wakati sasa kwa nchi yetu jua la asubuhi kuiimulikia. Ni lazima tujenge Taifa la watu huru na wenye matumaini. Hatuwezi kuendelea na ukandamizaji hili ni Taifa moja na watu wetu ni lazima wawe huru.
Kodi lazima itumike vizuri kwa maendeleo ya nchi na sio kuwa starehesha viongozi. Ni lazima tujenge Taifa hili katika maadili na uzalendo. Kuna watu vijijini wanahitaji msaada wetu, maendeleo hayawezi kuwa ya sehemu moja tu. Hatutaweza kujenga taifa wakati upande mmoja ukiendelea na mwingine ukichechemea. Kama ni matumaini ni lazima yajengwe kwa wote.
Tumekuwa Taifa la watu wabinafsi. Taifa la watu wenye malengo ya kibinafsi. Hatuwezi kuendelea kuishi hivi tuka jiita Taifa. Ni lazima tuwasomeshe watu kwa malengo ya kuleta mabadiliko katika Taifa na si vinginevyo.
Elimu yako lazima itumike kuwaelimisha wengine juu ya utaifa, jinsi ya kuishi na mambo mengine yatakayokuza uelewa wa watu wetu. Hatuwezi kuendesha Taifa hili bila elimu iliyo bora.
Ni lazima tujenge upya fikra za watu wetu. Fikra za watu za sasa hazitaweza kutufikisha mbele. Hii imeonyesha hivyo. Bila maadili hatutaweza kupiga hatua kama Taifa.
Elimu yetu lazima ijengwe katika misingi ya maadili na nidhamu.
Fikra za watu wetu ni kitu ambacho ni lazima tujenge wenyewe. Nchi hii haihitaji starehe. Inahitaji kutumia akili nyingi na juhudi nyingi ili tuondokane na umaskini, ujinga na maradhi. Hatuwezi kujenga Taifa letu katika umarekani. Hatuwezi kujenga wasichana wetu ku behave kama wakina Rihanna NO we are Noble people. Sisi ni Taifa ambalo ni lazima tutie juhudi kukua.
Ni lazima tujenge fikra za watu wetu kutafuta maarifa kuliko kitu chochote kile ulimwenguni hapo ndipo tutafanikiwa. Hatuwezi kuendelea kwa kugeza tabia za kipuuzi za wamarekani na kuacha zile za kimsingi walizo nazo hasa za kulipenda Taifa lao na za kutafuta maarifa. Ni lazima tujitegemee kiutamaduni na mbeleni ki technologia.
Kwa nini tushindwe kama tutaamua na kama tutakuwa wamoja na kuweka fikra zetu katika ujenzi wa Taifa hili?
Watu wetu ni lazima wawe wazalendo. Ni lazima tulilete Taifa pamoja. Ni lazima tuwe kama jeshi lililojikusanya kuvamia. Hii nguvu iko mikononi mwetu. Nguvu dhidi ya umaskini, maradhi na ujinga iko mikononi mwetu. Ni lazima tujipange kuishambulia kwa akili na jash .
Hii inahitaji utashi wa kisiasa tu na utayari wa kuchukua majukumu.
Juu ya yote pamoja na umaskini wote wa Afrika na watanzania. Waafrika tumekuwa watu wenye ku relax zaidi kuliko wamarekani na watu wa ulaya. Tusitegemee maendeleo yataletwa pasipo kufanya kazi. Ni lazima tufanye kazi na ni lazima tuwe na program makini ya maendeleo letu bila kazi maendeleo hakuna. Bila kutumia uwezo wetu wa kiakili maendeleo hakuna. Taifa hili tutalijenga sisi. Ubora na uzuri wa Taifa hili ni jukumu letu.
Naona kabisa Taifa hili lina uwezo wa kuendelea na kuwa kubwa Taitizo ni uongozi.Kama tuta plan Elimu yetu vizuri itakayomfanya mwanafunzi kuwa mwenye kufikiri, mwenye nidhamu na uzalendo tutapiga hatua fulani.
Lakini kiini cha matatizo yetu ni uongozi. Kiongozi ni lazima awe na maono. Ni lazima awe na skills za uongozi. Kuwaleta watu pamoja katika malengo mamoja na ku mantain Order. Hatutaweza kuendelea na nchi hii na viongozi wanaofanya ufisadi na kuiacha nchi peke yake.
Ni lazima tutambue tunapoelimisha watu wetu sio kusudi wapate mkate tu wa kula, wana majukumu kwa Taifa hili. Kuendelea kuwepo kwa Taifa hili kutawategemea wao. Kulilinda na kuliendeleza Taifa hili kutategemea sana akili za watu wetu. Busara na maarifa ya watu wetu ndiyo itakayopelekea kuendelea kuwepo kwa Taifa hili au kupotea.
Tuwakabidhi watoto wetu Taifa hili kama yai na tuwaambie walilinde kwa maarifa yote. Serikali ni lazima watambue ni lazima wajenge elimu iliyobora ili baadae ya Taifa hili iwe na nuru sio kufanya tu ili kutimiza ilani. Tutakosa watu wa kujenga Taifa hili au tutatengeneza matabaka ya wale waliosoma Nje ya nchi na wale wa ndani. Watawala na watawaliwa na matokeo yake itakuwa ni mapinduzi. Ili Tujenge Taifa la ki democrasia ni lazima kila mtu ajihusishe katika ujenzi wa Taifa lake na kila mtu awe huru chini ya sheria. Tusiendelee kujenga taifa la watu wanaokandamizana au wanaoingia kwenye uongozi kwa maslahi binafsi.
Lakini pia ubora wa Taifa letu utategemea pia ubora wa vyama vyetu vya siasa na watu wanaoviunda. Mawazo yao na itikadi zao.
Juu ya yote ni lazima tuwe na itikadi ya Taifa ambayo itakuwa dira kwa vyama vyote. Hili ni jambo la muhimu kwa Taifa. Umoja wa Taifa letu ni jambo ambalo ni la kimsingi. Ni lazima tuunde Taifa la watu ambao wanajaliana. Kama unaenda jeshini unaenda kwasababu unapenda kutoka nafsini kulinda raia na unafanya hivyo kwa mapenzi na sio kwa mshahara au kwasababu umekosa kazi. Kila kazi katika Taifa hili ni lazima iwe ni kazi yenye thamani ili mradi iwe halali kwasababu ni yenye kusaidia wengine. Hii ni mantiki ya mgawanyo wa kazi hatuwezi kuwa wote madaktari, manesi nk. Tunatumikia Taifa moja.
Taifa hili lazima liwe katika mwelekeo mmoja na tumaini moja. Ni lazima tuamini tunauwezo wa kujenga Taifa nzuri mbalo roho zetu zitaiishi na watu wa makabila yote na dini zote watarifurahia na kushangilia utaifa wao. Taifa ambalo wanamichezo wataenda kulipigania sio sababu ya hela bali sababu ya uzalendo wao. Taifa ambalo watu watafurahia kulitumikia na watu wake bora watapewa nishani na kuheshimiwa na vizazi vyote.
Taifa ambalo thamani ya mtu ni utumishi wake uliotukuka kwa Taifa na kwa watu. Katika matumaini haya ninatembea, ninaishi na ninaota. Ya kwamba siku moja tumaini litafufuka kama mmea uchupuavyo kutoka ardhini na watu wa Taifa hili watatambua, ya kwamba; Taifa hili linauwezo wa kukua na kuwa kubwa na kama Taifa lolote lingine lililowahi kuwepo duniani kama tukiwa wamoja, kama tukitia juhudi na kama tukitumia muda wetu kutafuta maarifa na hekima. Katika tumaini hili ni lazima tuishi, ni lazima tuote ni lazima tulifanyie kazi.
Kaka na dada, baba na mama. wajomba na mashangazi kama tutakuwa wamoja hakuna kitakacho tushinda. Ndani yetu kuna roho ikiamua na ikadhamiria kutoka katika hakuna tutakuwa nacho. Kutoka katika dharau tutaheshimiwa. Ni lazima tutambue tunachohitaji kama Taifa. Hii ni ndoto na ni lazima imee kwa kila mtanzania, Kutoka mtaani mpaka chuoni. Watu wetu bora wa Taifa hili lazima tujiunge pamoja. Katika Roho hii ya utaifa huu ni wito wangu.