Katika Matajiri wetu 10 wa juu Tanzania, hakuna aliyesoma Chuo Kikuu ndani ya nchi! Uchumi wetu unategemea elimu za nje, kwanini?

Elimu ya Tanzania ni historia ya elimu...mtaala upo relevant kwa miaka ya 50, 60, 70....sio leo 2019....
watu hawafundishwi Mitaala haifundishi
  • social media,
  • entrepreneurship,
  • apps, AI, coding, internet of things,
  • personal finance,
  • Real life tax
  • Foreign language
  • online business, vlogging, blogging,
  • project management,
  • customer care,
  • branding,
  • real estate
  • trading
  • Agro-processing and value additions
  • Waste management
  • Foreign Markets - how to export product to Asia, Middle East, Europe etc
  • how to open a formal business
  • project financing??
Miaka mi3 wanajadili theory tu za Maslow etc....bila kugusia mambo ambayo yanahitajika kutatua changamoto za kila siku. lakini tunahitaji kubadili mfumo wa elimu uwe zaidi katika lengo la kutatua changamoto tulizonazo sasa.
 
Sasa mtu alishatajirika kabla hajasoma chuo kikuu asome chuo nchini kwa sababu gani. Hao tayari wanamapesa akisoma huko nje hata akifeli anakuja kwenye makampuni na mabiashara yao maana mitaji wanayo. Sasa wewe na first class yako ya bongo bado unarudi kusota unasubiri ajira ya JPM.
Mbona shigongo yupo chuo now anachukua degree licha ya kuwa tayari ni tajiri!?
 
Utajiri unapatikana kwa njia Nyingi, angalia historia ya Utajiri wa Marehemu Mengi kuna Ukakasi ila kwakuwa katangulia tukae kimya, Nakuja kwa mkono japo hayupo top ten ila wakubwa mnanielewa,

Tajiri Pekee ni Backhresa na Mo wame hassle sana na ukiangalia Said hana hata cheti cha Form Four,

Lakin pia zamani kusoma nje ilikuwa lazima maana kuna mambo tulikuwa tunayakosa,

Usishangae matajiri wa baadae wanatoka kwenye shule za kata
Yaani Mo utajiri wake hauna Ukakasi? Huyu huyu Mo mtoto wa Ghulam? Ina maana Mauza uza ya Ghulam huyajui?Britanicca hapa umechemsha aisee.
 
Msomi kama Mwigulu hivi anaweza kweli kuhustle nje ya siasa? Wanachoweza wasomi wetu ni kula kodi za wanyonge tu.

Ukiwaona kwenye majukwaa wanahimiza watu wajiajiri wakati wao na PhD zao wanakomaa kwenye ajira ya Magufuli
 
UDSM jina la kozi nimesahau
Hili ndio tatizo kuu la wabongo kujikuta wanajua kila kitu mwisho kuwalisha wenzenu matango pori... Shigongo yupo chuo cha Tumaini campus ya Dar (TUDARCO) pale Mwenge na sio UDSM kama unavyomuanisha huyo mdau na sasa hivi yupo third year means anamaliza mwaka huu
 
Habari Wadau..

Wote tumeguswa na msiba wa tajiri wetu mweusi Mr. Mengi aliyekuwa anaenda level zisizopishana sana na Watanzania weupe

Wasifu wake unaonesha hata yeye hakukanyaga chuo kikuu chetu ..

Na hapo hapo akapata akili ya kuwa tajiri na industrialist mkubwa sana...

Je, elimu yetu ipo sawa kweli?

Kwanini washika uchumi hawasomi elimu yetu

Simply kwasababu vyuo vyetu havitengenezi wafanyabiashara wa baadae bali vinatengeneza watu wakaajiriwe.
 
Utajiri unapatikana kwa njia Nyingi, angalia historia ya Utajiri wa Marehemu Mengi kuna Ukakasi ila kwakuwa katangulia tukae kimya, Nakuja kwa mkono japo hayupo top ten ila wakubwa mnanielewa,

Tajiri Pekee ni Backhresa na Mo wame hassle sana na ukiangalia Said hana hata cheti cha Form Four,

Lakin pia zamani kusoma nje ilikuwa lazima maana kuna mambo tulikuwa tunayakosa,

Usishangae matajiri wa baadae wanatoka kwenye shule za kata
Wivu kitu mbaya sana
 
Hili ndio tatizo kuu la wabongo kujikuta wanajua kila kitu mwisho kuwalisha wenzenu matango pori... Shigongo yupo chuo cha Tumaini campus ya Dar (TUDARCO) pale Mwenge na sio UDSM kama unavyomuanisha huyo mdau na sasa hivi yupo third year means anamaliza mwaka huu
Shigongo kapata utajiri akiwa na elimu ya msingi tu (darasa la saba)
 
Mengi alisoma Nje ya Nchi huko sasa wanaosema alitokea Familia ya kimaskini nashindwa kuwaelewaa????

Ukweli mtupu.....show me which family u were born and i will tell u why u are succesful......ishu nzima ni umezaliwa katika familia gani
 
Shigongo kapata utajiri akiwa na elimu ya msingi tu (darasa la saba)
Hayo ya kupata utajiri wala sikutaka kuyajua maana sio dhumuni la message yangu halafu sijui ume-quote kwenye message yangu wakati mie nilikua namjibu mdau mmoja aliyempoteza mwenzake kuwa Shigongo anasoma UDSM wakati sio kweli... Sasa nikuulize wewe mkuu umeni-quote na kusema Shigongo kapata utajiri akiwa na elimu ya msingi je kuna sehemu Umeona nimekataa swala hilo au pia kuna mahala nimetaka kujua kuhusu hayo mkuu????
 
Maprofesa wa Tanzania ni hao kina Kabudi, Mkumbo, Mwakyembe, Dr. Bana n.k yaani hawa wanafiki na wachumia tumbo ndio wamfundishe mwanafunzi awe milionea wakati hata wao wanategemea kumsifia magufuli ili wapate kuendesha maisha yao...
Hao akina prof Baregu na Safari wanaolamba viatu vya form six ZERO Mbowe wanelifanyia nini Taifa?
 
Back
Top Bottom