Katika jina la Mungu

Katika jina la Mungu

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,074
Reaction score
13,643
Katika jina la Mungu wajinga wengi walibatizwa au kusilimishwa.

Walipewa majina ya kigeni.

Walifundishwa lugha za kigeni.
Walifundishwa kuabudia kila upuuzi wa kigeni

Waliacha kufikiri na kuacha dini zifikiri kwa ajili yao.

Walidhalilishwa, kudharauliwa, na kunyonywa.

Walivisha kongwa vifuani na vichwani.

Walifundishwa kujichukia na kuchukiana.

Walianza kuana kwa ajili ya dini.
Waliporwa ardhi, mali, na utu wao.
Walitapeliwa.

Wamepotezwa na wamepotea milele.

Hilo ndilo neno la Mungu.
Aaaamina.
 
Mkuu kuna watu wakija hapa utapata kazi sana ya KUTHIBITISHA, uwe umejiandaa katika hilo
 
Katika jina la Mungu wajinga wengi walibatizwa au kusilimishwa.
Walipewa majina ya kigeni.
Walifundishwa lugha za kigeni.
Walifundishwa kuabudia kila upuuzi wa kigeni
Waliacha kufikiri na kuacha dini zifikiri kwa ajili yao.
Walidhalilishwa, kudharauliwa, na kunyonywa.
Walivisha kongwa vifuani na vichwani.
Walifundishwa kujichukia na kuchukiana.
Walianza kuana kwa ajili ya dini.
Waliporwa ardhi, mali, na utu wao.
Walitapeliwa.
Wamepotezwa na wamepotea milele.
Hilo ndilo neno la Mungu.
Aaaamina.
Mbona rahisi mkuu
 
Unachokiandika kimejaa hisia kali, lakini hakina usahihi wa kihistoria wala uwiano wa kiakili.

Kwanza, huwezi kuchukua historia changamano ya mabadiliko ya jamii nzima na kuipunguza kuwa kauli za “wajinga walibatizwa” au “walipotezwa milele.” Huo si uchambuzi, ni propaganda ya hasira.

Pili, Ukristo na Uislamu Afrika havikuingia kwa njia moja tu ya “kulazimishwa na kuharibu kila kitu.” Kuna sehemu za ukoloni zilikuwa za ukandamizaji, hilo halina ubishi. Lakini pia kuna historia ya watu waliokubali dini kwa hiari, waliitumia elimu, waliijenga, na hata waliigeuza kuwa chombo cha kupinga ukoloni wenyewe.

Tatu, madai ya “walifundishwa kuacha kufikiri” si ya kweli. Kama hilo lingekuwa sahihi, usingeona:

  • wanazuoni wa Kiafrika ndani ya dini,
  • harakati za ukombozi zilizoongozwa na watu waliokuwa ndani ya makanisa na misikiti,
  • wala falsafa na mijadala ya kiakili iliyotoka ndani ya taasisi hizo hizo.

Nne, suala la majina, lugha na utamaduni halimaanishi “kupotea kwa utu.” Historia ya dunia nzima inaonyesha jamii hubadilika, huchanganyika na hujifunza. Hiyo si kifo cha utambulisho, ni evolution ya kijamii.

Mwisho, kutumia kauli kama “hilo ndilo neno la Mungu” kuhitimisha maoni ya kihisia hakufanyi kuwa ukweli. Imani ni jambo moja, lakini historia na uchambuzi wa jamii unahitaji ushahidi na uwiano.

Ukosoaji wa ukoloni na madhara yake ni wa msingi na muhimu. Lakini kugeuza kila mabadiliko ya kihistoria kuwa “kupotezwa kwa milele” ni kurahisisha sana ukweli na kupoteza uhalisia wa historia yenyewe

Karibu kwenye uzi huu
Uelewe zaidi

Naheshimu maoni yako japo si hisia zako. Kila kitu kiko wazi. Tena, nimerahisisha na kufupisha mambo ili kila asomaye aelewe kirahisi. Kama hujaelewa, basi, nashauri. Soma tena ili uchangia kwa siha kiakili.
 
Aliyefufuka Leo na mapema

Tuimbe nyimbo nzuri Ngoma na saburi na Ngoma tucheze tumsifu mwokozi.
 
Back
Top Bottom