Katika hili wanawake wanakosea

House girl kupata mimba na kuendelea kukaa si jambo rahisi jamani, kipindi cha ujauzito anahitaji ku pumzika na kuna kazi nyingine anakuwa hawezi kufanya

akijifungua anahitaji msaada wa kuuguzwa yeye na mtoto, ina maana anatakiwa kuja house girl mpya kusaidia kuhudumia mzazi na kufanya kazi za ndani

zaidi ya gharama ya kumuhudumia yeye kama mzazi kunakuwa na gharama mpya ya kuhudumia mtoto...

bora kwanza kabisa hata kama wanakula na kuvaa na kulala kwetu tuwape mishahara yaani angalau pesa wanazoweza kuweka akiba, sio hizi pocket money za alfu 15 au 20 kwa mwezi mzima,

pia tuwa peleke kwenye shule za jioni ili angalau waweze kujifunza kitu hata kama ni ushonaji au chochote tuu kwa sababu hata wasipopata mimba bado kuna siku wata fikia umri wa kujitegemea wataanzia wapi wakati hata senti hawana? au wengine ndio wale wakiolewa hawajui shughuli yoyote ya kuwapa kipato zaidi ya kuwa goli kipa

after all nia ya kumleta mjini si kumwezesha ili asaidie wazazi? sasa hata hao wazazi atawasaidia vipi kama anapokea 15 000 a months

waki pata mimba bora warudi kijijini na tunawajibika kuwapa hela ya ziada ili wakichanganya na ile akiba waweze kufanya shughuli nyingine maana, kwa kuwa kufanya kazi za ndani inakuwa sio practical...unless ana pangisha chumba chake mwenyewe na analipwa mshahara wa kima cha chini na anafanya kazi day time jioni anarudi nyumbani..
 
Unakwenda kijijini unakuta familia masikini sana, hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kutwa, kuwaonea huruma unachukua binti yao hadi kwako mjini akufanyie kazi za ndani, apate pesa awasaidie wazazi wake

Binti akiwa kwako anapata ujauzito, bila kujali ameupata wapi, wewe unamludisha kwao,

-Je! huu ni uungwana?
-Hauoni kuwa unaiongezea familia umasikini na mzigo wa kulea mimba na hatimaye mjukuu?
-hakuna njia nyingine ya kumsaidia huyu binti zaidi ya kumrudisha kwao?
-Je ukikuta mimba hiyo ni ya mwanao wa kiume? na wakati huo umeisha mrudisha kwao!

...mambo matatu ya msingi.


kwanza, ni kumhoji Mimba ni ya nani.
Pili, iwapo anakubali kuilea mimba kisha mtoto, au anataka kuitoa
tatu, kama atailea... yeye na mhusika wa mimba hiyo wapo tayari kuilea mimba na mtoto huyo.

Haijalishi kama aliyemtia mimba ni Mtoto wa wenye nyumba, baba mwenye nyumba au rafiki tu...

Kumrudisha kwao ni kosa kubwa sana! Wazazi walimkabidhisha kwa mtu mzima mwenye akili timamu kwakujua atalelewa na kutunzwa asiharibikiwe na vishawishi vya mjini... Iweje atimuliwe na mzigo huo?

Akirudishwa kwao, wakulaumiwa ni wote, mama mwenye nyumba na Mumewe kwa kushindwa kufanya maamuzi ya busara.
 
Kumrudisha kwao ni kosa kubwa sana! Wazazi walimkabidhisha kwa mtu mzima mwenye akili timamu kwakujua atalelewa na kutunzwa asiharibikiwe na vishawishi vya mjini... Iweje atimuliwe na mzigo huo?

Akirudishwa kwao, wakulaumiwa ni wote, mama mwenye nyumba na Mumewe kwa kushindwa kufanya maamuzi ya busara.
Ongera mwanangu umenena, wengine mbona wanashindwa kuongea kama wewe? hata hivyo humu kuna waalibifu wengi na hao ndio ninapambana nao kuwaelimisha,
 
Back
Top Bottom