Katika hili wanawake wanakosea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katika hili wanawake wanakosea

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kaitaba, Nov 10, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unakwenda kijijini unakuta familia masikini sana, hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kutwa, kuwaonea huruma unachukua binti yao hadi kwako mjini akufanyie kazi za ndani, apate pesa awasaidie wazazi wake

  Binti akiwa kwako anapata ujauzito, bila kujali ameupata wapi, wewe unamludisha kwao,

  -Je! huu ni uungwana?
  -Hauoni kuwa unaiongezea familia umasikini na mzigo wa kulea mimba na hatimaye mjukuu?
  -hakuna njia nyingine ya kumsaidia huyu binti zaidi ya kumrudisha kwao?
  -Je ukikuta mimba hiyo ni ya mwanao wa kiume? na wakati huo umeisha mrudisha kwao!
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo ushauri wako ni kumlea huyo binti na mwanae atayemzaa, au kumpa pesa za kwenda kutoa mimba badala ya nauli ya kurudi kwao, au kuacha kuajiri mabinti toka vijijini kwa ajili ya kazi za ndani?

  Sijakuelewa!!!!
   
 3. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wewe unaona ukimrudisha kwao umemsaidia nini, kwa nini aliyempa mimba asipatikane akaozeshwa?

  Kama ni baba mwenye mji (mme wa huyo mama) anahusika aozeshwe
   
 4. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hilo suala ni zito, lazima uripoti kwao kwanza na hata kumrudisha, ukiitoa akifa utafanyaje,.na huyu naye umeenda kufanya kazi au kuvunja amri ya 6..ah suala zito.
   
 5. M

  Msindima JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Masaki hata mimi pia sijamwelewa jamaa kabisa yaani alikuwa nalenga nini? Kaitaba please hebu tufafanulie ili tuelewe zaidi.
   
 6. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ninacho maanisha ni hiki, ebu tafakari mtoto katoka familia masikini, anakuja kwako kujikwamua na umasikini, bahati mbaya anapata ujauzito, badala ya kumbana kumtaja aliyempa huo ujauzito, badala yake hakina mama wanacho fanya ni kumpa kipigo kama mwizi, kisha kumrudisha kwao,

  Sasa angalia, kwao ni masikini halafu anarudi kwao na mzigo, wewe unafikri wazazi watakuonaje,

  Njia nzuri ni kumuozesha tu, na mimba wasiitoe anaweza kupata matatizo ukafungwa

  namaanisha hilo.

  niulize tena
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  wakati ukimchukua ulimchukua kama mfanyakazi au ulimchukua ili uwasaidie wazazi wake au umsaidie yeye?..hueleweki.
  kama ni msaada, ungemsomesha ili aje kuwasaidia wazazi wake, kama umeamua kumpa kazi basi kuwe na terms........kama unaishi naye kama ndugu basi act kama ndugu.

  kila mtu t=yuko responsible na maisha yake.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nafikiri hili suala inabidi tuliweke ktk mazingira ya kitanzania yaani tunawachukua hawa watoto wa kike kama wafanyakazi wa ndani lakini kiukweli huwezi kusema ni wafanyakazi per say. Wengi wao unakuta wadogo au hata kama wakubwa mambo mengi hawajui so ni kama kuwasaidia.

  Kwa hiyo kwa uungwana unaweza kumsaidia kwamba ajifungue huyo mtoto lakini wazazi wake wataarifiwe kuhusu hali ilivyo na pia lazima amtaje aliye mpa uja uzito, ili mambo ya kisheria yafuate baada ya kujifungua.

  Akisha jifungua kama utaona bado anafaa kuendelea kufanya kazi mimi sioni tatizo kwa nini asiendelee kuwepo mpaka yeye aseme anataka kuacha kukaa kwangu. Haya ni mawazo yangu na nafikiri ndivyo inapaswa kuwa.
   
 9. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nakubaliana na wewe, pia na wengine hata kama hawatakubali hapa lakini ukweli unabaki ulivyo, wewe ni kichwa
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hii mada ni muhimu sana kwa wanao elewa matatizo yanayo wapata watoto wetu wengi katika jamii yetu. Wito wangu tu kwa akina mama kwenye familia zetu tuwalee hawa watumishi wetu wa ndani kama watoto/wadogo zetu na wanapo kosea basi waadhibiwe kama watoto/ndugu zetu na siyo kuwa fukuza au kuwapiga kama wezi.

  Huwezi kumuita mtu mfanyakazi wakati unamlipa shs 10,000 au 15,000 kwa mwezi!!! Hawa ni ndugu zetu!!
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hivi wewe ni kaitaba,mr au mrs?
   
 12. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Humu kuna makaitaba wangapi?
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hivi ukimuuliza mimba kapata wapi na akataja ya mumeo bado utaendelea kukaa nae na kumsaidia?
  kwa swala la mshahara ni kweli halina mvuto 15,000.00 ni ndogo sana
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hivi kwa mfano ukimuuliza mimba katoa wapi akakwambia ni ya mmeo utafanya nini hapo??
  swala la mshahara nalo ni issue 15,000.00 ni ndogo sana kwa maisha ya sasa sijui huwa tunafikilia nn kuwapa mshahara mdogo namna hii?
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hapo ndo ukweli utaujua lakini ukimfukuza haraka hutaujua ukweli na hata kama ni mumeo ndo kampa mimba mtumishi wa ndani sheria lazima imbane, tumeyaona kwa Mahita.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  aah leo JF inanifanyia kiini macho :mad:
   
 17. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mpaka anapata ujauzito, Mkeo hakujua tabia yake imebadilika arudishwe mapema kabla ya mimba?
   
 18. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hili sio suala dogo la kukurupuka,Inategemea na kipato cha mtu kikoje,kama wewe mwenyewe haujitoshelezi utawezaje kumhudumia mjamzito na akishajifungua na mwanae?Makubaliano yalikuwa ni kufanya kazi.
  Na huo mshahara mdogo wa 15 elfu pia inategemea na kipato cha mtu,kuna wengine ni mabaamedi wanalipwa hela ndogo kwa mwezi.
   
 19. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nini tena FL1??
   
 20. M

  Magezi JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ukikuta mimba ni ya mmeo hapo uamue kumuadhibu mmeo na siyo huyo binti kwni ni wewe ulimleta na amedanganywa na mumeo.

  Ndiyo maana nikasema tushukulie mazingira ya kitanzania ambapo tunafanya mambo kiudugu lakini tukisema kazi kama kazi hakuna mtu wa kawaida atakaye chukua mtoto wa mtu eti ni mtumishi wa ndani.

  Kuhusu mshahara hii inatokana na kwamba chakula wanapata ktk familia, matibabu, kulala, n.k. Lakini tukifanya kama nchi za wenzetu kwa mab ni ajira rasmi mshahara utapanda lakini inabidi huyu mtumishi ajitegemee kwa chakula, matibabu, maji, umeme (kama upo), malazi n.k. kwa hiyo hakuna mtoto wa maskini atakaye weza hayo.
   
Loading...