Katika hili, wanawake mtuhurumie sisi wanaume

Katika hili, wanawake mtuhurumie sisi wanaume

Imetokea.
Shemeji alivyo mcheshi, mpole na mchangamfu na mwenye kujali ni ngumu kuamini..
Ilikua kama utani baada ya kujifungua na mtoto kukua na kuanza kuonyesha tabia zake, ndipo wakubwa wakaya wakadai hyu mtoto mbona hafanani na tabia za koo zetu.?? Walihoji
Ugomvi kati ya kaka na familia ukanza, familia ikidai kutaka kutambua uhalali wa mtoto kama ni damu yao kupitia vipimo vya DNA.
Ikabidi kaka awaelewe na akakubali kufanya hivyo majibu kurudi mtoto si wetu.
Namuonea huruma kaka mnoo hakika mapenzi kwa mwanae ambae si wake yalikua mkubwa mnoo kila akimtazama mwanae huishia kulia tu.

Haelewi akubali tu kumlea mwanae sababu amezaliwa ndani yke au amkatae tu.

Wanawake tuoneni huruma na hii dhambi ya kutupa watoto ambao sio wetu.
Ndio hapo sasa utambue kuwa hawa wanawake ni wakugegeda na sio kuishi nao.
 
Umefanyiwa hivyo wakati mahari umepangiwa kama hii,lazima pachimbike
 

Attachments

  • Mahari.2.jpg
    Mahari.2.jpg
    15.3 KB · Views: 26
Daaah yaani kanisa ninalo sali kuna jamaa alikuwa anamla mke wa mwenzie balaaa,Mpaka likafika kwenye ngazi za uongozi wa kanisa..Mambo yakaisha kimtindo,ila baada ya muda Bidada akapata ujauzito,ebwana mtoto copy ya Mgoni...Tatizo kwa mwenye mke,jamaa hata useme nini hakuelewi na mtoto wake.
 
Baba yake akimfata? Hivi mnajua migogoro ya watoto? Hakuna cha baraka sana sana Mke atazidi kuchepuka kwa baba mtoto. Sipendi uongo mm ningekuwa Huyo mwanaume ningefukuza.akaolewe na baba mtoto wake

luckyline siku hizi umekuwa na roho ya korosho kweli.
 
Kitanda hakizai haramu, nyie leeni tu.
 
Usithubutu kulea mwana siyo wako, atakubutua tu siku moja, hata kukusimanga waziwazi, ndo wale wanasemaga baba alinitesaaa! sana, kama Kanumba alivokuwa anamlaumu baba yake waziwazi, kwenye vyombo vya Habari, kwa mambo ya hovyo sana,
eti kuchunga mbuzi wakati wa jua kali! ni kosa la jinai? anataka nani akamchungie mbuzi wa babake, cha baba ni changu, wakati huyu mzee alikuwa anampa Kanumba skills ya kulea mbuzi km mzazi wake.

toto lisilo lako haijalishi ni Rais au superstar atakunanga tu. hata kukutoa ndagu.

Damu yako itasema daaa! mshua alikuwa anapenda kuni discipline, na kunifundisha kazi, alikuwa hana mchezo ktk kazi, ili nikue kwa adabu, na kujitegemea.
angalia Diamond kwa baba yake , yaani yule mzee Diamond ni damu yake kabisaaaaa! hana makuu kwa babae yule mwanamuziki.
 
Tusimuhukumu mwanamke,
Wakati mwingine tuwe tunageuka na upande wa pili

Unakuta binti unampenda kumuoa yeye anakwambia anae mpenzi wake. Unakazania kuanzisha penzi jipya kwake huku yeye ana mpenzi wake wa zamani,

Kwa kuwa anaona anaempenda bado hajajipanga na umri unakwenda, anakubali kuolewa na wewe huku alikuwa na mpenzi wake.

Kibaya zaidi mnaonana saa mbili asubuhi, saa tisa jioni mnafunga ndoa. Mwisho wa siku akija na ka mimba ka jamaa kosa lake litakuwa wapi??


Kabla huyi mwanamke hajahukumiwa, mume atoe maelezo ya namna alivyoingia ndoani
 
Back
Top Bottom