Katika hili mimi nasimama na Mbowe, hakika jamaa kakomaa kisiasa na anaijua vizuri siasa

Yah mnafuta ili msije kumtangaza mungine kinyume na alivyojitangaza yeye, afu ikaja kuonekana kuwa kaonewa.
Sheria inataka kufuta matokeo au kumpeleka mahakamani? Kwahiyo 2020 Lisu angejitangaza kuwa ndio mshindi wa uchaguzi, ungefutwa na kurudiwa?
 
Sheria inataka kufuta matokeo au kumpeleka mahakamani? Kwahiyo 2020 Lisu angejitangaza kuwa ndio mshindi wa uchaguzi, ungefutwa na kurudiwa?
Hapana Zanzibar wana sheria zao ambazo huku kwetu huwa hazifanyi kazi.
Nafikiri kama hilo swala lingekuwa sio la kisheria basi maalim angeenda mahakamani.
 
Hapana Zanzibar wana sheria zao ambazo huku kwetu huwa hazifanyi kazi.
Nafikiri kama hilo swala lingekuwa sio la kisheria basi maalim angeenda mahakamani.
Mahakama ipi boss kwa viongozi hawa hawa wanaopora chaguzi? Huku Bara ndio kuna ruhusa ya kujitangaza bila kuchukuliwa hatua? Una uhakika kuwa huko Zanzibar sheria inasema ukijitangaza mshindi uchaguzi unafutwa?
 
Uhakika sina maana mimi sio mfuatiliaji wa sheria zao. Ila kama muhusika hakwenda mahakamani basi huenda sheria hiyo ipo na ndio iliyombana yeye kuchukua hatua.
 
Huo mkutano ndio ambao pia Lissu amezungumzia habari za nusu mkate na mengine...

Hoja hapa, hayo anayozungumza ameshawaambia wenzake chamani wakagoma kumsikiliza mpaka aende kuropoka barabarani?

Au tunakubaliana Chadema hakuna taratibu zozote, kila mwenye jambo lake anaruhusiwa kusema popote atapoamua?

Hii tabia ya kila kiongozi kujiamulia kuongea anachotaka popote ikiota mizizi itasababisha wale wanaosema Chadema ni kama kambale baba ndevu..watoto ndevu.. wapate hoja, lazima ikemewe mapema.
Afadhali na wewe umeliona hili mkuu.
Tatizo jamaa ana tabia ya kuongea lolote linalokuja katika mdomo wake, hata yale ambayo kama kiongozi wa chama hatakiwi kuyaongelea ongelea hovyo majukwaani.
 
Si Mbowe tu, sema CDM nzima imeshiba viongozi wanaojitambua, Chama makini, viongozi makini, wanachama makini.
Mwenzako anawashambulia kwamba hawako makini ndio maana wanaburuzwa katika maridhiano afu wewe unakuja kusema eti chama kizima kimejaa viongozi makini!

Sasa wewe na Lisu nani mkweli?
 
..Ccm wana utaratibu wa kukabidhi akili zao kwa Mwenyekiti.

..Chadema kila mwanachama ni "kambale" na ana ruhusa ya kutoa mawazo na msimamo wake.
Ya inawezekana kuwa sasa hivi kila mtu ni kambale, lakini wakati wanaokotwa na kuletwa chamani walikuwa bado ndubwi ndomaana kila walichoambiwa wakati ule walifuata utaratibu wa chama.
 
Back
Top Bottom