Katibu wa Nyerere: Jina la mwalimu linatumiwa vibaya na kambi ya Lowassa

Mshahara wa Lowassa
  1. Akiwa AICC TShs. 362,500 (~$2,500)
  2. Akiwa Waziri Wa Ardhi TShs. 1,881,600
  3. Hapa ndio akajenga lile jumba la ubalozi wa SA, lenye thamani ya ~TShs. 300,000,000 (1994)

Hebu atupe kwa kuanzia maelezo ya jinsi alivyojenga hilo hekalu na jinsi alivyopata kiwanja kule Masaki.

Kupata kiwanja masaki wewe unaona dili sana eee mbona kawaida tu.
 
Mutajidanganyana sana kwa kudhani wamasai Wote Ni kama SOKOINE..........haya Sasa ngoma imeanza kuvuma, watetezi wa Lowasa fanyeni hima mje upande huu.

Hivi nani huwadanganya watu kuwa Lowassa ni Mmasai?
 
Mshahara wa Lowassa
  1. Akiwa AICC TShs. 362,500 (~$2,500)
  2. Akiwa Waziri Wa Ardhi TShs. 1,881,600
  3. Hapa ndio akajenga lile jumba la ubalozi wa SA, lenye thamani ya ~TShs. 300,000,000 (1994)

Hebu atupe kwa kuanzia maelezo ya jinsi alivyojenga hilo hekalu na jinsi alivyopata kiwanja kule Masaki.

Na pia Jengo la zamani la ubalozi Wa marekani ni la kwake ....Hoji na hilo endelea kuuza sura wakati wanaume wanatafuta pesa
Viva Lowasa
 
Mshahara wa Lowassa
  1. Akiwa AICC TShs. 362,500 (~$2,500)
  2. Akiwa Waziri Wa Ardhi TShs. 1,881,600
  3. Hapa ndio akajenga lile jumba la ubalozi wa SA, lenye thamani ya ~TShs. 300,000,000 (1994)

Hebu atupe kwa kuanzia maelezo ya jinsi alivyojenga hilo hekalu na jinsi alivyopata kiwanja kule Masaki.

Hujatueleza marupurupu mengine aliyopata akiwa kwenye nafasi hizo mfano safari nje ya kituo cha kazi,saa za ziada ofisini nk. Kwa mtu mwenye kujielewa pesa aliyokuwa analipwa ni nyingi na mchumi mzuri angeweza kufanya mambo makubwa tuu.wengi wa level yake waliwekeza kwenye ngono na starehe.Leo ndio wanaohangaika kuushangaa utajiri wa Lowasa.Kiukweli wapo wengi serikalini wenye utajiri kuliko huo wa Lowasa licha ya muda wao mfupi wa utumishi.
 
Hujatueleza marupurupu mengine aliyopata akiwa kwenye nafasi hizo mfano safari nje ya kituo cha kazi,saa za ziada ofisini nk. Kwa mtu mwenye kujielewa pesa aliyokuwa analipwa ni nyingi na mchumi mzuri angeweza kufanya mambo makubwa tuu.wengi wa level yake waliwekeza kwenye ngono na starehe.Leo ndio wanaohangaika kuushangaa utajiri wa Lowasa.Kiukweli wapo wengi serikalini wenye utajiri kuliko huo wa Lowasa licha ya muda wao mfupi wa utumishi.

Itabidi pia labda nielezee michango ya harusi n.k, n.k?? Kwa ufupi ni kuwa LOWASSA ni mwizi, ukitaka kumtetea utetee tu wizi wake.
 
Na pia Jengo la zamani la ubalozi Wa marekani ni la kwake ....Hoji na hilo endelea kuuza sura wakati wanaume wanatafuta pesa
Viva Lowasa

Hongera, naona umeamua kutetea wizi badala ya kusoma na kufikiria kilichoandikwa.
 
Kupata kiwanja masaki wewe unaona dili sana eee mbona kawaida tu.

Miaka ya 1990s kuendelea mbele, mahali alipojenga LOWASSA ilikuwa ni big deal kupata kiwanja, achilia mbali gharama za lile hekalu. Maelezo mafupi toka kwa mheshimiwa yangetosheleza lakini kama mla rushwa yeyote, rushwa hailezeki zaidi ya kudai tu kuwa yeye ni mchukia umasikini.
 
Mshahara wa Lowassa
  1. Akiwa AICC TShs. 362,500 (~$2,500)
  2. Akiwa Waziri Wa Ardhi TShs. 1,881,600
  3. Hapa ndio akajenga lile jumba la ubalozi wa SA, lenye thamani ya ~TShs. 300,000,000 (1994)

Hebu atupe kwa kuanzia maelezo ya jinsi alivyojenga hilo hekalu na jinsi alivyopata kiwanja kule Masaki.

Vipi mwalimu wako wa hesabu bado yupo?


362,500/$2,500=145 tsh @$1 viwango vya mwaka gani huu?




[h=2]Table for recent years[/h]
CountryCurrencyCode2014(est.)[SUP][4][/SUP]20092006200520042003200220012000
19981990

TanzaniaTanzanian shillingTZS1,178.11,2551038924.70876.41800.41744.76664.67612.12
Arusha International Conference Centre
Managing Director19891990
 
Hivi kwani yeye Nyerere ni nani?

Si ndio huyu aliyeua vyama vingi mara baada ya TANU kuchaguliwa na kuweka vipengele ndani ya katiba mwaka 1962 ili awe Sultani wa Tanzania kwa kuua demokrasia na kumfanya Rais awe Mungu mtu hapa Tanzania kwa kujishindanisha yeye mwenyewe na kivuli chake kwenye uchaguzi bila kuwa na mpinzani?

Si ndie huyu aliyechakachua elimu ya ahueni ilioachwa na Mkoloni ambayo naye aliisomea kwa kuingiza Siasa ndani ya elimu ya Tanzania kwa kuondoa lugha ya Kiingereza kama ya kufundishia na kutumia Kiswahili bila matayarisho yoyote ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia na hivyo kuwafanya Watanzania wanamaliza darasa la saba wakiwa mambumbumbu wakati waliosoma kwa kutumia mitaala ya kikoloni walikuwa wanamaliza darasa la nne wakiwa wameiva kisawasawa kuyakabili mazingira yao?

Si ndie huyu baada ya kukaa zaidi ya miaka ishirini Ikulu akaondoka wakati nchi iko hoi kiuchumi mpaka tukawa tunakula unga wa njano (Yanga) kwa ajili ya Farasi ambao ulikuwa ni wa msaada kutoka marekani?

Si ndie huyu aliyekuwa muasisi wa ufisadi hapa nchini kwa kuwaruhusu makada wa TANU na baadaye CCM kuiba wanavyotaka na kisha wakishafilisi kiwanda au shughuli ya biashara wanahamishiwa kwingine?

Si ndie huyu wakati wake wananchi walikuwa hawawezi kununua vitu vya msingi kabisa kama chakula na sabuni za kufulia kwenye maduka ya kawaida bali kwenye maduka ya ushirika tu na tena kwa foleni na tena mpaka upate kibali cha mjumbe wa nyumba kumi ili uweze kuruhusiwa kununua?

Si ndie huyu aliyekuwa muasisi wa siasa za ukabila kwa kuyatenga makabila makubwa (Wachaga, Wasukuma, Wahaya na Wanyakyusa kwenye kushika nafasi za juu kabisa za kisiasa hapa Tanzania ilihali walishiriki kikamilifu wakati wa kudai uhuru kabla hata yeye mwenyewe hajaingia kwenye ulingo wa siasa?

Si ndie huyu aliyeasisi muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa ajili ya maslahi yake binafsi pamoja na wanasiasa wachache wa ngazi ya juu ndani ya muungano dhidi ya maslahi ya Watanganyika na Wazanzibari walio wengi?

Si ndie huyu aliyeingilia kati na kumfundisha Mkapa jinsi ya kuiba kura kwa kutumia mtutu wa bunduki wakati CCM iliposhindwa kule Zanzibar na kusababisha damu ya Wazanzibari wasio na hatia kumwagika bila huruma hata kidogo ili CCM iendelee kutawala kwa mabavu?

Sasa msituletee habari za huyu jamaa na mkadhani kwamba jina lake ni mtaji wa kisiasa. Ni mzigo (Liability) kwa maendeleo ya kidemokrasia na kiuchumi hapa Tanzania.

Na UKAWA wanalijua hilo. Ndio maana kwenye kampeni zao wanajumuisha utawala wote wa tangu enzi ya uhuru (miaka 54) kama kipindi cha CCM kushindwa kuleta maendeleo ndani ya Tanzania.

Na ni kwa sababu hii ya UKAWA kuelewa tatizo letu kama nchi ndio maana ninawaunga mkono. Bila shaka Lowassa na wagombea wa UKAWA wana kura yangu kwenye eneo langu la uchaguzi, kura ambayo Lowassa asingeipata kama angeteuliwa kugombea akiwa ndani ya CCM.
 
Mtu kuwa tajiri, kusimnyime haki ya yake msingi ya kuchaguliwa kiwa kiongozi.

Kwahio Nyerere alichotaka kusema ni kwamba mtu alie tajiri zaidi yake hawezi kuwa rais?! Mimo natafsiri kama wivu!

Mbona Purushenko ambae ndo Bahkressa wa nchi ya Ukraine, amekuwa rais na anafanya safi sana tu.
 
Kwaio kama Nyerere alimkataa na mimi ndo nimkatae. Nyerere kafanya mengi mazuri sikatai, lakini hakua Mungu! Alikua binadamu tu kama mimi na wewe.

Nyerere alimkataa EL kwa sababu zake, na mimi nimemkubali EL kwa sababu zangu!
 
Mwaka 1990 kama ulikuwa ushabalehe wakati huo basi utajua kuwa pesa yetu ilikuwa na thamani.

Kiasi kwamba hesabu ulizoziweka huzioni siyo?

Siyo wewe umeweka hii hesabu kwamba alikuwa analipwa 362.500 sawa na $ 2,500 ?

Kwa maana hiyo 1990 mimi ambaye siku balehe elimu yangu ya Shule ya Kata napata kuwa Dola mmoja ilikuwa 145tsh kwa hesabu zako. Ndiyo maana nakuuliza uliyebale wakati huo!

Unadhani kwa hizo dola 2500 hawezi kufanya uwekezaji ambao leo hii amekuwa Bilionea?

362,500/$2,500=145 tsh
 
Mwalimu amekufa na Siasa zake za Ujamaa na Kujitegemea na Chama chake cha Tanu na CCM ile.
Nchi ilibadilika tukaingia kwenye uchumi wa soko huria ambapo sasa "market forces" ndio determinant ya bei ya bidhaa!, hivyo Azimio la Arusha likazikwa na Azimio la Zanzibar!, CCM ya sasa imebinafsishwa kwa wenye nazo!, imehodhiwa na wenye pesa, hivyo rais wa Tanzania wa 2015 doesn't have to be chaguo la Mwalimu, kwa sababu hata Mwinyi hakuwa Chaguo la Nyerere, Mkapa hakuwa chaguo la Mwinyi, na JK hakuwa chaguo la Mkapa!.

Rais tunayemtaka 2015 sio chaguo la mtu bali ni chaguo la watu!.

Pasco
Na kwa vile jana ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali
 
Back
Top Bottom