Katibu wa Nyerere atishwa

Katibu wa Nyerere atishwa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
Katibu wa Nyerere atishwa

KATIBU Myeka wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Samweli Kasori, amepokea vitisho kutoka kwa watu kadhaa baada ya uamuzi wake wa ‘kufukua' ukweli uliofichika, baada ya baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kulihusisha jina la Mwalimu Nyerere na mbio zao za urais. Hali hiyo inajitokeza ikiwa ni siku kadhaa tangu Mzee Kasori kunukuliwa na gazeti dada na hili la Raia Tanzania, kwamba baadhi ya wanasiasa wanatumia vibaya jina la Mwalimu Nyerere kwa malengo yao.

Gazeti la Raia Tanzania lilimnukuu Kasori, ikiwa ni siku kadhaa kupita tangu Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba, anayedaiwa kuwamo kwenye kambi ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kunukuliwa na gazeti hilo la Februari 10, mwaka huu, akidai kabla Mwalimu Nyerere hajaaga dunia alimkubali (aliridhika na) Lowassa.

"Ni kweli kwamba jina la Lowassa lilikatwa na Mwalimu kwa sababu mbalimbali, lakini Rais Mkapa alipotangaza Baraza lake la Mawaziri mwaka 1995, baada ya miaka miwili tu mwenyewe akaona kuna upungufu; akaamua kumuingiza Lowassa katika Baraza la Mawaziri. Ninaamini Mkapa alipewa ushauri na Mwalimu Nyerere," alinukuliwa Komba. Vitisho dhidi yake Baada ya gazeti hilo la Raia Tanzania kuchapishwa likimkariri kujibu sehemu ya madai ya Komba, Mzee Kasori aliwasiliana na chumba chetu cha habari kueleza vitisho alivyopata kutoka kwa mmoja wa watumishi serikalini (jina lake na taasisi inahifadhiwa).

Katika vitisho hivyo vilivyotolewa kwa njia ya simu kwake, Kasori anatakiwa kuacha kuharibu mipango ya maisha ya watu (hata hivyo, gazeti hili halikuweza kubaini mara moja mipango hiyo inayovurugwa ya maisha ni ya nani hasa). Taarifa zaidi kutoka vyanzo vyetu kadhaa vya habari kutoka serikalini zinaeleza kwamba, Mzee Kasori amechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzitaarifu baadhi ya mamlaka za juu serikalini.

"Salaam, leo Alhamisi Februari12, 2015, saa 4:45 asubuhi nimepokea simu kutoka kwa (anamtaja mtumishi wa serikali) akilalamika kwamba namharibia (anataja jina la mwanasiasa) shughuli zake za kutafuta maisha katika kuwania (anataja nafasi ya uongozi wa dola)," inaeleza sehemu ya ujumbe wa Mzee Kasori kwenda katika moja ya mamlaka za juu serikalini.

Ujumbe huo unaendelea kueleza; "Kweli huyu Mungu mpya aitwaye fedha ana nguvu za ziada ndani ya akili na mioyo yetu."

Alichokisema Mzee Kasori Kwa kuzingatia maelezo ya Komba kama yalivyonukuliwa awali, gazeti la Raia Tanzania lilimtafuta Kasori, mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa karibu wa Mwalimu Nyerere, ambaye aliweka bayana kwamba, haamini kama Mwalimu Nyerere aliridhishwa na Lowassa kama alivyodai Komba.

"Haya masuala nilikwishayaeleza yote na kuyaweka kwenye mtandao. Siogopi nilikwishayaweka wazi," alianza kueleza Mzee Kasori. Katika maelezo yake hayo, Kasori anaendelea kusema: "Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu Mheshimiwa Edward Lowassa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.

Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha. "Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowassa alinipigia simu na kusema yafuatayo: "Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma'.

Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowassa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa Taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu.

Hiyo ikawa itifaki njema kwangu! "Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni Mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema, Bwana Kasori, jana ulizungumza na Edward Lowassa, naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa Taifa tafadhali" "Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu. "Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa, Mheshimiwa Edward Lowassa kupitia kwa Mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma.

Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa, nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowassa"! "Kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili, Kawawa sikumwambia hivyo! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena Watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa.

Mheshimiwa Kawawa alikubali. "Nikarudi kwa Baba wa Taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa, Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowassa tutakapofika Dar es Salaam. Baba wa Taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mheshimiwa Mzee Kawawa kuwa Lowassa na Guninita na wapambe wengine wa Lowassa wote wafike Msasani. "Siku ya siku ikafika.

Tukawepo Msasani na Mheshimiwa Mzee Kawawa akaja. Lowassa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe (muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano.

Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowassa yuko wapi? "Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema, Rashidi, huyu Kasori ananiambia eti niende Monduli nikasafishe jina la Mheshimiwa Lowassa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM.

Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowassa. Kasori alikuambia eh?" "Oneni, huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mheshimiwa Mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mheshimiwa Mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia "NDIO ALINIAMBIA".

Mwalimu akacheka sana! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana. "Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa, Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowassa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowassa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowassa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowassa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa Chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowassa asikose ubunge. "Kweli Lowassa ni jasiri sana kusema maneno hayo.

Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowassa ni jasiri sana! Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowassa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu.

Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda, umesikia eh?" "Mkutano ukaisha hapo Msasani.

Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowassa. Hadi Baba wa Taifa anafariki, sikuwahi na sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowassa anakanusha alivyolimbikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza," alidai Mzee Kasori.


Chanzo: Raia Mwema


CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, Daudi Mchambuzi, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Kill 3, everlenk, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto,
 
Nadhani tatizo siyo tu kuna mtu anatishwa kwa kuingilia maisha ya watu, ila kuna watu wana kiburi kilichopitiliza kiasi cha kufikiria wanaweza kufanya lolote tu , popote tu na hakuna anayepaswa kuhoji. Kama vile wao ni miungu flani hivi na wananchi woote ni mifugo yao tu, unayoweza kupanga "huyu uza"..."huyu chinja kesho!"....

Tatizo ni kuwa tumewapa hiyo jeuri wenyewe, na hatuonyeshi kuelewa kama ni kosa letu. Leo mtu mmoja anateua watu wa ovyo ovyo kabisa kuwa watumishi wa chama na serikali hakuna hata anayehoji ni kwa nini. Leo mtu anapora silaha akijisikia tena kituo cha polisi. Na intelijensia hakuna kabisa! Unbelievable!

Tusipoacha tabia ya kupuuzia kila kitu, itatugharimu mno hapo baadaye kidogo tu. Na kwa ninanvyoona hatuko salama tena! Na nitasema tena...Tanzania ikipoteza utulivu ni kwa sababu ya CCM na serikali yake. Siyo wahuni flani, siyo vibaka, panyarodi au wapinzani. Na historia itakuwa shahidi wa kauli hii.
 
Unachosema Mkuu Elly B ni kweli kabisa. Kumbuka jinsi Mh Warioba alivyodhalilishwa kisa tu cha kufanya kazi aliyotumwa na Kikwete pamoja na Tume yake. Kwa kuwa tu yeye na Tume yake waliamua kufanya kazi ile ya kukusanya maoni ya katiba toka kwa Watanzania kwa umakini mkubwa na hivyo kuamua kuweka maslahi ya Tanzania mbele badala yale ya CCM wakaonekana watu wabaya na hata Warioba kutukanwa matusi mbali mbali ya nguoni na hata kupigwa. Yule aliyemteua badala ya kumtetea akatoa kauli kwamba, "Warioba kajitakia mwenyewe" na anaomba yeye yasimkute kama yaliyomkuta Warioba!!!

Hivyo sitashangaa hata hawa wanaomtisha huyu Mzee wasifanywe lolote na wanaweza kabisa kuchukua uhai wake na hakuna yeyote kati yao atakayeguswa na mkono wa sheria. Kama ulivyosema Watanzania hatuko salama tena na hali hii tumejitakia wenyewe kwa kuamua kukaa kimya kwenye matukio mbali mbali ya kutisha, kusikitisha na kuudhi mno ambayo yanatokea karibu kila leo sehemu mbali mbali nchini mwetu.



Nadhani tatizo siyo tu kuna mtu anatishwa kwa kuingilia maisha ya watu, ila kuna watu wana kiburi kilichopitiliza kiasi cha kufikiria wanaweza kufanya lolote tu , popote tu na hakuna anayepaswa kuhoji. Kama vile wao ni miungu flani hivi na wananchi woote ni mifugo yao tu, unayoweza kupanga "huyu uza"..."huyu chinja kesho!"....

Tatizo ni kuwa tumewapa hiyo jeuri wenyewe, na hatuonyeshi kuelewa kama ni kosa letu. Leo mtu mmoja anateua watu wa ovyo ovyo kabisa kuwa watumishi wa chama na serikali hakuna hata anayehoji ni kwa nini. Leo mtu napora silaha akijisikia tena kituo cha polisi. Na intelijensia hakuna kabisa! Unbelievable!


Tusipoacha tabia ya kupuuzia kila kitu, itatugharimu mno hapo baadaye kidogo tu. Na kwa ninanvyoona hatuko salama tena! Na nitasema tena...Tanzania ikipoteza utulivu ni kwa sababu ya CCM na serikali yake. Siyo wahuni flani, siyo vibaka, panyarodi au wapinzani. Na historia itakuwa shahidi wa kauli hii.
 
Last edited by a moderator:
Atatolewa kucha huyu mzee ajiangalie sana kwani naamini meno hana kulingana na umri.

Tuna muombea mema
 
Serikali ya ccm imebaki kutishia watu kwa sasa
 
Unachosema Mkuu Elly B ni kweli kabisa. Kumbuka jinsi Mh Warioba alivyodhalilishwa kisa tu cha kufanya kazi aliyotumwa na Kikwete pamoja na Tume yake. Kwa kuwa tu yeye na Tume yake waliamua kufanya kazi ile ya kukusanya maoni ya katiba toka kwa Watanzania kwa umakini mkubwa na hivyo kuamua kuweka maslahi ya Tanzania mbele badala yale ya CCM wakaonekana watu wabaya na hata Warioba kutukanwa matusi mbali mbali ya nguoni na hata kupigwa. Yule aliyemteua badala ya kumtetea akatoa kauli kwamba, "Warioba kajitakia mwenyewe" na anaomba yeye yasimkute kama yaliyomkuta Warioba!!!

Hivyo sitashangaa hata hawa wanaomtisha huyu Mzee wasifanywe lolote na wanaweza kabisa kuchukua uhai wake na hakuna yeyote kati yao atakayeguswa na mkono wa sheria. Kama ulivyosema Watanzania hatuko salama tena na hali hii tumejitakia wenyewe kwa kuamua kukaa kimya kwenye matukio mbali mbali ya kutisha, kusikitisha na kuudhi mno ambayo yanatokea karibu kila leo sehemu mbali mbali nchini mwetu.




Ni ajabu zaidi kuwa mpaka leo watu wanaamini madikteta walikuwa Uganda na Rwanda na wapi sijui. Kwamba hii yetu ni ya kijamaa na kidemokrasia! Halafu bado hawataki tuandike upya katiba......Kwa sababu mimi ningeshauri tuandike Jamhuri yetu ni ya Kibepari na kijambazi. Siyo kwa sababu hayo ni mazuri, la hasha! ila kwa sababu ndiyo ukweli.
 
Yaani Marehemu anabaki kuwa na Katibu!???...shida sana Tz..niliwahi pokea application moja ikiwa na recommendation letter na muhuri wa katibu wa Nyerere.siku shortlist aisee
 
kp02022015.jpg
 
Katibu wa Nyerere kwa miaka yote alikuwa ni huyu mama wa kizungu, msitake kudanganya uongo usio na mpango, huyo mnaesema labda alikuwa tarishi wa Nyerere, Nyerere hakuwahi kumuamini Mwaafrika mwenzake kuwa katibu wake, kwa miaka yote aliyokuwa Ikulu:



Queen Elizabeth II, J.K. Nyerere and former Personal Assistant to Nyerere, Joan Wicken
 
Itakuwa ni ajabu na aibu kuwa na Rais "MJINGA"!! Chonde chonde watanzania, TUSIWE WAJINGA KAMA LOWASA!!
 
Kama watu wameanza kuutafuta urais kwa kutaka kuwang'oa wenzao kucha baada ya fedha kushindikana wakifanikiwa kuupata urais sindiyo wategeuka ma Idi amini wa kuwakata wenzao vichwa.
 
Tanzania, tusiwe wajinga. Taarifa kama hizi, zinamwondolea moja kwa moja LOWASA sifa za kugombea hata ujumbe wa baraza la seriakli za mtaa kwa sababu ni muuaji na jambazi.

Hawa wanaomng'ng;ania lowasa na ccm. Na hawa anataka kuwatumia nawako kukubali kutumikishwa kufunikia uozo wake ni ccm. Wanaotoa vitisho kwa wasema kweli ni ccm. Walifikisha taifa letu mahala pa kuabudu rushwa, kufumbia macho uovu na kupongezana wananchi wanapofanyiwa ndivyo sivyo, ni ccm. maisha magumu kwa watanzania, yamesababishwa na ccm. Na sasa wanavyolazimisha migombea yao isiyo na sifa, ni dhahiri ccm haina uzalendo, ilishaondoka kwenye chama cha kutetea wananchi na sasa kinajibainisha ni chama cha kimafia kinachotetea mafisadi wachache kwa gharama yoyote, hakina lengo, sifa,uwezo wa kurudisha ule utanzania wetu.

NINATOA WITO KWA KILA MTANZANIA POPOTE PALE ULIPO, BILA KUJALI CHAMA DINI WALA KABILA, PIGA MBIU NA MBIO ZA KUIKATAA CCM NA MAMBO YAKE YOTE.

Wanaccm wale wa kawaida wasijidanganye. Ccm ile waliyoifahamu, ilishanyongwa na kuzikwa kimya kimya. Adui wa ccm alivaa vazi la ccm na kuendelea kumiliki ofisi za ccm pasipowao kujua. na huyu adui yao ndiye anayeendelea kumiliki maisha na akili zao kiasi ch akuwatishia, atakayetumia akili zake kufanya maamuzi afukuzwe chama!.

Ccm fukuzeni hilo zimwi mnalofuga, linawamaliza na nchi yote!.

Tuungane kulikataaa hili zimwi lililovaa uccm kwa nje huku likitumaliza sisi na vizazi vyetu. Mwenye masikio asikie.
 
Tanzania hatupo salama kabisa, sitashangaa huyo alietoa vitisho yupo na anakula bata.
 
Katibu wa Nyerere kwa miaka yote alikuwa ni huyu mama wa kizungu, msitake kudanganya uongo usio na mpango, huyo mnaesema labda alikuwa tarishi wa Nyerere, Nyerere hakuwahi kumuamini Mwaafrika mwenzake kuwa katibu wake, kwa miaka yote aliyokuwa Ikulu:



Queen Elizabeth II, J.K. Nyerere and former Personal Assistant to Nyerere, Joan Wicken

She
became his personal
assistant in 1960, two years
before he became president.
She remained his PA almost
until his death in 1999
 
Back
Top Bottom