Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Ninamfahamu vizuri Ndg. Primus Nkwera kitaaluma ni Civil Engineer. Elimu yake ni Shahada ya Pili (Masters-uzamili) ya uhandisi aliyoipatia nchini Hungary.Gazeti la Dira la jana Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo no.405,limekuja na habari inayomtuhumu Katibu Mtendaji wa NACTE,Dr.Primus Nkwera kugushi vyeti vya shahada ya uzamivu na pia gazeti limedai alisomeshwa "PHD" Afrika Kusini na serikali akafeli.
Hizi tuhuma ni nzito maana kugushi bila shaka ni jinai.Sasa baada ya gazeti kuandika hii habari,wahusika wanachukua hatua gani?
Tunaendelea kuwapima na kesho nitakuja hapa na tuhumu nyingine kuhusu Idara ya Habari-Maelezo kutoa taarifa ambayo sio ya kweli kumetea Sefue ikiwa imeandikwa na gazeti hili pia.
Kilichoandikwa kuhusu Idara hii kama ni kweli,basi itakuwa ni fursa nyingine ya kupima dhamira ya serikali katika kile kinachoitwa "kutumbua majipu".
Nitawajuza kesho jioni baada ya kumaliza mithinani(UE) leo nimebanwa sijui hata kama usingizi utakuja.
NB:
Mjumbe hauwawi.
Kabla ya kujiunga na NACTE alikuwa ni mwajiriwa wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT) kama mwalimu katika Idara ya uhandisi ujenzi (Civil Engineering Department).
Wakati akiwa Mwalimu DIT ndipo alipata fursa ya kwenda kusoma shahada ya uzamivu (PhD) nchini Afrika Kusini kwa ufadhili wa serikali ya JMT na kurejea nchini mwishoni mwa mwaka 2004. Baada ya kurudi akaanza kujiita Dk. Nkwera hadi katikati ya mwaka 2005 ndipo akabainika kuwa amefeli masomo yake ya uzamivu na hivyo hana hadhi ya kuitwa Dk.
Wakati bado yupo kwenye wimbi hilo la kuidanganya jumuiya ya DIT kuwa ni Dk kumbe akawa ameanza mipango ya kuikimbia aibu aliyojitengenezea na kwa kushirikiana/msaada wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mafunzo hapo DIT akafanikiwa kupata kazi NACTE ambapo ameendelea kuwadanganya watanzania kuwa ana shahada ya uzamivu (PhD) hali iliyopelekea kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa NACTE.
Kama aliwasilisha vyeti vya elimu ya uzamivu (PhD) ni wazi kuwa amedanganya au amegushi vyeti hivyo.