Katibu Mtendaji NACTE ajiuzulu, kufuatia tuhuma za kughushi vyeti

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Vyuo vya Ufundi( NACTE),Dr. Primus Nkwera amejiuzulu nafasi yake.

Uamuzi wa kujiuzulu kwa Dr. Nkwera ulitangazwa katika ofisi kuu za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi,Mhandisi Steven Mlote na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kuangua kilio.

Akizungumza katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote wa baraza hilo,Mlote alisema Dr. Nkwera amejiuzulu ili kulinda hadhi ya Nacte kutokana na habari iliyoandikwa na Gazeti la Dira ikimtuhumu mambo mbalimbali.

Gazeti hilo la Dira la Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo no.405 lilimtuhumu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr.Primus Nkwera kughushi vyeti vya shahada ya uzamivu baada ya kusomeshwa na serikaliAfrika Kusini na kufeli.

Mlote alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo haipaswi kushikwa na mtu mwenye tuhuma ya aina yoyote, na ametafakari na kuona ajiweke kando na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa pembeni.

"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja ya Dr. Nkwera na hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na kuongeza:

"Kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa Nacte inafahamika na kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake yanadhihirisha kuwa kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.

"Najua mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa, yuko hai na huyu bado ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua kuachana na ukatibu utendaji.

"Tutaendelea kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati mwingine lazima mkubaliane na hali hii, lakini pia endeleen kuchapakazi kwa ufanisi kama kawaida kana kwamba bado mko na Dr. Nkwera."

Kutokana na kujiuzulu kwake, Mlote alisema bodi imemteua Mkurugenzi wa Mitaala wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi hiyo wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu alivyoviacha Dr. Nkwera ni vikubwa kwake, lakini akaahidi kuendeleza yote aliyoyaacha.
 
huo ndo mfano bora kwa nchi yetu
sio akina NUNDU wao wanadai lazima wajiridhishe kwanza kama kuna wafanyakazi hewa huku wakiahidi mbele ya CAMERA wa 1390+1 watamfuta
 
Uwajibikaji wa kiwango cha juu, wanasiasa wanatakiwa kujifunza

Sana tu mkuu,nimemkubali sana huyo daktari,kajitathmini kaona isiwe tabu kaamua ang'atuke,wanasiasa wangekuwa hv,ingekuwa poa sana,aliyeweza hili alikuwa Rais mstaafu mwinyi tu alivyokuwa waziri alijiuzuru kwa kashfa iliyomkabili na ndio maana baadae akapewa shavu la urais kwa kuwa ukishajiwajibisha mwenyewe unakuwa umejitafakari vya kutosha sana kwa maslahi mapana ya wengine
 
AMEJITUMBUA?!Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! uchunguzi ukigundua ni kweli, basi arudishe na pesa za umma alizo ripiwa ada na kufeli(kama kweli) ila DIRA DUUUUUUUUUUUUUUUUUUU! Nawaopeni kama ukoma , ngoja na mimi nirisit mwaka huu maana Mh JP, ameniaidi kunipa mchongo mzito tatzo, nina F YA number maana kuwa mkurugenzi wa kitengo cha msimamizi mkuu wa VYOO vya umma lazima ujue NUMBER.
 
Wataalamu wa kiswahili wanisaide tofauti ya Kujiuzulu na kuacha kazi kama Ipo!
Mwanaume hapaswi kuwa na tabia za kususa susa-Dr.Shein
 
huo ndo mfano bora kwa nchi yetu
sio akina NUNDU wao wanadai lazima wajiridhishe kwanza kama kuna wafanyakazi hewa huku wakiahidi mbele ya CAMERA wa 1390+1 watamfuta
Nundu akiwajibishwa watasema alikuwa amebakiza dakika tatu tu kustaafu na ashaoomba kufanya hivyo wakasema asububiri teh teh!
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Vyuo vya Ufundi( NACTE),Dr. Primus Nkwera amejiuzulu nafasi yake.

Uamuzi wa kujiuzulu kwa Dr. Nkwera ulitangazwa katika ofisi kuu za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi,Mhandisi Steven Mlote na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kuangua kilio.

Akizungumza katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote wa baraza hilo,Mlote alisema Dr. Nkwera amejiuzulu ili kulinda hadhi ya Nacte kutokana na habari iliyoandikwa na Gazeti la Dira ikimtuhumu mambo mbalimbali.

Gazeti hilo la Dira la Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo no.405 lilimtuhumu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr.Primus Nkwera kughushi vyeti vya shahada ya uzamivu baada ya kusomeshwa na serikaliAfrika Kusini na kufeli.

Mlote alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo haipaswi kushikwa na mtu mwenye tuhuma ya aina yoyote, na ametafakari na kuona ajiweke kando na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa pembeni.

"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja ya Dr. Nkwera na hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na kuongeza:

"Kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa Nacte inafahamika na kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake yanadhihirisha kuwa kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.

"Najua mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa, yuko hai na huyu bado ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua kuachana na ukatibu utendaji.

"Tutaendelea kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati mwingine lazima mkubaliane na hali hii, lakini pia endeleen kuchapakazi kwa ufanisi kama kawaida kana kwamba bado mko na Dr. Nkwera."

Kutokana na kujiuzulu kwake, Mlote alisema bodi imemteua Mkurugenzi wa Mitaala wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi hiyo wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu alivyoviacha Dr. Nkwera ni vikubwa kwake, lakini akaahidi kuendeleza yote aliyoyaacha.
Kujiuzulu tu haitoshi bali inabidi afikishwe kwa pilato
 
Bora huyu doctor of philosophy "feki" kama alifoji kajiondoa mwenyewe, jambo jema sana kuliko kusubiri utangazwe kwenye statement kwa vyombo vya habari
 
Dira ilimtuhumu huyu Nkwera au yule wa Baraza la mitihani? Nauliza tu
 
Back
Top Bottom