jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
Katibu Mkuu wa CCM(T) Msomi Dkt. Bashiru Ally anatarajiwa kuwepo katika kipindi cha TV cha Dakika 45 (ITV).
Unakaribishwa kusikia
1 - Mambo makubwa yaliyofanywa na CCM Kimataifa, kikanda, kitaifa hadi ngazi ya Kata na vijiini kwa kipindi kifupi cha miaka mitano ya Rais Magufuli.
2 - Sera na Ilani mpya ya CCM
3 - Ufafanuzi wa maswala mbalimbali kuhusu CCM na wanachama wake
4 - Muelekeo wa Kampeni
5 - Tathmini ya mapokeo ya jamii kwa Wagombea wa CCM.
Dkt. Bashiru hataropoka bali ataeleza kwa ustadi wa kisomi ndani ya Dk 45.
===
Bashiru: Tuwe na kumbukumbu, swala la kupita bila kupingwa si jipya tangu mwaka 1995. Hata ccm wanalalamika na wameweka pingamizi, na hata wao pia wamewekewa pingamizi.
Wanaolalamika wanapaswa kupeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili ya uchaguzi, hata walipokuwa wanaomba teuzi ilikuwa lazima ajaze fomu ya maadili ya uchaguzi, na fomu ya gharama za uchaguzi.
Hatukuruhusu wajaze bila usimamizi, pia waseme watatumia kiasi gani kwenye gharama za uchaguzi, na mimi nisipolishughulikia hilo nitawajibishwa ndani ya chama, kulikuwa na mafunzo kwa makatibu na wanasheria wote wakigawana maeneo kwa wajumbe wote
Matokeo, wanalalamika kabla ya kupata kipinga katika sanduku la kura.
Jinsi watakavyofanya kampeni.
Tutafuata wapiga kura nyumba kwa nyumba, tumejipanga kutangaza ilani yetu kwenye vyombo vya habari mitandao ya kijamii.
Watu unaowaona hawajaandaliwa, wamevutiwa na wanaoyaona, swala sio kulaumu bali kujifunza umekosea wapi au mwenzako mwenye nguvu anaweza wapi.
Kuhusu Hoja za Uongo
Wapinani wetu wameanza kutuchafua kwa kusema uwongo, swala sio kulalamika swala ni kujibu hoja, matarajio yetu wataanza kubadilika, tunapozungumza mmoja wa wagombea urais yupo Dubai, na kule kuna wanachama wetu wamemuona, mgombea wa kwetu yupo Geita akitoka Geita anaenda Kagera kisha ataenda Kigoma.
Sasa huyu aliyekwenda Dubai akishindwa akisema ameonewa wapiga kura watampima. Kipande kingine ni kuanzia tarehe 12 Zanzibar, tunashindanisha watu na sifa, tunashindanisha vyama, tunashindanisha rekodi kijumlisha hayo ndio unapata mitambo.
Kutumia, wasanii na kuwabeba watu na magari
Nani kasema wasiwatumie, wasanii sio watumwa, unawezaje kumbeba Diamond, Alikiba, Zuchu, Mrisho, Mpoto, wasanii ni watu wenye akili na ujuzi ukiona wameenda sehemu kuna jambo jema. Kwa taarifa yako wasanii wanajitolea.. wanafanya kazi ktk mazingira magumu, wasanii wengine wako wanatafuta kura.
Wakulima, wafugaji na wasanii wanatuunga mkono hao wote wanaletwa na malori, na hii wanayoona ni midogo iko mikutano haionyeshwi kwenye vyombo vya habari, na wao wajaribu kutafuta wasanii tuone watapata wasanii wangapi
Chama hiki kina uwezo na nguvu kubwa... fikra itikadi na falsafa.