Tatizo la CCM ni kufilisika kisiasa, kukosa mbinu mbadala za kuwaletaea wananchi maendeleo. Chama chochote kilichopoteza mvuto kwa wananachi hung'ang'ania madarakani kwa kutumia nguvu za dola. HISTORIA IMEJAA MIFANO LUKUKI. Swala si Bajeti.
Hapa CCM wanajaribu kudhoofisha CDM kwa kuwaandama viongozi wake. Nawambia CCM hata wafanyaje CDM si Mbowe wala SLAA. CDM ni ideology mbadala. Wako wakina Mbowe / Slaa wengi ndani ya CDM. Tena mshukuru kuwa hao wanapoza joto. Subiri kizazi kipya cha uongozi wa CDM kinakuja.
Kamwe nchi hii haitaendelea kuwa chaka la mafisadi, wala rushwa, wakwepa kodi, viongozi uchwara, wafanya mzaha katika mambo mazito ya taifa hili, na kadhalika. HUU NI UJUMBE KWA CCM.
CCM walianza kwa kuimba wimbo wa udini, ujimbo, eti ndio sera za CDM; WAKASHINDWA. Magamba yamewashinda sasa wanatumia mbinu za udikteta za kukamata viongozi wa upinzani. Mbinu hizo haziwafikishi popote bali ni silaha katika arsenal ya CDM. Wananchi watatoa sympathy votes. Hawa washauri wa siasa wa CCM kweli hawana kitu....
KUKAMATA VIONGOZI WA CDM hakuleti maendeleo kwa wananchi wala kuwaondolea kero zao za kukosa umeme, maji, shule, tatizo la rushwa iliyokithiri, ajira, etc. Tanzania ya leo sio ya wajinga. NDUGU ZANGU, SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA. Si siri naipenda CDM.