Katiba ya Tanzania na Sifa za wabunge

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,177
2,281
Hivi ni kweli Watanzania wanahitaji KATIBA MPYA kwa sasa?

1) Wasomi na wote wasio na maslahi binafsi na katiba. Hawa watasema ndio kwa kuangazia mambo kadha wadha ambayo yanaonekana ni chechefu. Mfano, KATIBA ya sasa ya Tanzania inazitambua sifa nyingi za mgombea nafasi ya siasa km Ubunge, Diwani, wenye viti wa mtaa/KIJIJI au balozi wa nyumba kumi kumi kubwa zaidi ikiwa ni Urai ( mgombea sharti awe Mtanzania), kuwa na miaka 18, na KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA).

Sifa zingine zinazobakia ni za ziada tu kwa mgombea.
Hoja yangu ipo hapo " Kujua Kusoma na Kuandika". Wote tunatambua kazi kuu kwa mfano ya mbuge bungeni ni kutunga sheria (ndivyo tulivyofundishwa darasani na Walimu wa Uraia -Civics, na General Study).

Swali hapa ni je Kusoma na Kuandika ni kigezo tosha cha kumfanya mtu awe msemaji wa wengi kwa dunia ya sasa? Mtu anaeingia Bungeni wala hajui nini maana ya Sheria. Mtu km huyu ataona shida kusinzia bungeni maana hajui wala hana cha kujadili na pengine kuishia kugonga meza tu.

Tanzania kitu km bunge KATIBA inawaachia hata wasio na meno wakatafune mfupa unaohitaji umakini ktk kutafuna na kumeza.

Kwa kujua tu Kusoma na Kuandika ni wazi kigezo hiki kinaenda kinyume na sera ya Elimu inayomtambua Mwanafunzi mwenye kujua Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu ( K .K. K) km mtu mwenye sifa za kuwa Mwanafunzi anaeweza kutahiniwa.

Je tunakubaliana kuwa kwa kuwa na sifa 2 za kusoma na kuandika manake ni kuwa KATIBA inatoa nafasi kwa watu wasio na sifa ya Elimu toshelezi kwa mjibu wa sera ya Elimu Tanzania? Kwa lugha nyepesi KATIBA inaruhusu hata wawakilishi ambao hawakukidhi vigezo kuhitimu elimu zao? Kwa nini sifa KUHESABU sio kigezo.

Mtu anaejua K.K anawezaje kutunga sheria itakayotumiwa na mamilioni ya Watanzania. Tena wengine ndio wanakuwa Mawaziri wanaoingia mikataba na watu wanaojua K .K .K

Maoni yangu: Elimu ya kujua tu Kusoma na Kuandika ni sifa isiyo na uhai kwa Dunia ya sasa. Angalau Elimu ya chini ianzie Form 4.

2) Wanasiasa. Hawa kwao wanachukulia mapungufu ya KATIBA ya sasa km furusa. Ukiwauliza km ibadilishwe au isibadilishwe, watasema isibadilishwe tena inafaa sana kuliko KATIBA zote Duniani na kwamba imewavusha Watanzania kwenye milima na mabonde. Utawasikia wakiweka kibwagizo kwa kusema " kwa sasa shida ya Watanzania sio KATIBA MPYA, ni maji (bila kusema maji safi), barabara( bila kusema za aina gani), umeme ( bila kusema wa namna gani), vituo vya afya ( bila kusema vitajengwaje, na vifaa pamoja na wataalamu watapatikabaje).

Mbaya zaidi kwa vile wao ni wenye sifa za K. K hutawasikia wakiongelea Elimu bora. Ikitokea ametamka neno Elimu kwa bahati mbaya hatasema elimu ya namna gani. Kwa lugha nyepesi wanasiasa hawa kwa KATIBA ya sasa ni sawa na nzi kwenye kidonda. Kidonda kinavyozidi kuoza ndio hivyo hivyo nzi huzidi kuvutiwa na kufurahi. Wao kadri KATIBA ya sasa inavyozidi kuonekana ina mapungufu ndio hivyo hivyo wanavyo zaidi kushangilia na kutetea kwa hoja zisizo anuhai. Watu km hawa ukiwambia juu ya KATIBA MPYA ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa afurahi ili anywe maji. Hawa ni watu masilahi tu sio watendaji.

3) Watu wa kawaida (wakulima, wafugaji, wenye kazi rasmi (ila sio walioajiriwa) na zisizo rasmi. Hawa hawana upande, ukisema KATIBA MPYA iwepo watasema ndio, ukisema ya zamani iendelee watasema ndio. Kwa ufupi KATIBA ya nchi kwao sio kipaumbele. Wao huona km si wahusika, si tu ktk KATIBA bali hata ktk siasa.

Huishia tu kusema " vyovyote itakavyokuwa ni sawa tu". Hawa ni watu ambao wameshakata tamaa ya maisha yao kutokana na zao la wanasiasa wa K.K.

Mwisho, Watanzania ni muda sasa kuamua kubaki na viongozi wa siasa wanaojua tu K. K au KATIBA MPYA iletwe ili kuboresha ufanisi ktk kutunga sheria na kusimamia rasilimali za nchi.
 
Back
Top Bottom