jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Mwanakijiji,Hii inaweza kuwa catch 22:
a. Kikwete akikataa kuusaini mswada huu kuwa sheria ataonekana amedharau maamuzi ya wabunge wake ambao kwa mbwembwe na vijembe waliupigia debe kuwa ni mswada mzuri.
b. Akiamua kuuweka sahihi (kitu ambacho ndio kinauwezekenao mkubwa) bila kuufanyia marekebisho atakuwa ameonekana kudharau na kukataa kabisa hoja za CDM na hivyo kuwafanya CDM waonekane mashujaa kwani ni wao waliotoa ofa ya kuomba kukutana naye na ni wao ambao hawakuchukua msimamo mkali bado na hivyo akiwakatalia CDM wataonekana wana hekima zaidi. Watasema "tumejitahidi na mmetuona lakini Rais kaweka pamba masikioni" kwa hiyo tunarudi mitaani! Well.. kila mtu kaona wamejitahidi.
c. Akiamua kuusaini na kuuridisha tena Bungeni bado tatizo litakuwa pale pale kwani hoja ya madaraka makubwa aliyonayo itajadiliwa vipi wakati wabunge wa chama chake wanaamini anastahili madaraka hayo? Ikumbukwe kuwa hata ukirudishwa haina maana hoja za CDM zitaingizwa zaidi ni kuwa zitajadiliwa na wabunge wa CCM kwa mara nyingine watapitisha mabadiliko yale yanayokifaidisha chama chao.
Lolote kati ya a,b, na c likitokea tutarudi kwenye square one!
Kama Rais anajuwa kabisa kuwa kwa hakika hatakubaliana na maoni ya CDM,then ni kwanini amekubali kukutana nao?
Ok,umezungumzia matokeo ya kama akichukuwa option b kwa upande wa CDM,lakini tumesahau kuwa na yeye ana plan yake na pia anategemea matokeo flani hata endapo atachukua option b.
Je mategemeo yake ni tofauti na hayo CDM wanayotegemea endapo "ataweka pamba masikioni"?
Je madhumuni yake ni yapi haswa kukubali kukutana na CDM huku akijuwa kuwa hatapokea ushauri wao?
Binafsi naamini mwishowe anaweza akawaambia ushauri wenu ni mzuri sana naomba muupeleke kwenye tume niliyoiunda.
Sasa sijui hiyo ndo square one ama vipi.
Naamini CDM watakachoenda kuongea nae ni kuhusu mfumo mzima na utaratibu wa kupata katiba mpya ambapo ni wazi Rais amejirundikia madaraka yote ya kwenye process ya kupata katiba mpya.
Je CDM wataenda kumwambia kuwa tumekuja hapa kusema kuwa una madaraka makubwa sana kwenye hii process na kwa hiyo jipunguzie?
Akikubaliana na maoni ya CDM,basi siasa za Tanzania zitabadilika kabisa,ni maoni yangu hapo.