Katiba: Rais Kikwete kuusaini Muswada wa Tume ya Kusanya Maoni ya Katiba kwa Kishindo!

Hii ni sehemu ya Hotuba ya JK, ukiisoma kwa makini utaona ni ndoto za alinacha kuamini kuwa atabadili uamuzi alioukwishaufanya yeye na chama chake lakini kwa kuwa Watanzania ni watu wa kuishi kwa matumaini tuendelee tu kusubiria muujiza:

Ni kutokana na hoja hizo Spika akaamua Muswada uendelee kujadiliwa na Bunge na leo Bunge limeupitisha Muswada huo. Baadae Muswada utaletwa kwangu kwa ajili ya kutiwa saini uwe Sheria. Baada ya hapo itabakia kazi yangu na Rais wa Zanzibar kuunda hiyo Tume ili mapema mwakani kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ianze. Lengo letu ni kuwa ifikapo mwaka 2014 zoezi zima liwe limekamilika ili mwaka 2015 tufanye uchaguzi tukiwa na Katiba mpya. Itapendeza tukisherehekea miaka 50 ya Muungano na Katiba mpya. Ni matumaini yangu kwamba wananchi wote watashiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yao kwa Tume hiyo.

....

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa mchakato wa kupata Katiba mpya nawasihi Watanzania tujiandae kwa maoni ya kutoa kwenye Tume ya Katiba mara itakapoanza kazi. Kwa wale ambao hawatapata walichokitaka nawaomba warudi kundini, sote tuungane kwa hatua inayofuata. Najua wanayo maoni mengi mazuri wayatayarishe na kuyawasilisha kwa Tume itakayoundwa. Njia ya maandamano na vurugu si ya busara kufuata. Haijengi bali inabomoa, haina faida bali hasara nyingi, haina faraja bali machungu kwa pande zote. Busara ituongoze sote kuchagua njia inayojenga, yenye faida, furaha na faraja kwa wote. Tutofautiane bila kupigana. Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu.

Mwisho
Ndugu Wananchi,
Naomba nimalizie kwa kuwashukuru wananchi kwa kuwa na subira kwa kipindi chote hiki toka tutangaze nia yetu ya kuanza mchakato wa kupata Katiba mpya. Kwa mara nyingine tena nawaomba mjiandae kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata Katiba mpya mara utakapoanza ili tuendelee kuijenga na kuiendeleza nchi yetu na vile vile tuendelee kuithamini na kuitunza amani ya nchi yetu.

BUNGE NA DOLA YA CHAMA TAWALA LIMEUNGANA KATIKA HILI!

Four (working) days to go!. Tarehe ya kuanza kutumika ni 1 Dec, 2011.
 
..mimi naogopa sana hizi Tume za Raisi za kukusanya maoni ya wananchi.

..mara ya mwisho kulikuwa na Tume ya Prof.Wangwe kuhusu EAC.

..baada ya tume kuwasilishwa kwa Raisi, then serikali imejifanyia kile ilichokuwa imeamua tangu awali, bila kuzingatia maoni ya wananchi.
 
Four (working) days to go!. Tarehe ya kuanza kutumika ni 1 Dec, 2011.
Inatisha... lakini still I have hope maana bunge na dola mwanzoni havikuafiki... Je ni kipi kilichowabadilisha?.. nguvu hiyo hiyo haiwezi kulazimisha tena katiba yao ikashindikana na machafuko yakaanza... sijui kama kajiuliza hilo.
 
Inatisha... lakini still I have hope maana bunge na dola mwanzoni havikuafiki... Je ni kipi kilichowabadilisha?.. nguvu hiyo hiyo haiwezi kulazimisha tena katiba yao ikashindikana na machafuko yakaanza... sijui kama kajiuliza hilo.

Two days to go!
Ni leo Jumanne na kesho Jumatano, Alhamisi Muswada ni sheria!
 
Back
Top Bottom