Katiba: Rais Kikwete kuusaini Muswada wa Tume ya Kusanya Maoni ya Katiba kwa Kishindo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba: Rais Kikwete kuusaini Muswada wa Tume ya Kusanya Maoni ya Katiba kwa Kishindo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Nov 22, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,547
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Pamoja na juhudi zote zinazofanywa kumshawishi Rais Jakaya Kikwete asiutie saini huo muswada kugeuka sheria, nawaomba niwahakikishie kwa asilimia 100% chini ya 100%, rais Jakaya Kikwete, atautia saini muswada huo kwa kishindo na mbwembwe zote zinastahiki, tena atausani mapema zaidi kuliko hata ilivyokuwa inatarajiwa!.

  At this point, nawaomba tuu wanabodi muipokee kauli hii kama taarifa tuu, nawaombeni sana msiniulize nimejuaje, wala msiniulize sababu zozote kwa sababu sitazijibu, ila eleweni tuu kuwa muswada utasainiwa!.(Nyongeza A: Rais atatakiwa kuukubali Muswada huo kabla ya kumalizika muda wa siku ishirini na moja tangu Muswada huo ulipowasilishwa kwake la sivyo basi itabidi alivunje Bunge.) Ibara ya 97 ya Katiba ya JMT ya 1977!.

  Hii inamaanisha hata juhudi za Chadema, kutaka kumuona rais, zitagonga mwamba!. Kwenye hili la mchakato wa katiba, JK hatakutana na yeyote, hatasikia chochote, si la muadhini, wala mnadi swala, na wala hata bow down kwa shinikizo lolote, toka popote na kwa yeyote mpaka kwanza autie saini muswada ule!

  Jee, lengo langu ni nini kuwapatia taarifa hii?.
  Lengo la ni dogo tuu, kuwaanda wanabodi kuubali ukweli mchungu, hivyo wanakuwa tayari kisaikolojia kuipa tume hiyo ya maoni ushirikiano unaostahili.

  Baadhi ya Watanzania wengi tumekuwa tukiishi kwenye false hopes na matokeo yake wasipopata kile walichokipata, the weak wana despair hivyo kuwa tayari kufanya lolote.

  JK alipoingia madarakani, alikuja na kauli ya "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania", hivyo Watanzania wakawa na too much expectations kuhusu yeye. Maisha ya Mtanzania wa kawaida ndio haya tunayoishi sisi, walikuwa na matumaini makubwa ya maisha bora, wameanza kukata tamaa na kielelezo ni matokeo ya urais uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Kitendo cha kuwajaza watu too much expectation wakati unaujua ukweli halisi, ni kuwapa false hopes!.

  Enzi za Nyerere, baada ya Vita vya Kagera, alitangaza miezi 18 ya watu kujifunga mikanda, hivyo kuwaandaa kisaikolojia na tulijifunga mikanda kwa furaha.

  Hivyo wale wote, wenye too much expectations kwa kudhani kuwa this time rais Kikwete atasikiliza kilio cha Watanzania kutaka kuutendea haki muswada huo, nawaombeni mjiandae kisaikolojia msije kupata frustrations na kuwa tayari kwa lolote!.

  Namalizia kwa kutoa wito, "If you can't get what you want, please take what you get"!, yaani kama umekosa kile "kingi' ulichokitaka "Muswada Bora" ambao ungezaa "Sheria Bora", ambayo ingeunda "Tume Bora ya Kukusanya Maoni", ambayo ingetupatia "Katiba Bora", basi jamani, tujiandae kupokea hicho kidogo kilichopatikana ambacho ni "Bora Muswada" ambao utatupatia "Bora Sheria" itakayounda "Bora Tume ya Kukusanya Maoni" ambayo itatupatia "Bora Katiba" naomba tuipe tume hiyo ya kukusanya maoni, ushirikiano wa kutosha ili angalau tupate hiyo bora katiba, "Something is Better Than Nothing"!

  Wasalaam

  Pasco (wa jf).

  UPDATE 1.
  Rais Kikwete amepokea Barua ya Chadema na Amekubali Kukutana Nao!

  UPDATE 2.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ndiyo maana nasema ana Kichwa cha panzi. hanaga tabia ya kutafakari kwa kina, kujua impact ya kusaini kwake. anadhani watanzania ni wajinga.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu tumekusikia na hakika hiyo TUME ya rais itapokea MAONI ya wananchi... Mnnnnnh! - maoni! na sio PINGAMIZI hivyo kinachofuatia ni yale yale muendelezo wa mama Spika wa bunge - Bora muswada ukipata sheria utakuwa bora sheria ambayo itatuletea bora katiba..
  - Shukran
   
 4. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu Pasco
  Bandiko lako lina kila dalili ya kubali yaishe! huo pia ni utaratibu mzuri katika maisha ingawa si mara zote utaratibu huu una maana hasa unapoongelea suala kubwa la kitaifa kama Katiba. Wakati huu ni muhimu rais kukumbushwa kuwa nchi yetu inafuka moshi na kila hatua inayochukuliwa na serikali inatakiwa kuwa na tahadhari kubwa kama bado wanadhani kuwa nchi yetu ni ya amani. Bongo haina tofauti na nchi zinginw nyingi duniani zinazohangaikia stability ya nchi zao leo due to matatizo ya kiuchumi yanayosababisha maisha magumu kupindukia kwa kundi kubwa la watu. Kikwete ameshikilia majani makavu na kuna watu wameshikilia kiberiti hivyo kama majani haya hayatakuwa handled kwa umani mkubwa then wenye viberiti watia moto kisha nchi itakuwa ya ajabu sana kuliko tunavyodhani. Believe me there thousands of young people who have nothing to lose and therefore ready for anything.
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Hii thread yako imepitwa na wakati kwa taarifa yako tayari amekubali kukutana na kamati ndogo ya Chadema.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hebu nifahamishe matatizo makubwa mawili ya muswada huo ukiwa kama ulivyo???
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,056
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  ..huu ushauri ungeuelekeza kwa Raisi na CCM pia.

  ..itafika mahali they may not get what they want.

  ..hopefully at that time watatusikiliza wananchi na kuweka maslahi ya taifa mbele.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Shida ni kwamba JK anataka umaarufu na mbwembwe za kusaini mbele ya makamera, bila kutumia hata muda kidogo kutafakari impact ya haraka-haraka hizo kwenye muswada ambao utagharimu katiba ya life-time ya watanzania.
  Nashindwa kuelewa rais ambaye niliamini ni mtu rational anashawishiwa na nani kuwa na haraka hizo, badala ya kutulia...
   
 9. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  sijui lini utaacha kutumika......unatumika sana pasco...hata ule mswaada ya sheria ya uchaguzi aliusaini kwa madaha hivyo hivyo ...lakini ulirudi bungeni.....
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Source???
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,056
  Trophy Points: 280
  Topical,

  ..mswada unaitambua ZNZ kama mbia sawa wa serikali ya Muungano.

  ..ZNZ ni mbia sawa na TGK siyo serikali ya muungano.

  ..mswada pia hautoi nafasi kwa wananchi kupiga kura ya maoni kama wanataka muungano ama la.

  ..muswada unaruhusu kujadiliwa kwa muungano, bila kuwepo kwa Tanganyika ambayo ni mbia wa muungano huo.

  ..vilevile mswada umempa madaraka Raisi kuteua wajumbe wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba, na zaidi Raisi ndiye anaye-set hadidu rejea za tume hiyo.

  ..ingekuwa vema angalau bunge la Jamhuri liwe na uwezo wa kuwadhibitisha wajumbe wa tume ya katiba na zaidi kuzipitia na kuziboresha hadidu za rejea za tume hiyo.

  ..mwisho mswada una VITISHO vya ADHABU YA KIFUNGO kuhusu yeyote atakayeupinga.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ikulu wametoa tamko leo jioni kuwa RAis Kikwete amekubali kukutana na uongozi wa CDM na ameagiza tarehe ipangwe haraka ili waweze kukutana. I guess baada ya mambo yanayotokea Dodoma mkutano unaweza kufanyika kabla ya mwisho wa wiki hii au mwishoni mwa wiki. Kwamba, wataweza kumshawishi asiusaini sidhani kama hilo litatokea kwani kuna implication yake kwa Rais Kukataa kusaini mswada.

  Naamini atausaini lakini bila mbwembwe ili uweze kurudishwa bungeni na kufanyiwa marekebisho. Akikataa kusaini atakuwa na nafasi moja nyingine ya kuukubali kabla hajajikuta anajiweka yeye mwenyewe na chama chake matatani.
   
 13. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  hivi wewe pasco ni wa kutuandaa sisi?? wewe huyu unatuandaa kwa lipi ambalo tulikuwa hatulijui tangu mswaada umeenda bungeni ,jk amehutubia wazee wa ccm dsm....nini hatukijui hadi uje eti unatuandaa kutoa maoni....acha kujikosha mtoto wa kiume...yeye acha asaini mbele ya kamera sisi hatuna shida ila ajue tutakutana makutano junction....yeye na katiba yake na sisi na katiba yetu....
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  a. Zanzibar kuwa mbia sawa na JMT tatizo lake nini?

  b. Hilo la kutaka kupiga kura either tunataka muungano au la ?? (tuko pamoja)

  c. Hilo la kuchaguliwa na tume kwa wajumbe sioni tatizo kwasababu ukisema iende bungeni kama kawaida ccm ni wengi na watapitishwa hata mtu kama Tambwe..

  d. Hilo la kuweka hadidu za rejea, sioni tatizo kwasababu rais ni taasisi kwasababu hata ikienda bungeni ccm bado ni wengi..
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  wazee wa dsm.
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi mkuu wa 2010 umabadilisha kabisa Tanzania. Things will never be the same na mshindi (wa siasa) ni yule tu atakayeweza kukubali ukweli na kuufanyia kazi. Kwenye huu muswada H.E Jakaya Mrisho Kikwete anatakiwa achague ama afanye maamuzi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Mwenyekiti wa CCM. Kwa maneno mengine Kikwete anatakiwa achague ama amilikishe CCM huu muswada au aufanye uwe wa watanzania wote (wafuasi wa vyama vya siasa na wale wasio wafuasi wa chama chochote).
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Unajua nini, JK asipousaini huu muswada atakuwa amewapiga goli kubwa sana la kisigino wote wale wanaomdhihaki ndani ya chama na nje..hata kama hataweka mabadiliko makubwa. Yeye anaweza tu kuchukua sababu ndogo sana ya kutosaini kisha muswada ukarudi bungeni... tik...tak... siku zinakwenda na yeye hatakuwa na makosa wala wa kulaumiwa...
   
 18. j

  jigoku JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kwa leo Pascho msukuma mwenzangu nimekunawa hata hivyo siwezi kushangaa maana yawezekana una element hizo,endelea na juhudi zako iko siku utapata unachokitafuta kwa kuonyesha dhahiri uko upande gani.Ila nashangaa unajifanya kuwaandaa watu kutoa maoni.kwa kuwa kuhesabu kunaanza na moja ndipo upate idadi ya unaotaka kuwaandaa,mimi umenikosa,wala sitaki kushawishiwa na yeyote mi siko tayari wala sitoenda kutoa maoni.Ila nimejifunza kitu kutoka kwako nimeshajua uko upande gani
   
 19. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  mwanaume anapenda sifa huyu balaa...kwa hiyo kikwete kakutuma uje usema hapa kuwa atasaini?!!! nakushangaa sana kijana wewe.....hivi kama una mtoto wako mdogo(under 15)hivi unadhani kwa katiba hii ya ccm itakayoandaliwa huyo mwanao ataikuta tanzania yenye neema baada ya miaka 30?? hivi huwa unawaza kweli na kufikili sawa sawa? jaribu kushughulisha akili yako na mawazo yako yavuke masaa ya chakula cha usiku kijana!!! ......
   
 20. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 3,173
  Trophy Points: 280
  Kwenye mkutano wake na wazee "wananchi" alisema kwa majigambo 'NITASAINI MUSWADA' nitashangaa kama atabadili mawazo at last minute. JK anahitaji msaada wa kifikra,kiroho na kiakili analipeleka taifa kwenye shimo lenye kina kirefu kutoka kwake labda Yesu atakaporudi mara ya tatu ooops mara ya pili
   
Loading...