Katiba mpya yafuta urasimu wa kutoa habari

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=2]Katiba mpya yafuta urasimu wa kutoa habari[/h]


Na Salome Kitomary



11th June 2013













wariobagasoilzenji(8).jpg

Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Warioba.


Rasimu ya Katiba iliyotangazwa wiki iliyopita imependekeza serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi, kuwajibika kutoa habari kwa waandishi wa habari.

Pendekezo hilo linatofautiana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977), ambayo waandishi wa habari walitegemea Ibara ya 18 na sheria ya vyombo vya habari katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ibara ya 30 kifungu cha (3), kinapendekeza serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi kwamba, watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao.

Aidha, katika ibara hiyo kifungu cha (1), sehemu (a) na (b) inapendekeza kila mtu kuwa na uhuru wa kutoa maoni, ikiwa ni pamoja na kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na kusambaza taarifa hizo.

“Kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji habari bila kujali mipaka ya nchi,”

Rasimu hiyo inapendekeza vyombo vya habari kuwa huru na vilevile vitakuwa na haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazopata kwa wananchi na kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.

“Masharti ya Ibara hii yatalazimika kuzingatia masharti ya sheria ya nchi itakayotungwa kwa ajili hiyo na kwa madhumuni ya kulinda usalama wa Taifa, amani, maadili ya umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine.”

Katika Katiba Ibara ya 18 sehemu (a) hadi (d), inaeleza kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake, haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi.

Pia inaeleza uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake na haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

Mapendekezo hayo yanaonekana kuwa faraja kwa waandishi wa habari nchini, kutokana na kukosekana kwa ushirikiano wa upatikanaji wa habari kutoka serikalini na kwenye taasisi zilizotajwa.

Pamoja na kuwapo kwa mapendekezo hayo, kilio kikubwa cha waandishi wa habari ni kwenye sheria ya vyombo vya habari, ambayo imepitwa na wakati na kukandamiza vyombo vya habari.






CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom