Katiba mpya: Wakati muafaka wapinzani kuungana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya: Wakati muafaka wapinzani kuungana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Dec 4, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well, ni miaka takribani 20 sasa toka Tanzania tuingie siasa za vyama vingi na sio siri kwamba matokeo bado hayaridhishi kulinganisha na nchi zingine ambazo tuliingia nazo hii system kwa wakati mmoja, nchi kama Zambia, Kenya, na Malawi. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu I mean tumejaza utitiri wa vyama vingi vya Upinzani ambavyo ni waste of our kodi, yaani vyama vya kusubiri Ruzuku na kuchumia tumbo.

  - Sasa wakati umefika wa kurekebisha Katiba, ukweli unaanza kujitokeza kwamba chama Tawala kitakuwa na final say of how to do it kwa sababu Upinzani ni hafifu sana infact ni like almost haupo, that is sad indeed kwa taifa la wananchi Millioni 50, ninasema huu ni wakati muafaka wa Chadema kuongoza the pack na kuchora chini mstari wa kuungana na Wapinzani wote nchini mlinusuru hili taifa.

  - Ninasema Chadema waongoze the pack kwa sababu wao angalau kidogo wameonyesha kuwa na Viongozi wachache ambao ni Sober, na wanaojali Taifa ambao wakipewa nafasi ya kuuweka pamoja Upinzani wa Taifa, wanaweza kutusaidia sana lakini sio wakiwa Chadema tu, it has not worked, it doesnt work, and it wont work soon. Hili taifa tufike mahali tuwe na vyama vitatu tu, viwili vikuu na Independent Party, ama sivyo tutaendelea kurudi kinyume nyume tu as if tumelogwa, huku tumejaza ma-PhDs kila sekta ya taifa!


  UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU: MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA HASA WATU WAKE!  William @..NYC,USA: Mutuz Le Baharia.
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Options zilizopo ni CCM igawanyike tupate chama kingine...

  Hayo mengine ni biashara ya familia au kanda maalum na watu maalum..

  Hakuna muungano hapo..
   
 3. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - CCM haiwezi kugawanyika bila tishio kutoka nje, so far halipo!


  William @..NYC,USA: Le Baharia!

   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa habati nzuri ndani ya mwaka tumepata picha kamili juu nani yuko upande gani. Sasa hivi tunajuwa nani yuko upande wa ccm na nani apinga ccm. Bila chenga tumeona CUF, TLP, UDP wako kweny kundi moja na ccm, na upinzani unakuwa CHADEMA & NCCR mageuzi japo NCCR nako kuna walakini lakini walau wanaonekana kuwa na rangi inayosomeka.

  Hivyo William ule ugonjwa wa mamluki unaokena kufifia na sasa tunaanza kuwa na siasa zenye kupingana kwa 'dhati'. Siafiki hata kidogo concept ya kuungana for the sake ya kuungana maana hii ndio ilikuwa salama ya CCM huko nyuma. Upinzani ulikuwa umejaa mamluki mno. Inawezekana bado mamluki wapo lakini walau wamezidiwa na naweza kusema sakata lililowakuta wale madiwa wa Arusha - CHADEMA limekuwa fundisho. Shibuda is learning the hard way.
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  CCM ikimaliza 2015 bila kugawanya itakuwa ina bahati sana..just wait..
   
 6. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu Willy,
  Umesema umemaliza!!!!!!!!!!!!! Bila vyama kuungana kuangusha chama chako ni kazi isiyowezekana kwa namna yoyote ile otherwise ccm yenyewe ibomoke kwa kishindo mfano wa KANU! Tumeona matokeo ya chaguzi zilizopita, Igunga ni mfano wa Karibu ukijumlisha kura za wapinzani wote zinashinda ccm mbali tu but nachelea kusema kuwa wapinzani wengi wako tayari kuwa vibaraka wa ccm kuliko kuungana na wapinzani wenzao kuwaletea mabadiliko watanzania. Ni wazi sasa watanzania wanataka mabadiliko ya uongozi hili pia halikwepeki so ikiwa upinzani hautaungana waBongo watataufuta mtawala mpya tokea vichakani because young generation is real tired with ccm politics and politicians
   
 7. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Taifa lina didimia mkuu, kama CCM wapo kwenye Wapinzani basi wapo kila mahali upinzani mpaka Chadema, ukiwa kiongozi unapima between taking the risk Vs matokeo kwa taifa, Chadema haiwezi kusimama peke yake ni lazima iungane na wengine mamluki watakuwepo tu siku zote ni part of life kama sio siasa, lakini ufike wakati tujiulize tumetoka wapi na tunaenda wapi? Na hasa kwenye hili la Katiba mpya tukikosea hapo tu twafwa hili taifa!

  William @..NYC,USA: Le Mutuz!
   
 8. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #8
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Tizama historia ya CCM mlo unapokuwa kwenye line wana tabia ya kumaliza tofauti zao kwa muda na kuzirudia wakisha shika power, dont be fooled in the end Lowassa atatoswa wataendelea kama kawa JK is never a fool na political games, infact good Presidents kama Clinton, siku zote wameshamiri kwa kupiganisha makundi ndani ya vyama vyao na mwsho kupata the Good solution ya vyama vyao through matokeo ya the infighting, My friend CCM will never break! na hasa kama hakuna tishio from outside kama tulivyo sasa bongo!, I mean ni maoni yangu tu!

  William @..NYC,USA: Le Mutuz!

   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Ok,
  So una maana CDM peke yao hawatoshi kuwa wapinzani,na umesema mamluki ni lazima wawepo,sasa kama ni kweli CUF,UDP na TLP ni mamluki,huoni idadi yao ni kubwa vs CDM na NCCR mageuzi?

  Kwa upande wa pili,unadhani hiyo dhana ya kina Topical kuwa CDM ni chama cha "kikanda na kifamilia" zina resonate miongoni mwa wapiga kura?
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Inategemea nini hasa tafsiri yako ya 'tishio'. Kwa mtazamo wangu kama sio 'external' threat CCM wasingejiingiza kwenye hii foleni ya party-suicide. Kuvua gamba inatokana na mambo kubwa likiwa ni kuibuka kwa kasi ya kutisha kwa CHADEMA kwenye uchaguzi uliopita. Iwe kweli au la, lakini wapo watanzania wengi wanaoamini rais wa sasa hakushinda kwenye ballot box. Situation kama hii inaleta mtafaraku ndani ya chama maana hawana uhakika 2015 wananchi watafanya nini. Hapa tulipo CCM si wamoja tena na kila kukicha wanazidi kutofautiana.
   
 11. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Unataka CHADEMA iungane na CUF? Mke wa CCM bora NCCR kuna Wabunge wenye akili.
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Thats exactly where CCJ misses?

  Ngoja tumsubiri MKJJ...
   
 13. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hata vyama vidogo na dhaifu kwa sasa vitakuwa tu kama vina misingi imara na endelevu. Swala hapa ni kuangalia maendeleo ya vyama hivi katika kipindi cha miaka mitano. Kama hakikuu, ni bora kisishiriki uchaguzi mkuu kwani ni kuweka utitiri wa vyama kwenye uchaguzi usiokuwa na tija. Na hili nigeomba liwe pendekezo katika katiba mpya. Chama kama NLD vimekuwepo tangia mwanzo wa vyama vingi, 1992, lakini vinazidi kudidimia tu. Sasa kwa nini kisifutwe?
   
 14. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #14
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well, wanasema unaponyooshea vidole wengine, kuna vidole kumi vinakunyooshea wewe mwenyewe, so ni rahisi kusema vyama flani ni Mamluki onlt kwa sababu hujui ya chama chako, somebody has to take a charge na kutafuta solution ya mamluki wahile championing the unity ya Wapinzani kwa the good of the nation, I mean we cant operate our politics or life in general under fear ya mamluki, wapo hata CCM lakini good leaders wanatafuta njia ya kuwa-accomodate while moving forward na the agenda kwa taifa lao, lakini kushindwa kulisaidia taifa kwa sababu ya fear ya mamluki does not make a sense kwa watoto wetu huko mbele ya safari ya taifa!

  - Kuhusu Chadema na Familia ishus, I know one thing, ninamjua kiongozi mmoja kijana wa CCM very good leader, aliniambia one time kwamba aliombwa kuingia huko, akawapa sharti moja kwamba awe Mwenyekiti na ni lazima sura ya chama ibadilike na kuondoa Ukaskazini, well ninamuminia sana huyu Kiongozi, anasema jamaa walimshangaa sana! ha! ha!, now I know Chadema in out, ninasema mpaka watakapolitatua hili la neno la Familia bado ni zimwi litaendelea kuwapunguzia nguvu kwa muda mrefu sana mbele ya safari kama ilivyo sasa, nilisema kwamba wakati ulikuwa umefika kwa Chadema kuwapa nafasi kina DR. Kitila na Mkuu Wangu wa Kazi Mwanakijiji, hawa wakishirikiana na Lisu, wanaweza kukisaidia chama lakini still bado unahitajika Muungano na vyama vingine! kwa maoni yangu!

  William @..NYC,USA: Le Baharia!
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Usitumie neno NEVER kwenye chama cha siasa wewe!

  CCM itameguka kwasababu kuna paradigms tatu ndani chama kwa sasa..

  Ikifika 2015 kama (watashinda of course) lakini huyo mtawala hawezi tena kuwaunganisha wana CCM wa kambi zote kama alivyofanya JK..

  Hiyo busara inapungua sana..hence kuna kundi litaondoka (detach) na hilo ndilo litasaidia taifa kuliko hivi vyama vyenye kulea undugu, ukanda na udini..
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Ina maana hata kama wakifanya hayo mabadiliko bado ni lazima tu waungane?

  Pili,nimekupata hapo pa kiogozi huyo kijana wa CCM aliyetaka kujiunga na CDM na kutaka kuwa mwenyekiti, however hilo peke yake lingeweza vipi kuondoa hayo matatizo ya ukanda na ufamilia?

  Ama is there something else i am missing?

  Ok Mwenyekiti Mbowe, Katibu Slaa, na Zitto naibu, mbona sioni ufamilia hapo?

  Ama ni yale ya wabunge wa viti maalumu?

  Ok,on the other hand,ni chombo gani chenye maamuzi ya juu kabisa cha CDM?

  Na je ni nani member wa chombo hicho?

  Kama una majina weka hapa,then we can go from there...
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hawawezi kufanya hayo mabadiliko mtasubiri sana...individual and groups interest kuondoka itachukua muda.

  Wenye chama wakiondoka duniani labda..
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu how can you operate an opposition party under assumption ya kumeguka kwa CCM? I mean katiba mpya inahitajika sasa ambayo ndio the only thing now on our National agenda kinachoweza kutukomboa hili taifa, kama Katiba haibadiliki according to the times tulizonanazo sasa we are dooomed hili taifa na Katiba haiwezi kubadilika inavyotakiwa unless kuna Upinzani mzito against chama changu, forget kumeguka bro it won't happen soma Historia ya CCM Viongozi wengi wa CCM wamejifunza namna ya kusubiri their times, na it always happens!

  William @..NYC,USA: Le Baharia!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,670
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hapo kwenye namba yenye rangi inabidi ubadilishe.
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Come on..

  John Malecela tu ndio anaweza kusubiri hata kama amesulubiwa (kimakosa au kiukweli)

  Sidhani kama hiyo tabia ina hold kwa kila mwana ccm..

  Muda utakuwa ndio determinant nzuri..
   
Loading...