Katiba mpya: Wakati muafaka wapinzani kuungana!

Kama nimefuatilia vizuri hii hoja kuna mdau ameandika kuwe na provision ktk katiba inayoruhusu at least vyama vitatu,
Hapa namuunga mkono,nadhani ni W.J. Malecela, na hii nia si kila mtu kuwa kiongozi bali kutumia kodi zetu vyema na usahihi,
Mfano: Endapo CCM itapasuka, naomba iwe hivyo, kutakuwa na CCM Mafisadi na CCM Wapambanaji, na Chama cha tatu kibaki kuwa CDM ambae ana falsafa tofauti na CCM zote hapo mbili, yaani Nguvu ya Umma.
Hapa sasa tunaweza kujenga nchi, kwanza fedha za kuhudumia vyama, ruzuku itakuwa ndogo. Lakini pia kila mtu atakuwa na pa kuegemea kama wewe si Fisadi basi ni Mpambanaji la sivyo ni Nguvu ya Umma (CDM).
Issue sasa hivi vingine CUF,DP, NCCR, nk viende wapi?
Hawa kwa mtazamo tu watasambaratika maana ni kama vinyonga hawa hawana rangi, upambanaji wanaiga, ufisadi wanajaribu na nguvu ya umma wanajikweza, kwa hiyo watakuwa absorbed naturally.
Na hapa rasilimali za nchi hazita chezewa kama hivi leo, maana CCM hawa wanajuana kwa hiyo watakemeana nje nje na kuokoa mali za NCHI lakini huku CDM ikitumia nguvu ya Umma kuendesha mambo yake hadi kieleweke.
Kupeana vyeo kiupendele, ndio kutakoma kabisa!
Ni mtazamo tu.
 
- Well, ni miaka takribani 20 sasa toka Tanzania tuingie siasa za vyama vingi na sio siri kwamba matokeo bado hayaridhishi kulinganisha na nchi zingine ambazo tuliingia nazo hii system kwa wakati mmoja, nchi kama Zambia, Kenya, na Malawi. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu I mean tumejaza utitiri wa vyama vingi vya Upinzani ambavyo ni waste of our kodi, yaani vyama vya kusubiri Ruzuku na kuchumia tumbo.

- Sasa wakati umefika wa kurekebisha Katiba, ukweli unaanza kujitokeza kwamba chama Tawala kitakuwa na final say of how to do it kwa sababu Upinzani ni hafifu sana infact ni like almost haupo, that is sad indeed kwa taifa la wananchi Millioni 50, ninasema huu ni wakati muafaka wa Chadema kuongoza the pack na kuchora chini mstari wa kuungana na Wapinzani wote nchini mlinusuru hili taifa.

- Ninasema Chadema waongoze the pack kwa sababu wao angalau kidogo wameonyesha kuwa na Viongozi wachache ambao ni Sober, na wanaojali Taifa ambao wakipewa nafasi ya kuuweka pamoja Upinzani wa Taifa, wanaweza kutusaidia sana lakini sio wakiwa Chadema tu, it has not worked, it doesnt work, and it wont work soon. Hili taifa tufike mahali tuwe na vyama vitatu tu, viwili vikuu na Independent Party, ama sivyo tutaendelea kurudi kinyume nyume tu as if tumelogwa, huku tumejaza ma-PhDs kila sekta ya taifa!


UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU: MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA HASA WATU WAKE!



William @..NYC,USA: Mutuz Le Baharia.

Samahani sana mkuu, ni kweli kabisa umoja ni nguvu, na pamoja tupo imara lakini nadhani wazo lako halitekelezeki, litabakia kama wazo la tumaini tu.

Kama unaona wazo hilo ni practicle tueleze CDM kama ulivyopendekeza iungane na vyama vipi na kwa namna gani na unategemea nini baada ya muda?
 
Kwanini sisi wananchi tusiungane then tujue tukipe chama gan nchi from the current political parties? Elimu ya uraia ndo ya kuwezesha hayo na si muunganiko wa CCM b na TLP and the rest....kama option ni kuungana na kina mrema ni bora chadema kibakie nje ya huo muungano!
 

- Well, Mushi according to the word on the street, ni kwamba 80% ya maamuzi ya CDM hufanywa na Mtei, now I am not sure how true this is, lakini mara nyingi the clout ya Ufamilia na Ukaskazini, unakatisha sana tamaa Viongozi wengi wa CCM waliochoshwa na upuuzi kuingia huko upande wa pili!

William @..NYC,USA: Le Baharia!


CDM kuwa chama cha ukanda hiyo dhana ipo hapa JF tu. Tembeeni TZ muone, wananchi wa Nyamigota au Ibutamisuzi au Nyabusozi au Bombambili hawamjui hata huyo Mtei ni nani au anatoka wapi. Wao wanajua CDM ndiyo chama kinachowatetea na ndio chama CHAO. Wanajua CDM ni Slaa, Zitto, Mnyika, Lissu, Mbowe nk. Ukiwauliza hawa viongozi wao wanatoka wapi hawajui wala hawana interest ya kujua. Mzee Mtei kama wenyeviti taifa wastaafu wengine ni mjumbe wa kamati kuu lakini mwaka mzima wa 2010 hajahudhuria kikao hata kimoja. Amebakia kuwa mshauri na hajihusishi na maamuzi ya chama. KUsema yeye anamaamuzi 80% ni kuingizwa mkenge kama JF ilivyoingizwa mkenge na propaganda za kina Kingunge na Lusinde na Akwilombe. Chama cha upinzani kipo kimoja tu, CHADEMA, wengine wote wanafadhiliwa au wameshafadhiliwa kwa namna moja au ingine na CCM ili kuipunguza kasi ya CDM. Hii imedhihiriswa wazi ktk uchaguzi za karibuni zote zilizopita. Kuungana na makundi kama haya hamna tija yoyote, siyo kwa CDM tu bali hata kwa taifa kwa ujumla.

Utitiri wa vyama unasababishwa na mapungufu kwenye katiba yetu. Katiba yetu inaruhusu vyama kuwepo hata kama havifanyi kazi yoyote ya kisiasa na hata kama vinakwenda kinyume na katiba yao wenyewe. VInasajiliwa bila hata kutimiza masharti na hii inafanywa makusudi kabisa na CCM ili wawe na vibaraka. VYama hivi vinafahamu visipofuata amri ya CCM basi Tendwa anaweza kuamriwa avifute mara moja na wakakosa mialiko ya ikulu walioizoea. Kimsingi hivi sio vyama bali ni matawi ya CCM na kusema CDM iunganie navyo wakati hakuna ajenda zinazofanana ni kutokuelewa siasa za TZ.
 

- Ni mtizamo wako tu mkuu ni kawaida kwenye Demokrasia kuwa na mitizamo mingi, wangu ni kwamba Chadema hawawezi kushindana na CCM peke yao na mfano mzuri ni huu mchezo wa Katiba mpya, kujieneza kwenye kila kona ya Taifa letu ni kazi ya miaka mingi sana mbeleni, lakini kuviunganisha vyama vyote vya Upinzani ni kazi ya muda mfupi sana, kumbuka Katiba ikipitishwa na CCM tu kama tuNAVYOELEKEA SASA hivi basi hakuna hope tena ya ukombozi.


William @..NYC,USA: Le Baharia!


CDM haiwezi na haina huwo uwezo wa kushindana na CCM peke yake lakini CDM na nguvu ya umma inaweza kushindana na inaweza kuishinda CCM. Sasa hivi huko vijijini watu waliouchoka utawala mbovu wa CCM wanaanzisha matawi yao ya CDM bila hata kujua CDM ni nini na kinasimamia nini. Wananchi waliopigika na wanaotaka mabadiliko wameungana chini ya muamvuli wa CDM. Kwao CDM sio chama bali ni ukombozi. Ukombozi utakuja na uko njiani. Ni bora tukapata katiba mpya ili mabadiliko TZ yawe ya amani. Lakini bila katiba mpya bado CCM itaondolewa, KWA NGUVU. Watu wana uchu wa kujua CDM inasema nini. Ni rahisi zaidi kuwafikia wananchi kuliko kujaribu kuunganisha "upinzani" wa Tanzania. Kuna tija kuungana na NCCR ya Kigoma lakini ni kupoteza muda kuungana na vyama vya mikobani au vyama vya majimbo kama UDP ya bariadi na TLP ya VUnjo.
 
Jembe Ulaya chonde chonde mkuu, CDM haipo sehemu nyingi Bara, Wacha Visiwani ambako haipo kabisa na Katiba ndio hiyo CCM wanaondoka nayo kwa kukosa Upinzani, tutakuja kuwaambia nini watoto wetu na haya ma PhD yote tuliyojaza hili taifa?
 
Jembe Ulaya chonde chonde mkuu, CDM haipo sehemu nyingi Bara, Wacha Visiwani ambako haipo kabisa na Katiba ndio hiyo CCM wanaondoka nayo kwa kukosa Upinzani, tutakuja kuwaambia nini watoto wetu na haya ma PhD yote tuliyojaza hili taifa?

Ukisema bara una maana gani? Si utuulize sisi tunaofanya outreach programs vijijini interior kbs! Ambapo CDM ipo na inafanya considerable well; Visiwani l agree na issue za PhD ambazo kwanza hazina study mtu aliyofanya (za kupewa) na hata kama ipo application yake ktk maisha ya mtz wa kawaida ni zero; l aggree with u!
 
Jembe Ulaya chonde chonde mkuu, CDM haipo sehemu nyingi Bara, Wacha Visiwani ambako haipo kabisa na Katiba ndio hiyo CCM wanaondoka nayo kwa kukosa Upinzani, tutakuja kuwaambia nini watoto wetu na haya ma PhD yote tuliyojaza hili taifa?

Kuna maeneo Bara ambapo CDM haipo lakini vilevile hivyo vyama vya siasa ambavyo unataka iungane navyo havipo. CDM iko vizuri sana Kigoma kwenye ngome ya NCCR, Vunjo kwenye ngome ya TLP na Bariadi kwenye ngome ya UDP. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi mkuu uliyopita. Ni kupoteza muda kuungana na vyama vingine vidogo ambavyo havina resources, havina watu wenye utashi wa kisiasa, havikubaliki, havijulikani, na havijui hata barabara ya kutokea dar kwenda vijijini ni ipi sembuse kuwahi kufika huko vijijini. Mtalumbana sana kuhusu kuungana huko na Mwisho wa siku watakuambia uwagharamie kila kitu. Watu kama wakina Dovutwa na Makaidi ambao wako kwenye payroll ya ccm na kila siku wao ni kusifia mafanikio ya JK sidhani kama wanaweza kupanda jukwaani na kuongea lugha moja wanayoiongea CDM. Na mpaka leo wako kimya kuhusu Katiba wangekuwa na hoja tungekuwa tumeshawasikia.

Visiwani hamna haja ya CDM kwenda. Mnyukano wa Katiba huko unajitosheleza, wanaopinga muswada unavyoendeshwa wapo na wanasikika na wananchi wanawaelewa.
 
Jembe Ulaya chonde chonde mkuu, CDM haipo sehemu nyingi Bara, Wacha Visiwani ambako haipo kabisa na Katiba ndio hiyo CCM wanaondoka nayo kwa kukosa Upinzani, tutakuja kuwaambia nini watoto wetu na haya ma PhD yote tuliyojaza hili taifa?
Wacha kupotosha watu wewe!!!!grow up.........nani kakwambia chadema hawako nchi nzima????we sasa umekaa marakani unasema CDM haiko sehemu nyingi bara!!!who told you??umezoea kupotosha...wala lengo lako si jema kwa chadema....wal upinzani tz....we unataka vyama viungane hata kama kuna vyama feki ili baadae vivunjike(history has proven that)........we kama una nia njema mbona usiseme CDM wajizatiti kwingineko tz???unasema CDM wana ukaskazini???what a joke you are????je ccm kwenye kuwekana watoto wa viongozi........na pia kwenye kuwekana kwa rushwa????you forget where you came from eh!!,for your info....CDM is far better and will be far far better without other so called opposition parties........unachotakiwa kuwaambia CDM(if you really care about the future of tz)ni kuhakikisha wanaandikisha wanachama wengi nchi nzima kwani ndio wapiga kura.....pia waambie viongozi wako waifanyie kazi ile tume ya uchaguzi ambayo ndio imekuwa ina determine nani awe rais wa nchi hii......kwa kufuata matakwa yenu ccm......be asured kuwa come 2015.......huu ndio mwisho wenu ccm.....kama tutakuwa tumepata katiba mpya na tume mpya ya uchaguzi..........
 
Back
Top Bottom