Mroojr
Member
- Nov 15, 2010
- 65
- 8
Kidogo kidogo kumeanza kuzuka mjadala na hoja za kutengenezwa katiba mpya Tanzania. Mjadala huu na hoja hii ianzishwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani na kujaribu kushawishi wananchi kuunga mkono hoja hii. Lakini mimi najiuliza kitu kimoja kichwani kwangu. Asilimia 90 kama sio 95 ya watanzania hatuijui kwanza katiba iliyopo. Hatuyajui kabisa yale yaliyomo ktk katiba iliyopo yanayotakiwa kuondolewa au kufanyiwa marekebisho. Tutakachounga mkono ktk katiba hii mpya ni kipi ikiwa yazamani yenyewe hatuijui! Mimi ninachoshauri mimi ni kwamba hao wanaotushawishi kuunga mkono katiba mpya wasilifanyie haraka hili waandae semina mbalimbali na warsha nyingi kuwaelisha wananchi kipi kimepitwa na wakati,kipi kiondolewe na kipi kirekebishwe ktk katiba ya zamani ndio itakuwa rahisi kwetu kuunga mkono au lah. Huo uharaka wao wa kudai katiba mpya utatutia mashaka kuwa pengine itakuwa kwa maslahi yao. Hapa nimewasemea watanzania walio wengi.