Katiba mpya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya Tanzania

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mroojr, Dec 16, 2010.

 1. Mroojr

  Mroojr Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kidogo kidogo kumeanza kuzuka mjadala na hoja za kutengenezwa katiba mpya Tanzania. Mjadala huu na hoja hii ianzishwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani na kujaribu kushawishi wananchi kuunga mkono hoja hii. Lakini mimi najiuliza kitu kimoja kichwani kwangu. Asilimia 90 kama sio 95 ya watanzania hatuijui kwanza katiba iliyopo. Hatuyajui kabisa yale yaliyomo ktk katiba iliyopo yanayotakiwa kuondolewa au kufanyiwa marekebisho. Tutakachounga mkono ktk katiba hii mpya ni kipi ikiwa yazamani yenyewe hatuijui! Mimi ninachoshauri mimi ni kwamba hao wanaotushawishi kuunga mkono katiba mpya wasilifanyie haraka hili waandae semina mbalimbali na warsha nyingi kuwaelisha wananchi kipi kimepitwa na wakati,kipi kiondolewe na kipi kirekebishwe ktk katiba ya zamani ndio itakuwa rahisi kwetu kuunga mkono au lah. Huo uharaka wao wa kudai katiba mpya utatutia mashaka kuwa pengine itakuwa kwa maslahi yao. Hapa nimewasemea watanzania walio wengi.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Wazamivu watatatuwakilisha!!elimu ya uraia yenyewe haijawafikia wananchi!wengine hawajui nini vyama vingi!!hivyo walio na huelewa wakatiba hii wanatosha kutuwakilisha!!kwakuwa kutakuwepo maoni watu watatoa maoni kama una kumbuka white paper ndo itakavyo kuwa!
   
 3. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wewe umewasilisha mawazo yako,na si ya watanzania waliowengi bana.
  Hivi unataka kuniambia watu wote[pamoja na wewe] wanaokwenda misikitini na
  makanisani kwenda kumuabudu muumba wetu, Je hao watu wote wanajua Bible na
  kuran vinaongeanini kuhusu dini zao? Hapo ulipo hujui hata kitabu cha dini yako hata
  misitari 2 na haujasema kuwa JAMANI TUSIENDE KWENYE NYUMBA ZA IBADA MPAKA
  mashekhe na wachungaji watuelimishe maandiko yote ndani ya vitabu vya mungu!
  au kwako wewe katiba ni muhimu kuliko mungu? Acha usanii wako hapa. Watanzania
  tuliowengi tunahitaji katiba mpya haraka iwezekanavyo.
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Soma hoja za Tume ya Nyarari aliyoiunda Mkapa!
   
 5. D

  DENYO JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wewe acha unafiki kwani umeingia lini jamvini hivi hujui kuna mambo mengi yanatakiwa kubadilika? Hujui kama kuna haki ya mgombea binafis imefinywa, je hujui uchakachuaji wa tume ya uchaguzi, je hujui kama watawala wako juu ya sheria?, je hujui kama principal of separation of pewers haipo tanzania? Mbunge anakuwa waziri, nini kazi ya mkuu wa wilaya wakati mkurugenzi yupo?, kwanini pccb, cag wawajibike kwa rais?, je hujui rais anao uwezo wa kuteua hata baraza la watu 200?, je hujui yote hayo??? Acha uzandiki soma ripoti ya nyalali utaelewa una point kuwae,emisha watanzania wengine lakini sio wewe ambae upo jamvini au umetumwa kama ni hivyo basi wewe sio great thinker, tafuta soft copy ipo humu jamvini ya katiba usome utaelewa.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nchi hii inavilaza wengi ndugu yangu unaweza kuzimia kwa huruma hiyo mijitu huwa tunaiacha kama ilivyo1
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Muda muafaka ukifika hata iweje lazima mabadiliko yawepo. It high time katiba mpya inahitajika ili kuleta ukombozi kisiasa, kijamii na kiuchumi katika nchi hii.
   
 8. Joyum

  Joyum Senior Member

  #8
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza tuwekea ripoti ya tume ya nyalali mkuu? Au kwa mwenye nayo pleaseeeeeeeeeeee soft copy aturushie
   
Loading...