Katiba mpya ni sawa na kupindua nchi - Nimrod Mkono

mujusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2010
237
58
Nimesoma kwenye Guardian ya leo (pg 3). Mbunge Nimrod anasema hakuna haja ya katiba mpya na kutaka kutengeneza mpya ni sawa na kutaka kupindua nchi. Anaendelea kusema " Rais, Wabunge na Viongozi wa Serikali wameapa Kuiheshimu na kuilinda Katiba na siyo kuibadili. Ninachouliza wana JF, kama wazo ndio liko hivi kweli hii Katiba ya sasa itaweza kuandikwa upya ukitilia maanani kwamba anaesema hivi ni Mbunge(miongoni wa watakaoamua kama kuna haja ya kuandika upya) na Mwanasheria maarufu hapa nchini?
 
@Jasusi...mkuu ... nimewahi kuuliza ... katika mihimili mitatu mikuu ya nchi.... ni muhimili upi unapinga kuandikwa kwa katiba mpya... na ni kwa maslahi yapi....haya Huyo ni Nimrod Mkono aliyepigwa Exile U.K na Mwalimu ... sasa anatesa
 
Ninachouliza wana JF, kama wazo ndio liko hivi kweli hii Katiba ya sasa itaweza kuandikwa upya ukitilia maanani kwamba anaesema hivi ni Mbunge(miongoni wa watakaoamua kama kuna haja ya kuandika upya) na Mwanasheria maarufu hapa nchini?
Wabunge ni watumishi wa umma hawawezi kujifanyia watakavyo hili vuguvugu la kutaka mabadiliko lipo nje ya uwezo wao.......akina Mkono ni mafisadi wakubwa .......kumbuka EPA na miradi yake pale BOT ambapo amekuwa akilipwa legal fees nje ya sheria zilizopo na hakuna wakumchukulia hatua............sana sana anatetea ulaji wake tu...........................
 
Mkono ni mmoja wa mafisadi nchini- anaogopa sana maana katiba mpya inakwenda kupindua mfumo wa ufisadi nchini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hivi siyo huyu mkono aliyetajwa kwenye Dowans???? wale wanaosubiri kuchukua fedha za wananchi bilioni 185????????????
Si heri tuwe wazi tangu mapema kwa kuwaambia mafisadi kwamba lengo la kuandika katiba mpya ni kupindiua mfumo wa mafisadi nchini-ufisadi ni unyonyaji usio na huruma kwa masikini wa Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nimesoma kwenye Guardian ya leo (pg 3). Mbunge Nimrod anasema hakuna haja ya katiba mpya na kutaka kutengeneza mpya ni sawa na kutaka kupindua nchi. Anaendelea kusema " Rais, Wabunge na Viongozi wa Serikali wameapa Kuiheshimu na kuilinda Katiba na siyo kuibadili. Ninachouliza wana JF, kama wazo ndio liko hivi kweli hii Katiba ya sasa itaweza kuandikwa upya ukitilia maanani kwamba anaesema hivi ni Mbunge(miongoni wa watakaoamua kama kuna haja ya kuandika upya) na Mwanasheria maarufu hapa nchini?

Mkuu,

Kama ni kweli amesema haya basi huyu Nimrod ni msahaulifu sana.

CCM wanasema kila siku mapinduzi daima...au vipi?
Kuna ubaya gani kama kuandika katiba mpya ni kupindua?
Ni muendelezo tu wa mapinduzi daima....tofauti ni kuwa zamu hii sio CCM watakaofanya mapinduzi, ni wananchi wenyewe...

Tuipindue tu kwa katiba mpya!!! Ni kwa manufaa ya wote.
 
usiwe na hofu, hayo ni maoni yake tu. kwa mwanasheria maarufu na mbunge hakumzuii kutofautiana maoni na wengine. take easy mpendwa, there is alwayz wayz out of anything
 
Nimesoma kwenye Guardian ya leo (pg 3). Mbunge Nimrod anasema hakuna haja ya katiba mpya na kutaka kutengeneza mpya ni sawa na kutaka kupindua nchi. Anaendelea kusema " Rais, Wabunge na Viongozi wa Serikali wameapa Kuiheshimu na kuilinda Katiba na siyo kuibadili. Ninachouliza wana JF, kama wazo ndio liko hivi kweli hii Katiba ya sasa itaweza kuandikwa upya ukitilia maanani kwamba anaesema hivi ni Mbunge(miongoni wa watakaoamua kama kuna haja ya kuandika upya) na Mwanasheria maarufu hapa nchini?
...Kwa hivyo Nimrod anataka kutuingiza darasani kwamba marekebisho ya viraka kwa katiba ni sawa na uchaguzi mkuu??
Sikutegemea mweledi kama huyu kutoa povu kama hilo
 
Nia yake hasa huyu ni ku-maintain status quo, yaani anataka tupite kulekule kwene njia waliyotegeshea mbigiri ili tuumie ili wao waendelee kufaidi keki ya taifa peke yao na vimada wao.

Matakwa ya wananchi ultimately ndio huweka misingi ya uongozi wa nchi, hakuna kilicho kikuu zaidi ya matakwa ya wananchi. Katiba sio matakwa ya wananchi na hayaezi kuwa juu ya utashi wa wananchi. Ukiona mtu anaanza kupinga matakwa ya wananchi unajua huyu hayupo kwa maslahi ya wananchi.
 
Acha nchi ipinduke licha ya kupinduliwa kwani sasa tunapata faida gani na hii katiba?mzee anajua hatima ya ufisadi wake inakaribia. BANK M anamiliki yeye mkapa na jeetu patel!
 
pamoja na kua fasadi huyu jamaa atakua na matatizo ya akili kama kweli katamka hayo maneno hadharani
 
Huyu Mkono nadhani ni miongoni mwa watu wanaoheshimika sana lakini walio very myopic wasioona mbali. Sasa kama wananchi wameona kuwa katiba tulonayo haiwafai iweje huyu jamaa atwambie kuwa ni uhaini? Bahati mbaya najiheshimu ningemtukana matusi huyu bwana!
 
The government is installed by the people, and the people's power have power to changes they way they want to be ruled.
 
Nimesoma kwenye Guardian ya leo (pg 3). Mbunge Nimrod anasema hakuna haja ya katiba mpya na kutaka kutengeneza mpya ni sawa na kutaka kupindua nchi. Anaendelea kusema " Rais, Wabunge na Viongozi wa Serikali wameapa Kuiheshimu na kuilinda Katiba na siyo kuibadili. Ninachouliza wana JF, kama wazo ndio liko hivi kweli hii Katiba ya sasa itaweza kuandikwa upya ukitilia maanani kwamba anaesema hivi ni Mbunge(miongoni wa watakaoamua kama kuna haja ya kuandika upya) na Mwanasheria maarufu hapa nchini?

tatizo ni Jogoo la mjini likiingia shamba..... kazi kweli kweli...... mkono ni gwiji la ufahari na umimi.... za mwizi arobaini....
 
haya Huyo ni Nimrod Mkono aliyepigwa Exile U.K na Mwalimu ... sasa anatesa
Dah, aisee huyu Nyerere alifaa kuwa candindate wa PhD ya heshima hata kama amekufa! Alikuwa anaona mbali sana. Yaani wale aliowakataa ndio wengi wao wanatuharibia nchi!
 
pamoja na kua fasadi huyu jamaa atakua na matatizo ya akili kama kweli katamka hayo maneno hadharani

sio yeye tu na wengine wakijani kama mijuc.... me nawaona hawana akili na wamefanya ujinga wa maskini ndo mtaji wao.... Wanachaguliwa ili wawakomboe wao wanawageuza vitega uchumi.....

Ctabiri na cwatakii mabaya ila hawa kwa mungu i cant get a picture...
 
Back
Top Bottom