Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,926
- 31,169
Heri ya X Mass.
Tunamshukuru Mungu kwa siku kuu ya leo,na kwa namna ya kipekee kabisa nawapongeza waKristo wote Tanzania na Duniani.
Wakati bado tunaendelea kusheherekea siku hii muhimu naomba tuwarejeshe katika mjadala wa mchakato wa KATIBA MPYA.
Ni hakika KATIBA ya sasa ina mapungufu mengi na tena imepitwa na wakati.
Ukitazama STRUCTURE ya Katiba utaona imejikita katika KUMSIKILIZA,KUMTII,KUMWABUDU,KUMSIFU,KUMNYENYEKEA RAIS wa JMT.
Si vibaya RAIS wa JMT akatengenezewa utaratibu wa kiMungu Mungu tatizo kubwa ni kwamba RAIS wa JMT ni mwanadamu mwenye mapungufu mengi.Akitumia vibaya katiba watu wengi wataumia sana tena sana.Hakuna mahali pa kupinga maamuzi mabaya ya RAIS.Akiamu kutuingiza katika vita tutaingia,akiamua kukwapua fedha za wananchi nje ya utaratibu wa sheria atakwapua hakuna wa kumzuia,akiamua kuingiza jeshi mtaani kutandika wananchi asiowapenda hakuna wa kumkatalia.Viongozi wote wanaapishwa kumtii Raia na si katiba.
Hakuna tatizo iwapo Rais atakuwa malaika lakini kama ni hawa watawala mapenda madaraka hakika sioni Tanzania ikipiga hatua za maana.
KATIBA MPYA ni muhimu sasa kuliko wakati wowote Mwl alituachia katiba mbaya ni wajibu wetu wote kuhakikisha KATIBA MPYA itakayopunguza madaraka makubwa ya RAIS.Itakayo hakikisha uhuru wa Mahakama,Bunge na tume ya uchaguzi.
Ngongo kwasasa KIBANDA MAITI.