Katiba Mpya na Ukimya wa Wazanzibari

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Wakuu,
Kati ya watanzania ambao walikuwa concerned sana na suala la Katiba Mpya walikuwa Wanzanzibari!
Lakini siku zinavyozidi kusonga hawa wenzetu wanazidi kunywea! Je,
1. Walipata walichokuwa wanataka?
2. Warioba anawafanyia kazi ambayo walitakiwa waifanye?
3. Ni delay tactic?
4. Baada ya kutimuliwa Mwanasheria Mkuu wao waliogopa?
5.....
Tujadili zaidi!
 
Wamepata walichokuwa wanakitaka.
 
Wasemee wapi?? Tungojee BW tuone watasemaje? Yawezekana kuwa wanajua kuwa kule waliitiwa kujichotea za mwisho mwisho wa ccm kwani wanajua kuibadili katiba ya Zenj si mchezo hivyo yoote hayo hayapiti hata limoja tu acho hayo mengi.
 
Wakuu,
Kati ya watanzania ambao walikuwa concerned sana na suala la Katiba Mpya walikuwa Wanzanzibari!
Lakini siku zinavyozidi kusonga hawa wenzetu wanazidi kunywea! Je,
1. Walipata walichokuwa wanataka?
2. Warioba anawafanyia kazi ambayo walitakiwa waifanye?
3. Ni delay tactic?
4. Baada ya kutimuliwa Mwanasheria Mkuu wao waliogopa?
5.....
Tujadili zaidi!

...kama mtu hukubaliani na kitu, kunyamaza kimya ni silaha isiyoonekana (an invisible weapon), hususani unapokuwa unaujua udhaifu wa upande wa pili..
 
Jamani..Jamani...Jamani..
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni "wakindungu" kwanza nadhani watu inawezekana hawaelewi au wanapotoshwa na hata ukisoma rasimu ya warioba hajazungumzia nchi bali serikali tatu naona wachangiaji wanaingiza hisia mambo ya wazanzibar na Tanganyika yanatokea wapi. Sio lazima tuige ulaya huu ni aina ya muungano wetu ambao hats mabeberu yanaushindwa.
$@#tujengeTanzania@#$
 
"Yanaushindwa".......,kiswahili kibovu cha kupigiwa mfano....wakati bado unao kajiunge na kisomo cha watuwazima
 
Kwa upande wa zanzibar saivi tumebakia kujiandaa na kuilinda katiba ya zanzibar tu hatuwezi kushindana na wanaotumia nguvu sisi ni kidogo sana,elimu ya makongamano ni kukumbushana tu kwa zanzibar kwa sababu siasa inaeleweka vizuri sana hapa na mbinu za viongozi wa tz(tanganyika) zinaeleweka vyakutosha hapa.
sote tumejionea jinsi ya bunge lilivyokwenda ni aibu tupu,na kura zilivyopigwa,kwa hio yale yalikuwa maamuzi yao na sio maamuzi ya kisheria kama ilivyotarajiwa kuwa.

sasa nijibu baadhi ya maswali ya mtoa mada

1. je Walipata walichokuwa wanataka?
katika mchakato wa katiba kwa zanzibar tulitaka mkataba wengi wetu na katika mtazamo mzima wa saisa za tanzania zanzibar tunataka kuwa na hadhi na heshima kama nchi mshirika wa muungano na pia uwezo wa kufanya maamuzi yanayohusu muungano yaani kuwa na say katika muungano kwa kiwango cha sawa kwa sawa na mshirika mwenzetu tanganyika bila ya kuangalia ukubwa au wingi wa watu hizi ni nchi na sio muungano wa makundi ya watu.
jawabu hapa ni bado ubeberu wa tanzania unaendelea,na hakuna kilichopatikana kwa zanzibar ila ni tricks na dharau tu.
2. Warioba anawafanyia kazi ambayo walitakiwa waifanye?
mimi bin nafsi yangu kama mzanzibari namshukuru sana nd.warioba na watanganyika wote ambao wana mtazamo wa haki na sheria,na anavyofanya mzee warioba ni wajibu wa kila mmoja kuelimisha na kuamsha watu ili kukaa katika mstari wa haki na sheria,wale ambao wanamuona warioba anawafanyia kazi wazanzibari wafikiri upya ya kuwa nchi hii inaelekea kwenye uongozi wa kidictator na itaathiri kila mtu,serikali ikianza kupinda sheria hadharani bila ya kujali ni sawa na kula nyama ya mtu na ni hatari sana,mwisho wake ni udictator tu na haya yanaanza na rushwa ambayo imepindikia. na itaathiri kila mmoja wetu regardless of political affiliation
jawabu ni nd.warioba anatimiza wajibu wake

3. Ni delay tactic?
jawabu ya hili hakuna delay tactic,wazanzibari tumeshtushwa sana na matukio ya bunge la katiba,kwa sababu mambo yaliyofanywa pale zamani yalikua yakifanywa kwa siri na ndani ndani lakini kuona sasa kima kakosa miti anarukia kila mtu inashtua kwa kweli
tunaangalia mustakbali wa katiba ya zanzibar tu ndio ngao kwa sasa

4. Baada ya kutimuliwa Mwanasheria Mkuu wao waliogopa?
zanzibar hakuna khofu ya aina hii kabla ya kufkuzwa mwanasheria alifukuzwa mansour na kabla ya mansour wako walitishwa na kufkuwa pia wengi tu na wengi wamepoteza maisha zanzibar yote hayo na mengine hayatoondoa uzanzibar maisha,ni kupoteza wakati na mapesa tu,
wakati tanzania in 2014 bado inajikita kuandaa mbinu za kisiasa kuendelea kuidhibiti zanzibar na/ili kuwafanya raia wake kama mazombi wasiweze kufkiri kenya na rwanda zinaondoka kimaendeleo,juzi nimeona plan 2040 ya rwanda its impresive,hapa bado tunaruhusu siasa za kikoloni.
jawabu hapa ni kuwa kwa zanzibar haitatokea siku ya kuacha kutetea haki iwapo haki na sheria hazitatawala.

asanteni na wale wanaofikiri tafauti msinielewe vibaya i wish things could have been different in different circumstances but its seems as thou politics is our biggest challenge so far,its lack of imagination that keeps us back in old colonial days and here we will stay unless we find the right way
 
Waswahili wanasema kimya kingi kina mshindo mkubwa.

Wazanzibari tumenyamaza lakini sio kama ndio tumenyamaza kuhusiana na 'katiba ya ccm'.

Katiba pendekezwa tutaipa HAPANA kwa wingi sana kuhakikisha ya kuwa kwa Zanzibar (unguja + Pemba) haipiti.

Endapo CCM wataipitisha kwa mabavu kama walivyolazimisha theluthi tatu za Zanzibar basi hapo haitakuwa ndio mwisho ila tutawaekea RED LINE ambayo CCM kwa nguvu zao zote hawatathubutu kuvuka.

RED LINE hapa nakusudia katiba ya ZANZIBAR. Wao CCM watataka irekebishwe jambo ambalo litahitaji kupigiwa kura ya maoni, na Wazanzibari walio WENGI watakataa kwa kuweka HAPANA.

Na mwishowe katiba pendekezwa kwa Zanzibar haitapita, Wazanzibari wapo kimya kwa sababu weshajua nini la kufanya wakati ukiwadia.
 
Wafanye midahalo kama ya wana-UKAWA!

Buchanan;
Wana UKAWA hawatangazi katiba mpya. Wanawafungua watu macho, wanatutoa tongotongo tulokuwa tumelala. Leo tumeamshwa na kelele za wapiga baba zao, babu zao. Atii, tusifunguliwe macho tuzidi kulala usingizi wa pono.
Twasema, kumekucha. Uwepo mdahalo, usiwepo mdahalo lakini kile kitendo cha Mtanganyika kupewa Uzanzibari na kiongozi wa CUF aliyeapa kwa kilio kuwa hajapiga kura ili tu akidi itimie tumpitishe huyo Mwana.haram kimetuamsha kuwa kuna jambo.
Midahalo au hakuna, mapesa yalotengwa kuwapumbaza wananchi huku hospitali hazina madawa na mashule hakuna ilimu yatosha kuitangaza. Atakaye ikubali Mola wake atamhukumu mwenyewe
 
Hata mimi nilikuwa nasema kuwa Wazenj wawatoe watu "tongotongo" kama zipo, kama vile wanavyofanya wana-UKAWA!
 
Waswahili wanasema kimya kingi kina mshindo mkubwa.

Wazanzibari tumenyamaza lakini sio kama ndio tumenyamaza kuhusiana na 'katiba ya ccm'.

Katiba pendekezwa tutaipa HAPANA kwa wingi sana kuhakikisha ya kuwa kwa Zanzibar (unguja Pemba) haipiti.

Endapo CCM wataipitisha kwa mabavu kama walivyolazimisha theluthi tatu za Zanzibar basi hapo haitakuwa ndio mwisho ila tutawaekea RED LINE ambayo CCM kwa nguvu zao zote hawatathubutu kuvuka.

RED LINE hapa nakusudia katiba ya ZANZIBAR. Wao CCM watataka irekebishwe jambo ambalo litahitaji kupigiwa kura ya maoni, na Wazanzibari walio WENGI watakataa kwa kuweka HAPANA.

Na mwishowe katiba pendekezwa kwa Zanzibar haitapita, Wazanzibari wapo kimya kwa sababu weshajua nini la kufanya wakati ukiwadia.
Mkuu,
Mkiikataa Katiba inayopendekezwa si tunabaki na Katiba ya sasa? Au mnafikiri kutakuwa na Rais mwenye huruma kama JK akauendeleza huu mchakato?
 
Waswahili wanasema kimya kingi kina mshindo mkubwa.

Wazanzibari tumenyamaza lakini sio kama ndio tumenyamaza kuhusiana na 'katiba ya ccm'.

Katiba pendekezwa tutaipa HAPANA kwa wingi sana kuhakikisha ya kuwa kwa Zanzibar (unguja + Pemba) haipiti.

Endapo CCM wataipitisha kwa mabavu kama walivyolazimisha theluthi tatu za Zanzibar basi hapo haitakuwa ndio mwisho ila tutawaekea RED LINE ambayo CCM kwa nguvu zao zote hawatathubutu kuvuka.

RED LINE hapa nakusudia katiba ya ZANZIBAR. Wao CCM watataka irekebishwe jambo ambalo litahitaji kupigiwa kura ya maoni, na Wazanzibari walio WENGI watakataa kwa kuweka HAPANA.

Na mwishowe katiba pendekezwa kwa Zanzibar haitapita, Wazanzibari wapo kimya kwa sababu weshajua nini la kufanya wakati ukiwadia.

Kimya kingi kina mshindo. Na hata Tgk wanalijua hilo kwani dhwahir shahir waZnz wamelionyesha katika kura za Bunge la Katiba la Mh Sitta.

Sasa waZnz wanasubiri kura ya maoni ya kuipitisha/ kuikataa katiba hiyo.
nafikiri huko wa Znz watachinja bila huruma.

Tuvute subra

Mkipiga kura ya hapana tunarudi kwenye Katiba ya Mwaka1977, maisha yanakwenda tu, no problem!!
 
Back
Top Bottom