MWAKA 2023: Mwaka wa Tafakuri na Katiba Mpya - 3

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Hali ngumu ya maisha inayosababishwa na mfumuko wa bei za bidhaa masokoni,wazo la katiba mpya litatawa mwaka 2023 nguvu kutoka kwa wananchi,trade unions,NGO'S,wataalamu wa elimu ya siasa na uraia na vyama vya upinzani bila kusahau Media za Tanzania.Tunaweza ku-adopt mapendekezo yaliyokwishatolewa huko nyuma,tuna mapendekezo kutoka tume ya Nyalali, Shivji na Jaji Kisanga na rasimu ya Jaji Warioba,ripoti zote hizi zilianisha kwa kina matatizo ya katiba yetu na mapendekezo ya kufanyika,uwezi kuniambia leo Mbowe atakuja na mapendekezo tofauti na yale yaliyopo kwenye hizo tume zilizoongozwa na watu wenye vichwa vyao.

-Yapo Mambo ya Muungano yalijadiliwa vyema kwenye rasimu ya pili ya katiba mpya ya Jaji Warioba.

Rasimu II ya katiba mpya - SEHEMU YA KWANZA
JINA, MIPAKA, ALAMA, LUGHA NA TUNU ZA TAIFA

Ibara ya 1

Ibara ndogo ya (1).
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi na Shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964, zilikuwa nchi huru.

Ibara ndogo ya (2).
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na dini.

Ibara ndogo ya (3).
Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika ibara ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo.

Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni: (a) eneo lote la Tanzania Bara, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari ambalo kabla ya Muungano lilikuwa likiitwa Jamhuri ya Tanganyika pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka; na (b) eneo lote la Zanzibar, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari ambalo kabla ya Muungano lilikuwa likiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka,Wananchi wanahaki ya kufahamishwa ilikuwaje jina Tanganyika likatoka na Zanzibar likabaki,Au Tanzania bara likaanza na tanzania visiwani halikuanza?

Tunu za Taifa 5. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaenzi na kuzingatia Tunu za Taifa zifuatazo: (a) lugha ya Kiswahili; (b) Muungano; (c) utu na udugu; na (d) amani na utulivu.

Je utoaju wa haki na kuenzi uwajibikaji sio tunu ya kutamaniwa? Nilidhani kuwa tukiwa na na tunu, kuzienzi pia kufuatane na kujenga tunu zitakazotupeleka mbele hasa vizazi vijavyo.
Katiba au mchi itakayoenzi na kupigania haki na uwajibikaji ndio yenye dalili ya kusonga mbele.
Nchi yetu iko mbioni kupoteza tunu ya amani, haki, uwajibikaji, lugha, utulivu n.k. ni muhimu sana kuziwekea mbele.
Ni aibu sana kiongozi kutokuwa na hisia ya kufungwa kuwa na hizi tunu.
Lazima mtanzania uweke mbele muungano, haki kwa wote, lugha, amani utulivu na uwajibikaji.
Huo ndio uzalendo.
Nadhani hii ni omission kubwa kimaadili kutoa uwajibikaji na utoaji wa haki katika tunu za taifa.

-Sababu zinazokwamisha katiba mpya.

1.Wananchi kutegemea vyama vya siasa na wanasiasa ili kufanikisha madai ya katiba mpya jambo ambalo ni gumu kwa namna fulani.
Kutokana na sababu mbalimbali wanasiasa wanaweza kuchelewesha madai ya katiba mpya kutokana na kuwa na harakati zisizo na mwendelezo kutokana na kuendekeza maslahi yao binafsi na ya vyama vyao,mfano ikitokea Mwanasiasa anae tegemewa kuongoza kampeni ya madai ya katiba mpya akateuliwa kuwa kiongozi katika wadhifa fulani Serikalini ni wazi kuwa atapunguza nguvu katika harakati.

2.Hofu ya chama kilichopo madarakani kupoteza madaraka inaweza kuchangia kuchelewa kwa mchakato wa katiba mpya,kama CCM inaamini mchakato wa katiba mpya unaweza kuiondoa madarakani basi ni wazi kuwa inaweza kuwa sababu ya kuchelewa kwa mchakato.

3.Kukosekana kwa umoja baina ya makundi mbalimbali ya vyama vya siasa, wananchi na serikali juu ya mchakato wa katiba mpya kwakua kila kundi linavutia upande wake bila kuangalia maslahi mapana ya taifa kwa maendeleo ya kizazi kilichopo na kijacho.

4.Ukosefu wa elimu ya msingi juu ya katiba na masuala mbalimbali kuhusu mifumo ya utawala,demokrasia na haki za binadamu ambapo wananchi hawawezi kuchukua hatua na kutekeleza wajibu wao,kila mtanzania anasubiri yamkute ndio aulize hii nayo vipi nani aliiweka kwenye katiba ya Tanzania!?

Nimalizie kwa kusema,sisi sote ni waathirika wa mfumo mbaya wa siasa zetu,sasa basi tusiwaambie wapinzani tu wadai katiba,ni jukumu letu sote,nchi zote zilizofanikiwa kupata katiba nzuri za nchi zao haikudaiwa na wapinzani pekee,mfano wa karibu kabisa ni wenzetu wa Kenya,walioongoza na wanaoendelea kudai mabadiliko ya katiba Kenya ni ongozi wa dini,Civil Society Orgnisations,vijana,vyuo Vikuu halafu ndo wanakuja vyama vya siasa,tatizo letu ni pale tunapofikiri kuwa tatizo fulani si tatizo mpaka pale litakaponiathiri mimi,lazima tubadilike,kwa kawaida wanasiasa wa kiafrika hawaoni mbali zaidi ya madaraka,tukiwaachia wapinzani kudai katiba peke yao hawatadai zaidi ya tume huru ya uchaguzi,naamini tatizo la katiba ni kubwa kuliko tume huru ya uchaguzi.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
wazo la katiba mpya litatawa mwaka 2023 nguvu kutoka kwa wananchi,trade unions,NGO'S,wataalamu wa elimu ya siasa na uraia na vyama vya upinzani bila kusahau Media za Tanzania.
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Naunga mkono hoja,
P
 
Back
Top Bottom