Lazima tuchemshe bongo zetu tuone ni vipi elimu ya uraia-katiba itafikishwa hadi vitongojini ili wa-Tanzania wote waelewe, wajadili na kisha wachangie katiba wanayoitaka. Jadili Katiba Tanzania programme ni mradi umebuniwa na Tanzania Gender Accountability (TAGA); Women and Law East Africa-Tanzania na Rights Action Watch, kupeleka elimu ya katiba vitongojini ikiwanlenga wanawake na vijana. Kuwafikia wakina mama vijijini kunahitaji hatua zaidi ya kugawa nakala za Katiba ya sasa. Hapa jukwaani tumeonge sana na wengi wetu tumeelimika kiasi kwamba tukiulizwa tunataka nini kiwemo kwenye katiba mpya, na mchakato uwe vipi, tunaweza kusema kwa uhakika. Inabidi sisi wote tunaochangia humu kila mmoja achukue hatua ya kuto elimu ya katiba kwa ndugu, marafiki na jamaa zetu vijijini na mijini.