Katiba mpya itampa kura Lissu

Katiba mpya itampa kura Lissu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,255
Reaction score
16,185
Katiba yetu inahitaji kuandikwa upya kwakuwa Ina kasoro nyingi sana na viraka vingi. Uandishi wake umeshatafuna hela zetu nyingi Sana lakini hatukufika mwisho kwenye awamu ya 4 na haitaandikwa upya kwenye awamu ya 5 ingawa rasimu ipo. Na inavyoonekana hakuna Rais kutoka CCM atapenda iandikwe upya kwakuwa ya Sasa Ina manufaa makubwa kwa Rais na kwa CCM.

Hata Kama watu hawaipendi Chadema au hawampendi Mh. Lissu lakini wanapenda katiba mpya imaliziwe kuandikwa.
Wako watu ambao Wanaweza kuichagua Chadema ili kazi ya kuiandika katiba ikamilike.

Katiba Ikishakamilika miaka 5 ijayo watu wataamua upya chama kipi chenye sera safi za kiuchumi, kijamii na zinazoliunganisha Taifa na watu wake kiongoze nchi.

Kwenye ilani ya CCM hakuna kifungu kinachogusia kumalizia kuiandika upya katiba, hivyo hawataandika katiba. Ila Chadema na ACT Wazalendo wako wazi kwenye Ilani zao kuwa uandishi wa katiba mpya Ni kipaumbele Chao.

Samahani Kama Kuna mtu nimemkera lakini katiba ndio moyo wa taifa.
 
Katiba yetu inahitaji kuandikwa upya kwakuwa Ina kasoro nyingi sana na viraka vingi. Uandishi wake umeshatafuna hela zetu nyingi Sana lakini hatukufika mwisho kwenye awamu ya 4 na haitaandikwa upya kwenye awamu ya 5 ingawa rasimu ipo. Na inavyoonekana hakuna Rais kutoka CCM atapenda iandikwe upya kwakuwa ya Sasa Ina manufaa makubwa kwa Rais na kwa CCM.

Hata Kama watu hawaipendi Chadema au hawampendi Mh. Lissu lakini wanapenda katiba mpya imaliziwe kuandikwa. Wanaweza kuichagua Chadema ili kazi ya kuiandika katiba ikamilike. Ikishakamilika miaka 5 ijayo watu wataamua upya chama kipi chenye sera safi za kiuchumi, kijamii na zinazoliunganisha Taifa na watu wake.

Kwenye ilani ya CCM hakuna kifungu keep nachokusia kumalizia kuiandika upya katiba, hivyo hawataandika katiba.

Samahani Kama Kuna mtu nimemkera lakini katiba ndio moyo wa taifa.
Hata mimi naenda kumpa kura lengo ni katiba mpyaa tuu
 
Wanachofeli upinzani ni kuwaelezea wananchi kwamba katiba ni nini
Naamini kuna watu wengi tu wanasikia katiba, katiba lakini hawelewi ni nini na inafanya vipi kazi kwa hiyo wanachukulia Ni Jambo la kawaida tu
 
Watu wa hivyo wanapungua Sana nchi, hasa baada ya kila kata kuwa na shule ya sekondari. Kwenye somo la Civics Kuna mada ya KATIBA, hii inawafanya wawe walimu wazuri kwa wazazi wao, shangazi na babu zao kuhusu katiba na umuhimu wake. Ahsante Sana shule za kata pamoja na mapungufu yake lakini zinasaidia kuandaa wapiga kura madhubuti hata kwenye ngazi ya Kijiji kuliko ilivyokuwa zamani.
 
Hata mkimpa TL kura zenu 100 x 3000 hazitasaidia kitu kwani Tume sio huru sasa hapo atapenya vipi? fikiria kuwa mnacheza mpira na mnataka kufunga magoli ili upate ushindi kwani mmewazidia nguvu wapinzani mara mnaona na kutambua kuwa goli lote limezibwa kwa geti kubwa sasa hapo utaupitisha mpira wapi ili uhesabu kuwa ni goli?

Kwa mwendelezo wa matukio yaliyopo na yanayokuja ni ndoto tu za mwendawazimu anayeweza kuamini kuwa ktk hali hiyo bado ushindi utakuwepo acha sie wengine tusubirie kuona watu wakibambikiwa kesi za Tume ya uchaguzi hiyo tarehe 28
Mmmh! Mtu atafanya kosa kubwa Kama ataendelea kuubeza uwezo wa watanzania. Watanzania wa leo sio Kama wale wa awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu na awamu ya 4. Kwanza hebu ona aina ya mgombea wa Chadema wa awamu hii ya tano lugha anayotumia kwenye kampeni, Ni lugha mpya kabisa kwa watanzania, lakini Ni lugha ambayo Vijana wengi wanailewa Sana na wanamuelewa kile anachomaanisha.

Mazingira na maisha wanayokulia Vijana wetu yanawalazimisha wamuelewe Lissu, wako tayari kumsubiri afike hata Kama amechelewa sana kufika, wako tayari kumchangia hela ya maji kutoka kwenye hela yao ya bodaboda, mamalishe, na genge. Vijana Ni Kama wanemwagiwa mafuta ya petrol tayari wanasubiri tume ivute sigara.

Kama Kuna kosa kubwa tume ya uchaguzi italifanya Ni kufanya Kama unavyosema wewe kwenye uchaguzi huu.
 
Watanzania kwa sasa wanataka amani, elimu bure,vitambulisho vya machinga ,miundo mbinu ya kitosha,afya bora, maji safi umeme wa uhakika nk.watanzania hawaba demand ya katiba.waonataka katiba ibadilishwe ni wale wenye uchu wa madaraka wanatamani vifungu fulani viondolewe au vibadilishwe ila wao iwe rahisi kuingia madarakani, sasa hao ni wachache mno. Wengi wetu tunahitaji hivyo nilivyo taja hapo juu na jpm anelaendelea kuvitoa kwa wanainchi kwa kasi ya 5g.
 
Korosho mlilipa au 5g ya lumumba tu

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Watanzania kwa sasa wanataka amani, elimu bure,vitambulisho vya machinga ,miundo mbinu ya kitosha,afya bora, maji safi umeme wa uhakika nk.watanzania hawaba demand ya katiba.waonataka katiba ibadilishwe ni wale wenye uchu wa madaraka wanatamani vifungu fulani viondolewe au vibadilishwe ila wao iwe rahisi kuingia madarakani, sasa hao ni wachache mno. Wengi wetu tunahitaji hivyo nilivyo taja hapo juu na jpm anelaendelea kuvitoa kwa wanainchi kwa kasi ya 5g.

Peleka utopolo wako huko lumumba
 
Hata wanaccm watampa Lisu kura. Wameona madhara ya madaraka makubwa ya rais. Akina Nape, Membe, Kinana, Ngekeja, Makabas, Kikwete, Dr. Kafumu, Vicky Kamata, Shyrose Bhanji, e.t.c
 
Siasa ni Sayansi
Uchaguzi ni Hisabati
Hisia & mihemuko & maoni & Uongo & Uzushi & ,matarajio hayatoi Matokeo chanya Kwenye Uchaguzi
 
Bila Lissu tutajuta zaidi kwa mfalme kubali mifumo rasmi " atake asitake..."
 
Watanzania kwa sasa wanataka amani, elimu bure,vitambulisho vya machinga ,miundo mbinu ya kitosha,afya bora, maji safi umeme wa uhakika nk.watanzania hawaba demand ya katiba.waonataka katiba ibadilishwe ni wale wenye uchu wa madaraka wanatamani vifungu fulani viondolewe au vibadilishwe ila wao iwe rahisi kuingia madarakani, sasa hao ni wachache mno. Wengi wetu tunahitaji hivyo nilivyo taja hapo juu na jpm anelaendelea kuvitoa kwa wanainchi kwa kasi ya 5g.
Kwa kupuuza katiba Magufuli anataka twende kama tulivyo na raisi wa nchi hii aendelee kuwa mungu mtu anaejua kila kitu. Nitakacho mimi ni tuwe na mifumo endelevu na taasisi (institutions) zenye nguvu-check and balances. Mifumo bora ya utawala ni muhimu kwa maendeleo yetu. Matumizi ya pesa za maendeleo zisitegemee matakwa ya mtu mmoja. Hivyo basi kura YANGU nitampa Lissu bila kupepesa macho kwa sababu anaona mbele zaidi ya madaraja, ndege etc.
 
Hata wanaccm watampa Lisu kura. Wameona madhara ya madaraka makubwa ya rais. Akina Nape, Membe, Kinana, Ngekeja, Makabas, Kikwete, Dr. Kafumu, Vicky Kamata, Shyrose Bhanji, e.t.c
Hata Rais Kikwete ameumizwa Sana, amekejeliwa kupita kiasi hadi kukosa Cha kufanya. Mimi nashangaa Sana kuona JK anasema endeleeni
 
Siasa ni Sayansi
Uchaguzi ni Hisabati
Hisia & mihemuko & maoni & Uongo & Uzushi & ,matarajio hayatoi Matokeo chanya Kwenye Uchaguzi
Uko sawa mkuu, tatizo letu tukisema "uchaguzi ni hisabati" tunajumuisha kupindisha mambo, kutokuwa wawazi, kuiba kura,na kupindua matokeo.
 
Kwa kupuuza katiba Magufuli anataka twende kama tulivyo na raisi wa nchi hii aendelee kuwa mungu mtu anaejua kila kitu. Nitakacho mimi ni tuwe na mifumo endelevu na taasisi (institutions) zenye nguvu-check and balances. Mifumo bora ya utawala ni muhimu kwa maendeleo yetu. Matumizi ya pesa za maendeleo zisitegemee matakwa ya mtu mmoja. Hivyo basi kura YANGU nitampa Lissu bila kupepesa macho kwa sababu anaona mbele zaidi ya madaraja, ndege etc.
Kuwalazima watu maendeleo sio sawa, hakuna anaepinga ndege au reli kujengwa lakini sio badala ya mishahara, Uhuru wetu wa kujieleza na uhai wetu. Twende polepole kwa pamoja tutafika tu huku mihili yote ya dola (serikali, bunge, mahakama na media) ikiendelea kufanyakazi zake kwa ufanisi na rasilimali zetu zikitumika vizuri. Hatutaki atokee mtu mmoja au kikundi afikirie kwa niaba yetu. Tunataka bunge huru lifikie na liamue kwa niaba yetu.
 
Watanzania kwa sasa wanataka amani, elimu bure,vitambulisho vya machinga ,miundo mbinu ya kitosha,afya bora, maji safi umeme wa uhakika nk.watanzania hawaba demand ya katiba.waonataka katiba ibadilishwe ni wale wenye uchu wa madaraka wanatamani vifungu fulani viondolewe au vibadilishwe ila wao iwe rahisi kuingia madarakani, sasa hao ni wachache mno. Wengi wetu tunahitaji hivyo nilivyo taja hapo juu na jpm anelaendelea kuvitoa kwa wanainchi kwa kasi ya 5g.
Nimetamani. Kukupa jibu kubwa sana lkn sijui ww unaumri gani.mungu.nisamehe kwa majibu niliokua nimewaza kumpa kiumbe huyu ambaye simfahamu
 
Watanzania kwa sasa wanataka amani, elimu bure,vitambulisho vya machinga ,miundo mbinu ya kitosha,afya bora, maji safi umeme wa uhakika nk.watanzania hawaba demand ya katiba.waonataka katiba ibadilishwe ni wale wenye uchu wa madaraka wanatamani vifungu fulani viondolewe au vibadilishwe ila wao iwe rahisi kuingia madarakani, sasa hao ni wachache mno. Wengi wetu tunahitaji hivyo nilivyo taja hapo juu na jpm anelaendelea kuvitoa kwa wanainchi kwa kasi ya 5g.
Amani na utulivu Ni vitu viwili tofauti, wewe unamaanisha nini Kati ya hivyo 2?
 
Kwa kupuuza katiba Magufuli anataka twende kama tulivyo na raisi wa nchi hii aendelee kuwa mungu mtu anaejua kila kitu. Nitakacho mimi ni tuwe na mifumo endelevu na taasisi (institutions) zenye nguvu-check and balances. Mifumo bora ya utawala ni muhimu kwa maendeleo yetu. Matumizi ya pesa za maendeleo zisitegemee matakwa ya mtu mmoja. Hivyo basi kura YANGU nitampa Lissu bila kupepesa macho kwa sababu anaona mbele zaidi ya madaraja, ndege etc.
Mko wachache
 
Back
Top Bottom