Katiba mpya itaiondoa CCM madarakani kwa sababu zifuatazo. Hata mstaafu Kikwete aliona ndio maana akaitia kapuni

Katiba mpya itaiondoa CCM madarakani kwa sababu zifuatazo. Hata mstaafu Kikwete aliona ndio maana akaitia kapuni

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,170
Reaction score
8,622
Chaguzi za rais ,wabunge na madiwani zitakuwa huru. Sababu tume ya uchaguzi itakuwa huru.Wizi wa kura utadhibitiwa.

Mahakama zitakuwa huru, sababu majaji watakuwa wanaomba kazi hawatakuwa wateule wa rais.

Kesi zinazohusu uchaguzi zitakuwa huru na upendeleo utakoma.

Viongozi waliofanya uafisadi watafikishwa mahakamani hata na raia binafsi. Sio mpaka Takukuru au Dpp afungue kesi.

Ndio maana CCM hawaitaki katiba mpya. Wanaogopa sana kaka mtoto anavyoigopa pilipili kichaa
 
CCM kwa miaka nenda sasa wanatutawala kimabavu kwa msaafa wa Katiba yao mbovu ya mwaka 1977. Katiba hii imekuwa ni msaada kwao kwenye kuwapa ushindi, na pia kwenye kudhibiti taasisi zote muhimu ndani ya nchi vikiwemo vyombo vya dola.
 
Katiba itakayoundwa itakuwa ya hovyo kama jinsi ilivyo hiyo inayoitwa tume huru.
 
CCM kwa miaka nenda sasa wanatutawala kimabavu kwa msaafa wa Katiba yao mbovu ya mwaka 1977. Katiba hii imekuwa ni msaada kwao kwenye kuwapa ushindi, na pia kwenye kudhibiti taasisi zote muhimu ndani ya nchi vikiwemo vyombo vya dola.
Exactly
 
Wanakwambia katiba haileti maji wala Umeme wala barabara kumbe ni Uoga wa kuogopa kwenda jela baada ya katiba kuwatoa madarakani
 
Kama wakibadili katiba basi mali za vigogo zitakua hatarini tukianza na
Jk
Samia
Mkuu wa usalama wa taifa wa sasa
Mali za marehemu mkapa
Afu tunamalizia na zanzibar sasa kule kwa mwinyi nadhani wote watanyoongwa vibaya
 
Kwani Nepal wameweza kuuondoa uongozi mbovu madarakani kwa baada ya katiba mpya?mnaweza mkawa na katiba mpya na bado ikasiginwa tu,jambo kubwa ni waTanzania kujitambua kiakili na kujua nini haki zao.
 
Hii katiba ni tamu kwa chama tawala,,,kama chadema ingefanikiwa 2015 ingekua ni katiba tamu kwao, na ninaamini wasingekua na haraka ya kuibadilisha.
 
Back
Top Bottom