Mtu wa Mungu
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 444
- 19
1) Katika miaka yake mitano ya kwanza imedhihirika kwamba si yeye anayeongoza serikali yake bali kundi la wachache-mafisadi, ambao hawana utaifa ndani yao hata kidogo;
2)Mafisadi hawa, kupitia kwa mmoja wao aliye na nguvu kubwa ya fedha na mtandao mkubwa wa sheria kimataifa hivi majuzi tu amesema kwenye vyombo vya habari kwamba kuandikwa katiba mpya ni kupindua serikali; ni dhahiri kwamba mafisadi hawa watateka mchakato na kuupeleka kwenye mgogoro badala ya kusudio la taifa hili;
3) Chombo pekee chenye uwakilishi wa wananchi wote ni bunge; Katiba ni sheria mama; kama Kikwte ana utashi wa kisiasa juu ya hoja hii, basi kwenye kikao cha bunge cha Februari 8, 2011, waziri wake wa sheria awasilishe msuada wa kuandikwa katiba mpya, na bunge liridhie na kutunga sheria ya kuongoza mchakto wote ikiwa ni pamoja na hadidu za rejea-pamoja na time frame-ndipo sasa kila sekta na jamii nzima iweze kuelewa na kushiriki ipasavyo;
4) Msimamo wa waziri wa sheria Kombani na na mwanasheria mkuu Mrema unapinga dhana nzima ya kuandikwa katiba mpya; kuwakabidhi watu hawa hawa kusimamia mchakato ni kuwadanganya watanzania; kama si kuwahadaa
mkuu.... ninawasiwasi na hili..... kwani CCM inawabunge zaidi ya 70% EL na RA wakiamua kutumia influence basi hoja hiyo haitapita kwa kupitia bunge.... mimi nadhani kama hiyo constitution review commission itakuwa independent na sio presidential basi zoezi litakwenda vizuri tu
wakifanya hivyo upinzani unaweza hilazimisha jamii idai referendum ya katiba mpya kwa madai ya kuwa ni haki yetu.mkuu.... ninawasiwasi na hili..... kwani CCM inawabunge zaidi ya 70% EL na RA wakiamua kutumia influence basi hoja hiyo haitapita kwa kupitia bunge.... mimi nadhani kama hiyo constitution review commission itakuwa independent na sio presidential basi zoezi litakwenda vizuri tu
Kuna msamiati 'mafisadi' unaotumika ovyo ovyo inasemekana baadhi ya mafisadi ni wanasiasa, viongozi wa kijamii na hata wa dini lakini matokeo ya uchaguzi unaonyesha baadhi ya watu waliotuhumiwa mafisadi wameshinda vizuri ubunge na udiwani, Je wananchi waliowachagua ni mafisadi? Kwa maana kuwa fisadi kwa watu wa hai ni kila mwana ccm na fisadi kwa watu wa monduli ni kila mwanachadema....hii ndio tafsiri yake ...!
Ama sivyo dhana ya ufisadi ni kupakaziana tu..enzi zile za Mwalimu kila tajiri hapa nchini alitambulika kuwa mwizi na anapotaka uongozi wa siasa alikuwa lazima apigwe chini....!
Wasomi mmzeua balaa la mmoja hapa anasema nchini ilikuwa inaongozwa na mafisadi miaka mitano iliyopita ..mimi napingana na hilo huyo aliyeandika aseme wazi wazi kuwa ndani ya serikali kulikuwa na viongozi ana mashaka nao kwa utajiri wao, elimu yao au kule wanakotoka... neno ufisadi au fisadi linatumika kuziba dhana ya unyanyapaa wa kisiasa ambao umezalishwa na upinzani na hasa chadema... maana nafahamu katika chadema kuna viongozi matajiri je nao ni mafisadi... !
Unyanyapaa huu uliovishwa koti la ufisadi utatupeleka pabaya afadhali muwe wa wazi ....kuwa sisi hatumpendi kiongozi huyu kwa vile hatoki kwetu... au sio wa dini yetu...ufisadi...enzi za awamu ya kwanza kulikuwa na kashfa ya 'lord rajpar' ..tulikuwa na unga wa mahindi ya njano 'mwanayanga ..watu walikuwa wanavaa magunia...mkokoteni hata kama umebeba taka zilizowekwa katika gunia ulikimbizwa watu wakidhani ni mchele au mahindi...sasa nimetanabahi kuwa...akili nyingi huondoa maarifa.....
Wengi hamna lolote hamna utaalam, weledi wala uvumilivu wa kisiasa....fitina , vitimbi ndio mvijuavyo tu...! Wengi mlioko sasa mngewahi kuzaliwa haki ya Mungu tusingefanikiwa kupata uhuru mapema..... naona tungepata uhuru siku mayote nayo itakapoachiliwa na ufaransa...!
Nashangaa fisadi fisadi siku huyo mtuhumiwa akialika shajara waandishi habari kibao tv zote zinakava shughuli yake sasa fisadi yeye au sisi ....! natarajia katiba mpya itafuta neno ufisadi ambalo maana halisi ni tabia ya kiongozi fulani aliyekuwa akigombea urais akabwagwa...yaani fisadi ni mwanamume anayepora wake wa wenzake...! Mtu anayetumia nafasi ya uongozi au marafiki zake viongozi huyo ni mbadhirifu na tapeli! neno linalofaa zaidi tungesema hatutaki viongozi matapeli, wabadhirifu na wababaishaji...
Katiba mpya iwamulike kwa kuweka vigezo vya kuwatambua na kuwaumbua...mfano kuwepo kipengele kama katiba ya Urusi ambapo wapiga kura 25 wanaweza kufungua shauri la kumuachisha ubunge 'to recall' mtu asiye na uwezo yuko bungeni anasinzia tu na kujishughulisha na ufataki na ubazazi..! teheheee..!
Aidha waislamu wamejipanga kuhakikisha makosa yaliyofanyika miaka 60 ambapo katiba ilichezewa na kuwaondolea mahakama ya kadhi inarejeshwa katika katiba mpya kama ilivyo kenya ambapo waislamu ni kidogo sana... ukilinganisha hapa nchini ni nusu au zaidi kuliko manasara.
'Wakristu'! inasemekana sheria nyingi ni za Kijorjian au za Kikiristu zinazotawala dunia ...mapumziko Jumamosi na J2 nikuwapa wakristo wa kisabato na wengin e kuabudu hili halionekani kuwa ni upendeleo limezoeleka na kuwa kama sheria ..! sheria zinazotawala dunia nyingi zina ushawishi wa kikiristu uliotokana na utawala wa kirumi walipogeuza imani ya kikiristu kuwa ndio rasmi ya utawala wao na wale waliokuja baadae kuendesha dola...si mnajua vatican inatambulika kama nchi lakini hapa nyumbani tukisema Zanzibar ni nchi inakuwa nongwa...
Nasema katiba mpya njoo utamu kolea....!
kuna msamiati 'mafisadi' unaotumika ovyo ovyo inasemekana baadhi ya mafisadi ni wanasiasa, viongozi wa kijamii na hata wa dini lakini matokeo ya uchaguzi unaonyesha baadhi ya watu waliotuhumiwa mafisadi wameshinda vizuri ubunge na udiwani je wananchi waliowachagua ni mafisadi kwa maana kuwa fisadi kwa watu wa hai ni kila mwana ccm na fisadi kwa watu wa monduli ni kila mwanachadema....hii ndio tafsiri yake ...
Bunge ni mhimili wa dola unaofanya kazi kwa niaba ya wananchi. Hoja binafsi ya katiba mpya imewasilishwa bungeni, na huko ndiko kutaundwa baraza la kutunga katiba, na watakaofanya hivyo ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wawakilishi wao bila kuingiliwa na Serikali. Na ni huko pia ambapo makundi mbalimbali ya jamii yatashirikishwa katika mchakato wa kuandikwa katiba mpya na USHIRIKI huo hautakuwa kwa hisani ya RAIS Kikwete kupitia wateule wake.
Tunampongeza kwa KUKUBALI KATIBA MPYA.
Lakini si kazi ya Kikwete na wala Serikali yake, ni kazi ya Bunge, ni kazi ya Wananchi wa Jamhuri ya Tanzania.
Sidhani kama ni sahihi kwa Rais Kikwete kuunda tume, na sidhani kama ni njia sahihi ya kupata katiba mpya tunayoitaka. Huku ni kuteka nyara hoja ya watu, hii si kazi yake, hatukumtuma! President Kikwete and his Constitutional Review Commission should stay far aside and let the people of the United Republic of Tanzania decide their destiny kupitia BUNGE.
I think it worth to say boldly to him, NO, but NO THANK YOU!
Kuhusu hoja binafsi sitashangaa kale kamama kakiikataa eti Kiwete kashaunda tume maalum ya katiba mpya!