KATIBA MPYA: Hongera Kikwete kwa kukubali lakini mchakato usimamiwe na Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KATIBA MPYA: Hongera Kikwete kwa kukubali lakini mchakato usimamiwe na Bunge

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mtu wa Mungu, Jan 1, 2011.

 1. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa Watanzani wenye mapenzi mema na nchi hii, habari kwamba rais Kikwete amekubali kuandikwa katiba mpya, hizi ni habari njema!!!

  Ila, kama ana utashi wa kweli wa kisiasa juu ya jambo hili muhimu sana, na la kihistoria kwa yeye binafsi na taifa hili, asiachie mchakato kusimamiwa na serikali yake; mashaka yangu, na huenda ya wengi ni kwamba:-

  1) Katika miaka yake mitano ya kwanza imedhihirika kwamba si yeye anayeongoza serikali yake bali kundi la wachache-mafisadi, ambao hawana utaifa ndani yao hata kidogo;

  2)Mafisadi hawa, kupitia kwa mmoja wao aliye na nguvu kubwa ya fedha na mtandao mkubwa wa sheria kimataifa hivi majuzi tu amesema kwenye vyombo vya habari kwamba kuandikwa katiba mpya ni kupindua serikali; ni dhahiri kwamba mafisadi hawa watateka mchakato na kuupeleka kwenye mgogoro badala ya kusudio la taifa hili;

  3) Chombo pekee chenye uwakilishi wa wananchi wote ni bunge; Katiba ni sheria mama; kama Kikwte ana utashi wa kisiasa juu ya hoja hii, basi kwenye kikao cha bunge cha Februari 8, 2011, waziri wake wa sheria awasilishe msuada wa kuandikwa katiba mpya, na bunge liridhie na kutunga sheria ya kuongoza mchakto wote ikiwa ni pamoja na hadidu za rejea-pamoja na time frame-ndipo sasa kila sekta na jamii nzima iweze kuelewa na kushiriki ipasavyo;

  4) Msimamo wa waziri wa sheria Kombani na na mwanasheria mkuu Mrema unapinga dhana nzima ya kuandikwa katiba mpya; kuwakabidhi watu hawa hawa kusimamia mchakato ni kuwadanganya watanzania; kama si kuwahadaa;

  5) Katiba Mpya ni Tanzania Mpya!! Katiba ya sasa ya mwaka 1977 (wakati CCM imezaliwa) ni ya chama kimoja cha CCM; kimantiki, CCM hiyo hiyo ambayo tayari imeonesha kuingiwa na tabia ya Taliban ya Afganistan, haiwezi hata kidogo kuongoza mchakato wa kuunda na kupatikana katiba ya kweli-CCM sasa hivi si ile ya 1977 hata kidogo!!!!!!!!!!!!!!!(hata ingekuwa mimi ndiye CCM na serikali yake!!!!!!,yaani watengeneze kisu kikali cha kukata vichwa vyao??????!!!!!!)
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu.... ninawasiwasi na hili..... kwani CCM inawabunge zaidi ya 70% EL na RA wakiamua kutumia influence basi hoja hiyo haitapita kwa kupitia bunge.... mimi nadhani kama hiyo constitution review commission itakuwa independent na sio presidential basi zoezi litakwenda vizuri tu
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu you are absolutely right, wasiwasi wako ni very genuine. Kama ikifanyika blunder nyingine ya kuwaachia wanasiasa mchakato wa kuandika katiba mpya, itakuwa mkenge kuliko wa sasa. Katiba yetu itakuwa pingu kwa watanzania, na si mwongozo wa kutuletea maisha mazuri.

  Ajabu ni kwamba issue ya katiba ilishajadiliwa siku nyingi hakuna jipya, wanaojifanya kuzungumzia sasa wanarudia yale tuliyofanya mwaka 2000-2002. Wakati wa utawala wa Mkapa iliandaliwa white paper, maoni ya watu yalikusanywa na kila kitu kipo kwenye vitabu. Mkapa na wenzake walikataa mapendekezo yale kwa kuwa yalikuwa yanawabana na kuwawajibisha zaidi kwa taifa lao, wakatoa kisingizio kuwa yalikwenda nje ya hadidu za rejea, wengi tulijua kuwa ulikuwa uongo.

  It is just a matter of going through reports za tume ya Nyalali, Bomani na Warioba, kuna mengi kwenye ripoti za tume hizo yameelezwa kuhusu katiba. Walifanya mchakato wa kitaalamu kukusanya na kuchambua maoni hayo, hawakuwa laymen na hawakutumia uswahili kufanya kazi ile.

  Kuna wataalamu wengi tu wa sheria wenye uzalendo kwa Tanzania na wanaowakilisha maoni ya watanzania wanaoweza kufanya kazi hii kwa niaba ya watanzania, kuliko wabunge na wanasiasa. Habit ya kuwa-entrust wanasiasa na kila kitu na kuwafanya semi-Gods ni kuendelea kutuweka watanzania na kuiweka Tanzania hatarini.

  Tunaweza hata kutumia mifano ya katiba za nchi zenye hali inayofanana na Tanzania kuchukua mifano ya kuandaa katiba yetu, kuliko kuwaaachia wanasiasa kazi hii. Tukumbuke kuwa Tanzania ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 40, ni sehemu ndogo sana ya watu hao ni wanasiasa. Hata wabunge wenyewe wana mengi ambayo hawafahamu kuhusu katiba, not good idea at all to put all our eggs in that basket.

  Si kweli kuwa Bunge pekee ndio mwakilishi halali wa maoni ya watanzania (bunge letu kwa sehemu kubwa linalinda maslahi ya CCM na wabunge wenyewe, si ya wananchi na si ya Tanzania, kuna mifano mingi tu) moja ya malalamiko makubwa ni kuwa kuna watanzania tunaopenda wanasiasa, vyama vyao na wabunge wabanwe na katiba mpya. Wawe na wajibu zaidi kwa Tanzania na waliowachagua na si kwao wenyewe na vyama vyao kama ilivyo sasa.

  Si busara hata kidogo kuwaacha wao tu waandike katiba mpya, au wa-dominate mchakato wote wa kuandaa katiba. NI afahdari tuwe kwenye process ya miaka mitano kuandika katiba kwa kuwashirikisha watu wenye uwezo wa kujua mahitaji ya Tanzania na watanzania, kuliko kuharakisha na kuwa na katiba kama ya sasa au mbaya zaidi.
   
 4. M

  Mkatamiti Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna msamiati 'mafisadi' unaotumika ovyo ovyo inasemekana baadhi ya mafisadi ni wanasiasa, viongozi wa kijamii na hata wa dini lakini matokeo ya uchaguzi unaonyesha baadhi ya watu waliotuhumiwa mafisadi wameshinda vizuri ubunge na udiwani, Je wananchi waliowachagua ni mafisadi? Kwa maana kuwa fisadi kwa watu wa hai ni kila mwana ccm na fisadi kwa watu wa monduli ni kila mwanachadema....hii ndio tafsiri yake ...!

  Ama sivyo dhana ya ufisadi ni kupakaziana tu..enzi zile za Mwalimu kila tajiri hapa nchini alitambulika kuwa mwizi na anapotaka uongozi wa siasa alikuwa lazima apigwe chini....!

  Wasomi mmzeua balaa la mmoja hapa anasema nchini ilikuwa inaongozwa na mafisadi miaka mitano iliyopita ..mimi napingana na hilo huyo aliyeandika aseme wazi wazi kuwa ndani ya serikali kulikuwa na viongozi ana mashaka nao kwa utajiri wao, elimu yao au kule wanakotoka... neno ufisadi au fisadi linatumika kuziba dhana ya unyanyapaa wa kisiasa ambao umezalishwa na upinzani na hasa chadema... maana nafahamu katika chadema kuna viongozi matajiri je nao ni mafisadi... !

  Unyanyapaa huu uliovishwa koti la ufisadi utatupeleka pabaya afadhali muwe wa wazi ....kuwa sisi hatumpendi kiongozi huyu kwa vile hatoki kwetu... au sio wa dini yetu...ufisadi...enzi za awamu ya kwanza kulikuwa na kashfa ya 'lord rajpar' ..tulikuwa na unga wa mahindi ya njano 'mwanayanga ..watu walikuwa wanavaa magunia...mkokoteni hata kama umebeba taka zilizowekwa katika gunia ulikimbizwa watu wakidhani ni mchele au mahindi...sasa nimetanabahi kuwa...akili nyingi huondoa maarifa.....

  Wengi hamna lolote hamna utaalam, weledi wala uvumilivu wa kisiasa....fitina , vitimbi ndio mvijuavyo tu...! Wengi mlioko sasa mngewahi kuzaliwa haki ya Mungu tusingefanikiwa kupata uhuru mapema..... naona tungepata uhuru siku mayote nayo itakapoachiliwa na ufaransa...!

  Nashangaa fisadi fisadi siku huyo mtuhumiwa akialika shajara waandishi habari kibao tv zote zinakava shughuli yake sasa fisadi yeye au sisi ....! natarajia katiba mpya itafuta neno ufisadi ambalo maana halisi ni tabia ya kiongozi fulani aliyekuwa akigombea urais akabwagwa...yaani fisadi ni mwanamume anayepora wake wa wenzake...! Mtu anayetumia nafasi ya uongozi au marafiki zake viongozi huyo ni mbadhirifu na tapeli! neno linalofaa zaidi tungesema hatutaki viongozi matapeli, wabadhirifu na wababaishaji...

  Katiba mpya iwamulike kwa kuweka vigezo vya kuwatambua na kuwaumbua...mfano kuwepo kipengele kama katiba ya Urusi ambapo wapiga kura 25 wanaweza kufungua shauri la kumuachisha ubunge 'to recall' mtu asiye na uwezo yuko bungeni anasinzia tu na kujishughulisha na ufataki na ubazazi..! teheheee..!

  Aidha waislamu wamejipanga kuhakikisha makosa yaliyofanyika miaka 60 ambapo katiba ilichezewa na kuwaondolea mahakama ya kadhi inarejeshwa katika katiba mpya kama ilivyo kenya ambapo waislamu ni kidogo sana... ukilinganisha hapa nchini ni nusu au zaidi kuliko manasara.

  'Wakristu'! inasemekana sheria nyingi ni za Kijorjian au za Kikiristu zinazotawala dunia ...mapumziko Jumamosi na J2 nikuwapa wakristo wa kisabato na wengin e kuabudu hili halionekani kuwa ni upendeleo limezoeleka na kuwa kama sheria ..! sheria zinazotawala dunia nyingi zina ushawishi wa kikiristu uliotokana na utawala wa kirumi walipogeuza imani ya kikiristu kuwa ndio rasmi ya utawala wao na wale waliokuja baadae kuendesha dola...si mnajua vatican inatambulika kama nchi lakini hapa nyumbani tukisema Zanzibar ni nchi inakuwa nongwa...

  Nasema katiba mpya njoo utamu kolea....!
   
 5. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  wakifanya hivyo upinzani unaweza hilazimisha jamii idai referendum ya katiba mpya kwa madai ya kuwa ni haki yetu.
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  kusema kweli jk hakuwa na jinsi ila kukubali katiba mpya...deep down jamaa anaumia sana!!!
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  u have a point somewhere, lakini baada ya kuchanganya sana basi hata maana yenyewe imepungua kabisa. Yaani hata wewe bado huji nini maana ya UFISADI? are u madam speaker? who are u?
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli..... hivi asilimia kubwa ya watanzania na wapiga kura wengi wao wakiwa ni ktoka vijijini ni watu wa aina gani .... ni walala hoi....nini maana ya mlala hoi.... si yule maskini ambaye hulala hoi akijiuliza kesho atakula nini..... sasa fisadi akija wakati unafikiri utakula nini kesho halafu akakupa mlo wa siku moja ili umchague jibu lake ni nini..... si ndio umekuwa kiongozi kwa ufisadi wa kutoa rushwa..... mbona unawatusi wananchi walala hoi ndugu yangu..... au na wewe umekua brain washed....... ufisadi ni syndicate .... na hauna huruma ..... wala hauna dini ila una itikadi..... na hupitia vyama vya siasa kama .....?
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwa hili tunakushukuru na kukupongeza JK basi twasubiri kwani ahadi ni deni siku zote.
  Ndugu Wananchi;
  Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani
  Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao.

  [FONT=Palatino Linotype, serif]Baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwa kufanyiwa maamuzi. Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika.[/FONT]

  [FONT=Palatino Linotype, serif]Ndugu Wananchi;[/FONT]
  [FONT=Palatino Linotype, serif]Ni matumaini yangu kuwa mchakato huo utaendeshwa vizuri, kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya nchi yetu na mazoea yetu ya kujadiliana bila kugombana. Wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na pawepo kuvumiliana kwa hali ya juu pale watu wanapotufautiana kwa mawazo. Pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana. Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema. Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa.[/FONT]

  [FONT=Palatino Linotype, serif]Nawaomba Watanzania wenzangu wenye maoni yao wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huu. Katoeni maoni yenu mazuri yatakayowezesha nchi yetu kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa yetu ya sasa na ya miaka 50 ijayo. [/FONT]
   
 10. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  President Jakaya Kikwete said yesterday Tanzania needed a new constitution to march with the country's 50 years of nationhood.

  In his end-of-the year address to the nation, Kikwete said: "We, in the government, have agreed to lead the process for the constitution review in order to come up with a document that accommodates the current dynamics and developments."

  He said in fast-tracking the process he had formed a special Constitutional Review Commission. He said the body, which is led by the Attorney General, comprises members from different groups from both sides of the union - Zanzibar and Mainland.

  According to the president, the commission has been tasked to oversee the constitutional review processes by collecting views of social groups, political parties, business people, civil societies, religious organizations and experts.

  After collecting stakeholders' inputs, he said, the commission will give its recommendations which will be forwarded to the relevant organs for decision-making.

  "
  After these processes, the nation will have a new constitution," he noted, adding: "We want to have constitution that matches with the 50-years-old nation (Tanzania)."

  This year, Tanzania will mark 50 years of Tanganyika's independence, 47 years of the Zanzibar Revolution and 47 years of the Union.

  Kikwete, however, defended the current constitution engineered by the founders of the nation saying it moved the country from the post-independence period to "where we are now."

  The existing constitution, he said, contributed to the country's social, political and economic development.

  "
  But there are many changes that have occurred between the post-independence days and today, which require a constitution that accommodates all current developments and changes," said the president.

  The President's stance on the constitution has come at a time when the country was engulfed in heated debate over whether it should have a new constitution or not.

  Attorney General Frederick Werema's recent remarks that the country did not need a new constitution have been received with mixed feelings with a section of the public accusing him of trying to strangle debate on the issue.

  At one time, Constitutional Affairs and Justice Minister, Celina Kombani, played down public demand for new constitution on the simple reasons that "the process is unnecessarily expensive.

  Kombani's provoked heated public debates, with some people calling for resignation of the constitutional affairs' minister, accusing her of undermining concerns of Tanzanians for constitutional reforms.

  Prime Minister, Mizengo Pinda recently in a meeting with editors, promised to advise the president on the need to have new constitution.

  Dwelling on the country's security, President Kikwete said the situation was stable with all borders safe and secure and that there was no threat from any place or people regarding the security of the country.

  On democracy, President Kikwete said it has grown tremendously, admitting that opposition parties were becoming stronger and therefore posing a challenge to the ruling party.

  "
  Last year's general election posed great challenge and the power of opposition parties has increased tremendously," admitted the president.

  On the management of public funds, Kikwete said he had directed concerned authorities to ensure they supervise revenue collection and expenditure of public funds more efficiently.

  "
  I am not satisfied with the use of public funds. The discipline in this is still wanting," he commented.

  On the economy he said the country expected the economy to grow by up to 7.2 per cent compared to 6 per cent of 2009.

  He said inflation has also gone down from 12.1 per cent in 2009 to 5.5 per cent 2010 and it was expected that it would continue to go down.
   
 11. T

  Thomas David Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bunge ni mhimili wa dola unaofanya kazi kwa niaba ya wananchi. Hoja binafsi ya katiba mpya imewasilishwa bungeni, na huko ndiko kutaundwa baraza la kutunga katiba, na watakaofanya hivyo ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wawakilishi wao bila kuingiliwa na Serikali. Na ni huko pia ambapo makundi mbalimbali ya jamii yatashirikishwa katika mchakato wa kuandikwa katiba mpya na USHIRIKI huo hautakuwa kwa hisani ya RAIS Kikwete kupitia wateule wake.

  Tunampongeza kwa KUKUBALI KATIBA MPYA.

  Lakini si kazi ya Kikwete na wala Serikali yake, ni kazi ya Bunge, ni kazi ya Wananchi wa Jamhuri ya Tanzania.

  Sidhani kama ni sahihi kwa Rais Kikwete kuunda tume, na sidhani kama ni njia sahihi ya kupata katiba mpya tunayoitaka. Huku ni kuteka nyara hoja ya watu, hii si kazi yake, hatukumtuma! President Kikwete and his Constitutional Review Commission should stay far aside and let the people of the United Republic of Tanzania decide their destiny kupitia BUNGE.

  I think it worth to say boldly to him, NO, but NO THANK YOU!
   
 12. m

  mzambia JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hapo umenena lkn makinda hawezi kukubali hiyo hoja binafsi hata cku moja labda angekua sitta
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  watanzania bwana... hivi kuna tofauti yoyote tunaitegemea endapo spika ni mama makinda?

  au tunasahau upesi... she is a bulldozer and we should expect her to bias everything, labda zifumuke ngumi kama mabunge ya wenzetu
   
 14. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  in short hapo jamaa wamejiwahi. Hoja ikiwasilishwa Bungeni in February, Speaker atasema swala hilo tayari linafanyiwa kazi na serikali. Serikali itabuy time ili uchaguzi 2015 upite alafu mchezo umeshia hapo. sanasana tukibahatika watabadilisha baadhi ya vipengele vya katiba then finito
   
 15. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Suala la katiba ndio utakuwa mtihani wa kwanza kupima dhamira ya Anna Makinda. Akionyesha kuunga mkono hizi njama za kuondoa suala hilo katika muhimili husika na kulipeleka katika utawala, itaonekana wazi hatuna spika.
   
 16. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama unaliamini sana hili Bunge basi hautashangaa pale Bunge litakapoiridhia tume hiyo ya Rais, wait and see!!
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hizi post zinakuwa nyingi na mantiki ileile, mods mmelala?.
  Any way, How can u trust bunge lenye asilimia zaidi ya 70 ya ccm chini ya makinda kufanya tofauti na jk?
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kuhusu hoja binafsi sitashangaa kale kamama kakiikataa eti Kiwete kashaunda tume maalum ya katiba mpya!
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuhusu suala la kuundwa kwa Katiba Mpya nchini: maadama Mhe Mnyika alikwishasajili hoja binafsi ya kutaka KUUNDWA TUME YA BUNGE YA KURATIBU uandikwa upya Katiba yetu wiki kadha hadi pale Mhe Kikwete naye anatangaza nia yake juu ya hilo hilo, huyu KADA WA CCM hana budi kulitambua na kuheshimu MAMLAKA YA BUNGE ambalo ndilo chombo rasmi cha kushugulika na maswala ya UTUNGAJI SHERIA NA NDIKO KULIKO na wawakilishi wengi wa wananchi kuweza kutolea uamuzi hili jambo zito kitaifa.
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Hawezi kwa kusema hivyo kwa sababu swala la Tume ya Kikwete imebuniwa wiki kadha baada ya ile hoja binafsi kusajiliwa Bungeni. Isitoshe, Bunge, kwa mujibu wa Katika ya sasa, inafanya kazi zake kwa uhuru zaidi bila kuangalia chombo gani tena nje yake inafanya kitu gani.

  Kujitokeza kwa Mhe Kikwete katika hili ndio sasa kaongeza ari zaidi Nguvu ya Umma kuhamia Dodoma mpaka kieleweke.
   
Loading...