Katiba mpya: Badiliko moja la muhimu kwako

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Hivi ingekuwa tumebanwa sana kiasi cha kuandika katiba mpya ikabidi tubadili tu kitu kimoja. Je, wewe ungependa kitu gani/jambo gani moja lishughulikiwe na katiba mpya?

Najua ni ngumu lakini fikiri, chekecha, pata lako moja.

Mimi ningependa katiba itakayohakikisha Tanzania inakuwa na ZERO TOLERANCE KWA UFISADI!
 
Vyama vya siasa visidi vitatu.
wanaobaki wagombee kama wagombea binafsi.

Iwekwe kiwango flani cha idadi ya kura zikipigwa kama chama kisipofikisha kinafutiwa usajili hadi vibaki vitatu kama sio viwili
 
Rais asiwe mwanasiasa,, maana juzi tunashuhudia cdm pamoja na pilika zote za kwenda ikulu lakini wameshindwa kuamini nafasi ya mkuu wa wilaya ktk mchakato mzima, inaonyesha nia yao ni kuingia ikulu2 na cyo kutetea wananchi.
 
Ukikamatwa unatoa au kupokea rushwa, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya basi adhabu yake ni kunyongwa
 
Woooh

Tumejaa mawazo naamini huu uzi tukiuchangia unaweza kuwa chanzo kizuri michango ya katiba mpya

mfano wazo langu ni kuwa - kwa vile wengi wetu siyo wataalamu wa sheria tunachweza kusema ni mawazo kama haya wale wenye weledi wa kisheria watajua ili katiba ihakikishe ufisadi unashuhulikiwa tunahitaji 1,2,3...

Big up tuchange maoni
 
Wabunge wapatikane kwa proportional representation badala ya majimbo kama south africa, pesa za uma zinapotea sana kwenye kampeni za majimbo kwa serikali kutaka kung'ang'ania majimbo.
 
Mawaziri wasitokane na wabunge bali professionals kama ilivyo marekani, italeta kuwajibika badala ya kufanya kazi kwa misingi ya kujikomba kisiasa.
 
Kusiwe na wakuu wa wilaya, wanaongeza mzigo wa gharama kwa serikali kuwalipa mishahara na marupurupu, wakurugenzi watosha.
 
Hivi ingekuwa tumebanwa sana kiasi cha kuandika katiba mpya ikabidi tubadili tu kitu kimoja. Je, wewe ungependa kitu gani/jambo gani moja lishughulikiwe na katiba mpya?

Najua ni ngumu lakini fikiri, chekecha, pata lako moja.

Mimi ningependa katiba itakayohakikisha Tanzania inakuwa na ZERO TOLERANCE KWA UFISADI!

1. Kifungu kiingizwe kitakaacho idhinisha na kuwekea limitations safari za rais za nje ya nchi. Walau sizidi safari 20 kwa mwaka.
2. Shule za secondary zote za kata zisizokuwa na waalimu wasiozidi 5 zifungwa kuepuka failures za aibu kila mwaka.
 
Uangaliwe uwezekana wa kuwa na wizara chache muhimu, zisizidi kumi na kusiwe na manaibu waziri kwani ni mzigo kwa serikali katibu mkuu wa wizara atosha sana.
 
Back
Top Bottom