Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,951
- Thread starter
- #101
Katiba ya warioba haingeongelea mambo hayo kwa sababu kwenye mfumo wa serikali tatu, hayo siyo mambo ya muungano! Hayo mambo yote yangetajwa kwenye katiba ya Tanganyika na katiba ya Zanzibar. CCM wamewatupia changa la macho tena wananchi kama wewe kwa kuwaambia eti mzisome rasimu zote mbili mzilinganishe wakati siyo sahihi kufanya hivyo! Ya warioba ilijikita kwenye yale mambo ya muungano tu! Mambo ya ardhi, vijana, wakulima, wavuvi na kadhalika yote yangetajwa kwenye katiba za nchi washirika. Sijui umeelewa?!
Umeniuliza swali moja tu nalo ni 'Kwahiyo hapa hoja ya UKAWA ni serikali 3, mambo mengine ya wananchi wao hayawahusu.' Naamini nimekujibu vilivyo!
Kama ilijikita kwenye mambo ya muungano kwann iongelee haki za binadamu?