Katiba imekaa vizuri sana

Katiba imekaa vizuri sana

Hii ndiyo ilikuwa rasimu ya ukweli. Soma kwa makini utagundua kuwa unaongozwa kwa ushabiki zaidi.
Japo kuwa umeandika kwa mwandiko mdogo sana hebu soma Ibara 28 kifungu cha 2
(2) Kwa madhumuni ya Katiba hii, Bunge litatunga sheria
itakayoweka, pamoja na mambo mengine-
(a) tafsiri ya neno zawadi, aina, thamani, kiwango na uhifadhi wa
zawadi za Jamhuri ya Muungano;
(b) masharti ya kufungua akaunti za nje kwa kiongozi wa umma;
(c) masharti ya kumtaka kiongozi wa umma kutoa tamko la mali na
thamani yake, madeni yake pamoja na ya mwenza wake wa ndoa;
(d) masharti ya kuzuia kiongozi wa umma kutoshiriki kufanya
uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana maslahi nayo
yeye binafsi, mwenza wake wa ndoa, mtoto wake, jamaa au rafiki
yake au mtu yeyote wa karibu;
(e) masharti ya matumizi ya mali ya umma;
(f) utaratibu wa utwaaji wa mali za kiongozi wa umma
zinazopatikana kwa kukiuka sheria;
(g) utaratibu wa kumwajibisha kiongozi wa umma aliyekiuka maadili
na miiko ya uongozi wa umma;
(h) uanzishaji wa mitaala inayohusu Katiba, maadili na uraia, shuleni
na vyuoni; na
(i) mambo yasiyotakiwa kwa watumishi wa umma.
(3) Wadhifa wa "kiongozi wa umma" kama ulivyotumika katika
Sehemu hii utajumuisha kiongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa kama
itakavyoainishwa kwenye sheria za nchi.

Angalia na hapa
29.-(1) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, kiongozi wa umma
ataheshimu na kutii maadili ya uongozi wa umma na miiko ya uongozi.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoainisha:
(a) miiko inayopaswa kuzingatiwa na viongozi wa umma;
(b) utaratibu wa kumuondoa kazini kiongozi wa umma kutokana na
kuvunja miiko na kukiuka maadili ya uongozi wa umma;
(c) vitendo ambavyo Kiongozi wa umma hapaswi kuvitenda; na
(d) ngazi au orodha ya viongozi wa umma wanaofungwa na Ibara hii.
 
... Mkuu, Huyo Jamaa Atakuwa Kada Wa Ccm, Anajaribu Aone Kama Takataka Yao Inakubarika Au La

Ungetafuta wasaa ukatuliza akili na kuisoma hii rasimu iliyopendekezwa usingeandika hivi. Tatizo lenu ni wavivu wa kujisomea.

Mimi binafsi sijaona ubaya wake!
 
Ungetafuta wasaa ukatuliza akili na kuisoma hii rasimu iliyopendekezwa usingeandika hivi. Tatizo lenu ni wavivu wa kujisomea.

Mimi binafsi sijaona ubaya wake!

Utaonaje ubaya wake na wewe ni gamba?
 
Ungetafuta wasaa ukatuliza akili na kuisoma hii rasimu iliyopendekezwa usingeandika hivi. Tatizo lenu ni wavivu wa kujisomea.

Mimi binafsi sijaona ubaya wake!

... Ni Kwavile Umevaa Miwani Ya Mbao, Ndo Maana..
 
Katiba imepitishwa kiujanja ujanja na magamba pale Dodoma, na wewe ni gamba mwenzao japokua hukwenda Dom. Utaionaje ubaya wake?
 
... Nasikia Huyu Annael Siyo Mtanzania, Ni Mganda Alikimbia Vita Ya Idd Amin
 
Japo kuwa umeandika kwa mwandiko mdogo sana hebu soma Ibara 28 kifungu cha 2

Angalia na hapa

Tofauti yake ni kwamba rasimu ya Warioba ilikuwa moja moja bila kumung´unya maneno; huu uchafu wa 6 unajikanyagakanyaga na kutupia mpira bunge ambalo pia wanajua kuwa kwa kuruhusu darasa la saba kama "Kibajaji" kuwa wabunge, hilo bunge halitatunga chochote cha maana.
 
3. angalia Ibara 28 zilizo ondolewa kabisa kutoka katika RASIMU YA warioba ambazo hazijaguswa kabisa katika RASIMU YA WALIO WENGI ibara ya 15 - 20 ya Rasimu ya Walioba zinazoomuwekea mtawala taratibu za kutawala zime ONDOLEWA KABISA. Mfano 18.-(1) Kiongozi wa umma hatashiriki katika kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana masilahi nayo yeye binafsi, mwenza wake, mtoto wake, jamaa yake, rafiki au mtu yeyote wa karibu.

MWISHO. NAKUPONGEZA KWA KUANZISHA THREAD HII lakini unapojadili ya kwako, haya pia yakusaidie kufikia uamuzi kama kweli Katiba hii IMEKIDHI HAJA au LA.
Nashukuru sana ndugu yangu ila umesahau kimoja hebu soma hapa
225.-(1) Majukumu ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
yatakuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo wa viongozi wa umma
kwa madhumuni ya kusimamia na kuhakikisha kuwa maadili na miiko ya
uongozi wa umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa
Serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma.
(2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1), majukumu
mahsusi ya Tume yatakuwa ni:
(a) kusimamia maadili katika utumishi wa umma;
(b) kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma na kuchukua
hatua pale inapostahili; na
(c) kusimamia sheria kuhusu maadili ya viongozi wa umma.
(3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara
hii.
 
Tofauti yake ni kwamba rasimu ya Warioba ilikuwa moja moja bila kumung´unya maneno; huu uchafu wa 6 unajikanyagakanyaga na kutupia mpira bunge ambalo pia wanajua kuwa kwa kuruhusu darasa la saba kama "Kibajaji" kuwa wabunge, hilo bunge halitatunga chochote cha maana.
Kaka hapo ndio unapo enda tofauti. Kumdharau mtu sio vyema hebu tu chambue kwa hoja.
Unajua kuna vitu vingine vinatakiwa viwekwe kwenye sheria maana vinabadilika kila wakati.

Hebu jaribu na kujisomea hapa
225.-(1) Majukumu ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
yatakuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo wa viongozi wa umma
kwa madhumuni ya kusimamia na kuhakikisha kuwa maadili na miiko ya
uongozi wa umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa
Serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma.
(2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1), majukumu
mahsusi ya Tume yatakuwa ni:
(a) kusimamia maadili katika utumishi wa umma;
(b) kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma na kuchukua
hatua pale inapostahili; na
(c) kusimamia sheria kuhusu maadili ya viongozi wa umma.
(3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara
hii.
 
... Nasikia Huyu Annael Siyo Mtanzania, Ni Mganda Alikimbia Vita Ya Idd Amin
Mnyarwanda vipi tena. Umeanza kubabaika na kurukia kila tawi.
 
tume ya mipango
18.-(1) kutakuwa na tume ya mipango ya jamhuri ya muungano
itakayoitwa "tume ya mipango" ambayo itakuwa ndicho chombo cha juu cha
kupanga na kusimamia utekelezaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya
taifa.
(2) bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa ibara hii.
 
lengo la kijamii

14.-(1) lengo la katiba hii kijamii ni kujenga jamii yenye ustawi na
uwezo wa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali.
(2) katika utekelezaji wa lengo hilo, serikali itachukua hatua
zinazofaa ili:
(a) kuhakikisha kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na
kudumishwa kwa kufuata mila, desturi na kanuni za tangazo la
dunia kuhusu haki za binadamu na mikataba mingine ya
kimataifa iliyoridhiwa na tanzania;
(b) kuhakikisha kwamba serikali na vyombo vyake vyote vya umma
vinatoa nafasi na fursa sawa kwa raia wote, bila ubaguzi;
(c) kuhakikisha kuwa huduma na hifadhi ya jamii inatolewa kwa watu
wasiojiweza, wazee, watoto na watu wenye ulemavu;
(d) kuwezesha upatikanaji na utoaji wa huduma ya msaada wa
kisheria kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama
za mawakili;
(e) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa
haki ya mtu kujipatia elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya
kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi kufikia upeo wowote
kulingana na uwezo wake; na
(f) kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa watu wote
ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi salama.
 
Kaka hapo ndio unapo enda tofauti. Kumdharau mtu sio vyema hebu tu chambue kwa hoja.
Unajua kuna vitu vingine vinatakiwa viwekwe kwenye sheria maana vinabadilika kila wakati.

225.-(1) Majukumu ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
yatakuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo wa viongozi wa umma
kwa madhumuni ya kusimamia na kuhakikisha kuwa maadili na miiko ya
uongozi wa umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa
Serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma.
(2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1), majukumu
mahsusi ya Tume yatakuwa ni:
(a) kusimamia maadili katika utumishi wa umma;
(b) kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma na kuchukua
hatua pale inapostahili; na
(c) kusimamia sheria kuhusu maadili ya viongozi wa umma.
(3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara
hii.

Hebu jaribu na kujisomea hapa

Hizi ni porojo tu ambazo hazina tofauti sana na yaliyomo kwenye katiba ya sasa. Hii rasimu ya Sitta na Vijisenti imejaa unafiki na mambo yaleyale ya kale. Imekosa ujasiri wa kukataza maovu moja kwa moja. Kusema kwamba darasa la saba wasiruhusiwe kuwa wabunge sio ubaguzi, ni swala linalojibu mahitaji ya nyakati hizi za sasa; hivi mbunge wa darasa la saba atakuwa na kichwa cha kuchambua na kuhoji mkataba wa serikali na Statoil? darasa la saba anakichwa cha kuchambua hesabu za serikali? Matokeo yake ndiyo unakuwa na wabunge wenye hoja kama za John Komba (aka usingizi) kumuita Warioba shiiida.
 
Heshima kwako. Tatizo haujui kazi ya mbunge ni nini.
Hebu twende kipengere kwa kipengere kuhusu katiba ya iliyopo na rasimu hii.

Halafu useme kama ziko sawa.
 
cha msingi katiba haiwezi kumfanya kila mtanzania kuwa na maisha bora....! fanya kazi ndipo maisha bora yatakuja!
 
Heshima kwako. Tatizo haujui kazi ya mbunge ni nini.
Hebu twende kipengere kwa kipengere kuhusu katiba ya iliyopo na rasimu hii.

Halafu useme kama ziko sawa.

Haziko sawa, zingekuwa sawa wasingemwita Warioba shiida. Huitaji masters degree kulibaini hilo.
 
Haziko sawa, zingekuwa sawa wasingemwita Warioba shiida. Huitaji masters degree kulibaini hilo.
Mkuu wewe unapinga kitu gani? Hebu twende pointi kwa pointi. Maana nimekupa vipengere haujapinga kwa hoja. Naomba Labda unipe kipengere kwa kipengere tofauti ya Rasimu ya Tume na hii ya Bunge maalumu.

Maana tukiongea tuuu hatutamaliza.
Nawasilisha hoja.
 
Kwenye tatizo ni huko kwenye uongozi wa nchi. Kwa nini waliondoa vipengele muhimu kama wananchi kuwawajibisha wabunge na wanabunge kuwa watu wenye elimu ya form four? ndiyo maana bunge letu litaendelea kuwa substandard na lisilokuwa na viwango. Pia muundo huu wa muungano ni wa ovyo sana haijawai tokea. Kwa nini tusiwe na serikali moja au tatu ili muungano ueleweke? Sasa hivi Tanganyika inaminywa tu na wazanzibar wanadandia tu!
Hii katiba yetu huwezi kusimama hata kuilinganisha na katiba za nchi kama Kenya au SA au Ghana......haina viwango na ni ya kuundwa kimagendo kwa maslahi ya chama kimoja! Huu mpasuko wa kisiasa uliojitokeza lazima utaadhiri utekelezwaji wa katiba mpya pindi itakapokubaliwa na wananchi. Ila CCM kwa vile wanadhani watabaki madarakani milele, ndio maana wamepitisha katiba ya ovyo kama hii! Katiba inafaaa kuwa chama chochote kikishika dola kinaridhika na muundo wa serikali uliopo na si vinginevyo!
 
Ongelea katiba na pointi kwa point sio kuleta porojo hapa. Tao ibara ipi unaipinga kwanini. Sio kutoa bra bra tu.

Amir jeshi wa Tanzania ni nani? Je Rais wa Zanzibar anapigiwa mizinga kama nani? Sherehe za Mapinduzi nani anatangulia uwanjani?
 
Back
Top Bottom