Katiba imekaa vizuri sana

Katiba imekaa vizuri sana

Annael

Kazi yako umefikisha sassa nenda kachukue chako lumumba!
 
Katika hicho ulichoandika kuwa mtu yeyote hataruhusiwa,kuanzisha taasisikampuni au kikundi cha ulinzi na usalama katika Taifa,je green guard na chipukizi ccm wataacha?
 
Sasa wewe tatizo lako ni nini? maana umetoka nje ya pointi kabisa. Umeenda nje ya key.

Ardhi siyo ishu ya muungano mamdogo, wamekukaririsha vibaya. Mzanzibar akija bara ana uwezo wa kumilikishwa ardhi lakini mtanganyika akienda Zanzibar haruhisiwi kumiliki ardhi kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar. Sasa unakurupuka tu kulete ushabiki usiokua na tija, acheni unafiki kama mnanufaika na mfumo kuweni wawazi tu.
 
Uhuru wa mtu
41. Kila mtu anastahili kuwa huru bila kuathiri sheria za nchi, kukutana
na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na
watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na kwa ajili hiyo kuanzisha au
kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi
au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
 
Na taifa hili linazidi kuangamia kutokana na watu wa aina yako, badalaya kuwa mzalendo umekalia ushabiki tu hapa tuondolee upambafu wako hapa.
 
Katika hicho ulichoandika kuwa mtu yeyote hataruhusiwa,kuanzisha taasisikampuni au kikundi cha ulinzi na usalama katika Taifa,je green guard na chipukizi ccm wataacha?
Sasa umeanza kuona uzuri wa hii katiba sasa?
 
Ardhi siyo ishu ya muungano mamdogo, wamekukaririsha vibaya. Mzanzibar akija bara ana uwezo wa kumilikishwa ardhi lakini mtanganyika akienda Zanzibar haruhisiwi kumiliki ardhi kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar. Sasa unakurupuka tu kulete ushabiki usiokua na tija, acheni unafiki kama mnanufaika na mfumo kuweni wawazi tu.

Soma hii ibara kwa makini

25. Maliasili zote za Taifa ikiwa ni pamoja na madini, gesi na mafuta ni
mali ya umma, na Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar itaweka utaratibu wa kuhakikisha zinatumika kwa manufaa ya
kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Ongezea na hii
23. Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu mgawanyo wa
matumizi bora ya ardhi kwa makundi mbalimbali ya jamii.
 
Na taifa hili linazidi kuangamia kutokana na watu wa aina yako, badalaya kuwa mzalendo umekalia ushabiki tu hapa tuondolee upambafu wako hapa.
Kwa tafsiri yako mtu mzalendo yukoje? anatakiwa afanye nini?
Hebu nipe tafsiri....
 
.... Yaani Unasukuma Maji Yaingie Kwenye Jiwe, Yaan Zanzbar Ijitegemee Mambo Yasiyo Ya Muungano? Tanganyika Ndo Iwe Serikali Ya Muungano? Hahahahaaa.! Hivi Vituko Kweli.!!

Nilidhani nimemuelewa 'vibaya'. Thanks kwa kuliona pia
 
Dira ya Taifa ya Maendeleo
17.-(1) Kutakuwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo katika nyanja
mbalimbali kwa kuzingatia haki na wajibu wa kila raia kupata maendeleo.
(2) Katika kutekeleza ibara ndogo ya (1), Mamlaka za Serikali zitaweka
mipango ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo.
 
LENGO LA KIUTAMADUNI
15.-(1) Lengo la Katiba hii kiutamaduni ni kukuza, kudumisha na
kuhifadhi lugha ya Kiswahili, urithi wa asili na utamaduni wa wananchi.
(2) Katika kuhakikisha utekelezaji wa lengo hilo, Serikali itachukua
hatua zinazofaa ili:
(a) kulinda na kuendeleza lugha ya Kiswahili;
(b) kulinda na kuhifadhi urithi wa asili, malikale na sehemu zenye
umuhimu wa kihistoria ili kuepuka uharibifu, wizi au utoroshaji nje
ya nchi;
(c) kulinda, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali;
(d) kujenga utamaduni wa kuwepo ushirikiano, maelewano,
maridhiano, uvumilivu na kuheshimu mila, desturi na imani ya dini
ya kila mtu; na
(e) kuweka mazingira yatakayowezesha wasanii kutumia fursa zilizopo
na vipaji vyao katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na mabadiliko
katika jamii.

Wasanii katiba imesikia kilio chao
 
Nimeipitia katiba kipengere kwa kipengere.
Hakika imekaa vizuri sana. nimekuwa nikijiuliza wale wanaoipinga wanapinga kwa hoja zipi!!?
Ailimia kubwa mambo yaliyopendekezwa na tume ya Warioba yamo.
Eti kwa sababu tu kwamba serikali tatu haipo.
Asilimia kubwa ya watu wanaisoma kwa mrengo wa kuipinga. Hawako na free mind.

Kuna mambo mazuri sana mengi. Mfano:



Na kuna mambo mengi sana nitaendelea kuya toa.


Hii ndiyo ilikuwa rasimu ya ukweli. Soma kwa makini utagundua kuwa unaongozwa kwa ushabiki zaidi.

Ibara 28 zilizoondolewa

15. (1) Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa katibu mkuu wa wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:

(a) aina ya zawadi; (b) thamani ya zawadi; (c) sababu ya kupewa zawadi; na (d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.

(2) Neno "zawadi" kama lilivyotumika katika ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani atakachopewa kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.

(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.

16. Kiongozi wa umma-

(a) Hatafungua au kumiliki akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na (b) hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au heshima ya utumishi wa umma.

17.-(1) Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi, mali na thamani yake na madeni yake katika Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha taarifa ya mali na madeni: (a) yake binafsi; (b) ya mwenza wake wa ndoa; na (c) ya watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane, mara moja kila mwaka kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.

(3) Bunge litatunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine: (a) ngazi au orodha ya viongozi wa umma wanaopaswa kutangaza mali na madeni yao; na (b) utaratibu wa kuwasilisha taarifa ya mali na madeni kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kwa mujibu wa Katiba hii.

18.-(1) Kiongozi wa umma hatashiriki katika kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana masilahi nayo yeye binafsi, mwenza wake, mtoto wake, jamaa yake, rafiki au mtu yeyote wa karibu.

(2) Kiongozi wa umma hatazungumzia kitu chochote katika Baraza la Mawaziri, Bunge, Kamati au chombo kingine chochote rasmi ambacho ana masilahi nacho ya moja kwa moja au vinginevyo, isipokuwa tu kama atatoa taarifa ya mgongano huo wa masilahi katika chombo hicho.

(3) Itakuwa ni marufuku kwa kiongozi wa umma kushiriki katika uamuzi unaohusu kuongeza au kuboresha masilahi kwa namna yoyote ile yanayohusu wadhifa alionao na endapo atashiriki, basi masharti hayo mapya yataanza kutumika kwa kiongozi wa umma atakayekuja baada ya kiongozi husika kuondoka au kumaliza muda wa kukaa katika nafasi ya madaraka iliyompatia fursa ya kushiriki katika kuamua masilahi husika.

(4) Masharti ya ibara ndogo ya (3), hayatamhusu kiongozi wa umma ambaye kutokana na asili ya nafasi ya madaraka au aina ya kazi zake anapaswa kushiriki katika upangaji wa mishahara au maslahi mengine ya watumishi wa umma.

(5) Kiongozi wa umma hataruhusiwa kushika nafasi za madaraka zaidi ya moja au kutumikia mihimili ya dola zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

19. Kiongozi wa umma hataruhusiwa kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya umma, zikiwemo zilizokodishwa kwa Serikali, kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi au kumpatia mtu mwingine manufaa yoyote.
 
Kwa tafsiri yako mtu mzalendo yukoje? anatakiwa afanye nini?
Hebu nipe tafsiri....

Kwa unachokishabikia hapa ni wazi kuwa hujalelewa ktk misingi ya kizalendo. Wewe gamba tu kama magamba wengine wa Lumumba.
 
Annael: WAKATI MWINGINE USIJE NA HOJA ambayo itakufanya upate upinzani mkali kama huu; na kama KUNA JAMBO FULANI UNALOLIPENDA TATHMINI KAMA NA WATU WENGINE WANALIPENDA KAMA WEWE; labda kama umetumia njia hii kujaribu kupata ufahamu kama watu wamepokeaje RAIMU HII YA TATU.

HOJA:
madai ya mwanzo ya kudai Katiba mpya yalitokana na msukumo wa kuwa na Amani katika Chaguzi za viongozi ikiwa ni pamoja na malalamiko ya vyama vya Upinzani nchini kutendewa ndivyo sivyo katika zoezi la kura. Yapo mambo mengi yaliyosukuma kuandikwa kwa Katiba mpya. Muungano haikuwa hoja kubwa kwa wakati ule labda kama ilikuwa ajenda ya siri kwa wadau. MIMI NILITEGEMEA RASIMU HII INGEONDOA KERO YA TUME YA UCHAGUZI ibara ya 211 na uteuzi wao 211 (2) kwa kipengele hiki tu; NIA NZIMA YA kutatua shida kubwa za kiuchaguzi kupitia Katiba imepotea. Nchi hii inaweza kuingia katika machafuko kutokana na Chaguzi kama ilivyotokea Zanzibar miaka ya 90.

2. Mfumo wa Mamlaka kuu za Utendaji kutokana na kuteuliwa na raisi ni sababu nyingine iliyofanya Wapinzani kulalamikia Katiba ya 1977. kutokana na hilo tumekuwa na na Serikali isiyowajibika; na isiyo adilifu. nilidhani RASIMU HII hata kama imetokana na Waliowengi Bungeni ingetatua shida hii ya ukubwa wa Uteuzi wa Raisi angalia Ibara ya 110, 113, 115, 116, 211 nk huo ni uteuzi wa Viongozi wa juu katika nchi hii.

3. angalia Ibara 28 zilizo ondolewa kabisa kutoka katika RASIMU YA warioba ambazo hazijaguswa kabisa katika RASIMU YA WALIO WENGI ibara ya 15 - 20 ya Rasimu ya Walioba zinazoomuwekea mtawala taratibu za kutawala zime ONDOLEWA KABISA. Mfano 18.-(1) Kiongozi wa umma hatashiriki katika kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana masilahi nayo yeye binafsi, mwenza wake, mtoto wake, jamaa yake, rafiki au mtu yeyote wa karibu.

4. Madai ya Zanzibar yanatofautiana na ya Tanganyika kwa sehemu; angalia hoja za mwanasheria mkuu wa Zanzibar amezikataa karibu Ibara zote zinazohusu Muungano. yalikuwa ni mawazo yake lakini kwa uwakilishi mpana wa mawazo ya Wazanzibar. KUNDI LA WENGI lingeweza kurekebisha hilo katika Rasimu ya Tatu.

5. mwenendo mzima wa upatikanaji wa Katiba haukujikita katika Utaifa, Nchi imegawanyika kimtazamo na kwa Katiba ya Namna hii hata kama itapita INAWEZA KUZAA UASI KIFIKRA. ONA, makundi ya dini, makundi ya vyama vya siasa, makundi ya wasomi, makundi ya wawakilishi wa wanachi yote yamegawanyika. HAKUNA YEYOTE ANAYETHUBUTU KUYAUNGANISHA PAMOJA KATIKA HILI, hali ni mbaya kwa mstakabari wa nchi yetu.

MWISHO. NAKUPONGEZA KWA KUANZISHA THREAD HII lakini unapojadili ya kwako, haya pia yakusaidie kufikia uamuzi kama kweli Katiba hii IMEKIDHI HAJA au LA.
 
Back
Top Bottom