Katiba, demokrasia na Mahakama. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba, demokrasia na Mahakama.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mag3, Nov 9, 2008.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Yanayotokea hivi sasa jimbo la California nchini Marekani baada ya uchaguzi ulioisha hivi majuzi, yamezua maswali kuliko majibu.

  Hapo nyuma wakazi wa CA waliwahi kupiga marufuku ndoa za mashoga kwa kupiga kura na kurekebisha katiba. Mashoga ambao hawakuridhika na maamuzi ya wengi walifungua kesi mahakamani kupinga uamuzi huu kwa kusema inawabagua na kuwanyima haki yao ya msingi kwenye katiba. Mahakama ilikubaliana nao na kuruhusu ndoa za mashoga kwa kigezo cha usawa kwa wote kama ilivyooanishwa kwenye katiba.

  Kwenye uchaguzi huu uliopita wakazi wa CA kwa mara nyingine wamepitisha katiba kwa kuzikataa hizo ndoa. Mashoga hawaonekani kukubali hii hali na wako mbioni kufungua tena kesi mahakamani. Kusema kweli nimeshindwa kuelewa kinachotokea hapa na nimebaki najiuliza maswali kadhaa. Hivyo naomba wanasheria na wataalamu wa katiba watoe darasa hapa wanisaidie kujibu maswali yafuatayo;

  1. Je ipi inatangulia kati ya katiba na matakwa ya wananchi kujiamulia wanavyotaka kuendesha maisha yao.
  2. Mipaka ya mahakama inaanzia na kuishia wapi bila kuingilia katiba.
  3. Demokrasia, kama maamuzi ya wengi, inapewa uzito upi ndani ya katiba.
  4. Je katika kulinda haki za wachache ndani ya demokrasia, mahakama ina haki ya kutokuheshimu maamuzi ya wengi.
  5. Hili sakata litaweza kumalizika vipi kama mahakama itaendelea kubatilisha maamuzi ya wakaazi wa CA.

  Naomba kuwasilisha.
   
Loading...