Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Pasco,

..mawazo yako ni sawa na ya Dr.Kashilila, katibu wa bunge.

..tofauti ndogo ni kwamba Dr.Kashilila amekwenda mbali na kueleza kwamba baada ya mswada kusimamishwa na hoja kutolewa kura zingepigwa. sasa mtego upo hapo kwenye KURA.

..bila kutueleza kwamba you have some info that we dont have, kwamba kulikuwepo na wabunge wa kutosha waliokuwa wamepania mswada usipite ikiwa CDM wange-invoke hicho kifungu unachosema, then naweza kukubaliana na hoja uliyoileta hapa kwamba CDM made a mistake.

..vinginevyo inawezekana kabisa CDM walishajua watashindwa kwa namna yoyote ile, na wakaamua kufanya hicho walichoweza kufanya.

NB:

..naomba nikukumbushe kwamba you can invoke kila pingamizi unalolitaka ndani ya bunge, lakini at the end of the day lazima uwe na KURA za kutosha.

..hivi kuna wakati wowote ule in this whole process ambapo CDM wamejaribu kuwashawishi/kuwa-rectruit wabunge wa vyama vingine wawaunge mkono ktk kuupinga mswada wa katiba?
 
Wanabodi,
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.

Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja kuhodhi madaraka yote ya dola.

Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.

Suala la kususia jumla mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni kuunda katiba mpya ni kosa kwa sababu Chadema kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilikuwa na uwezo wa kuusimamisha na kuzuia uwasilishwaji kwa mara ya pili huo muswada kwa kutumia kanuni ya kifungu 86 hivyo kutoa fursa ya hoja ya kuzuia uwasilishwaji huo kusikilizwa, lakini Chadema haikufanya hivyo.

Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa wabunge wa Chadema katika umakini, kitendo cha oversight ya opportunies provided by kifungu cha 86 cha kanuni za bunge kuuzuia huo muswada, sio tuu ni udhaifu mkubwa, but kosa kubwa ambalo Chadema lazima wakiri, waombe radhi na kusonga mbele.

Kanuni hiyo ya 86 inaeleza wazi hatua kwa hatua za kufuatwa ili kuuzuia muswada usisomwe kwa mara ya pili. Chadema ilipuuza na kuendelea kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani.

Kama Chadema ingezingatia kanuni hiyo, isinge wasilisha maoni ya kambi ya upinzani bali ingewasilisha pingamizi!.

Kitendo cha Mhe. Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, yamemaanisha wameijibu hoja ya serikali hivyo kutoa go ahead majadiliano yaendelee. Uwasilishwaji wa hotuba hiyo ndio passport ya mjadala kuendelea, kama kambi ya upinzani wasingewasilisha maoni yao, muswada ungesitishwa kwanza na wao kusikilizwa. Hivyo iwasilishwaji wa hotuba ile ni kosa la pili, Chadema lazima wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Kitendo cha kususia mjadala kwa siku ya kwanza na kutoka nje, was the right move kuonyesha protest dhidi ya unyanyasaji wa Mhe. Spika, lakini kuisusa hoja jumla, was a mistake hivyo sheria imetungwa bila imput yao, hivyo hili ni kosa la tatu, Chadema wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Nimebahatika kuhudhuria mdahalo wa Star TV kuhusu Tanzania tuitakayo ambapo Mhe. Tindu Lissu ilikuwa ni mdahiliwa, na nilipata fursa ya kuuliza swali kuhusu kanuni ya 86 lililokuwa na vipengele a, b na c
(a) Kanini hawakitumia kanuni ya 86 kuuzuia muswada usisomwe?.
(b) Kwanini waliwasilisha hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani yaliyotoa passport mjadala uendelee badala ya kuwasilisha pingamizi ambayo ingeusimamisha mjadala?.
(c) Chadema wamesusa sheria imepitishwa, jee wamefaidika na nini na kususa kwao?.

Mhe. Lissu amepiga chenga kutoa majibu ya kina kwa kujibu
(a). Amenisomea hitimisho la hotuba yake. Kanuni ya 86 ilimtaka Mhe. Lissu awasilishe pingamizi na sio hotuba!.
(b) Amepiga chenga kueleza ni kwanini amewasilisha hotuba badala ya pingamizi!.
(c) Wananchi wanaelewa ni nani mtetezi wao wa ukweli.

Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the bettle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.

This is very exhaustive ila kama kawaida mwamba ngozi huvutia kwake na hapa ndipo ile tija na uhalisia wa forum unapoanza kugubikwa na mambo yasiyo ya msingi. Pasco you'v tried your level best to make sure that evry untouched stone is touched anyhow lakini kama kawaida usipogusa lile alitakalo flani uliguse basi utaonekana hufai kabisa. Ila kama tukiamua kuwa wakweli ufafanuzi huu watosha kukaa na kutafakari upya ninachoshangaa ni pale watu wanapojaribu kuji prempty kwamba kama Chadema wangetumia Kanuni husika na Fasili zake eti bado wasingesikilizwa hii ni ajabu kabisa why are we trying to predict the consequences, ukweli ni kwamba hawakutambua kanuni hiyo, na ndiyo maana wakawa wanaomba miongozo pasipo kujua ama wanakazwa au wanaruhusiwa na Kanuni ipi na kwa mtazamo wangu Kamati Kuu ya Chadema iligundua hilo na ndiyo maana wakaamua busara itumike kukutana na Rais manake kukutana na Rais bado wana exhaust local remedies ambazo kama wangejua wangeanza toka wakiwa Bungeni.

Na tatizo ni lile lile ukisema Pasco hoja yako inaonekana Kihoja ila akisema mwingine Kihoja chake ndicho kitalazimishwa iwe Hoja. Binafsi japo nilitamani tu kupita ila kwa udadavuzi wako nimeona nitie neno wengine hoja hakuna wameamua kuanza kukuchunguza u nani, its sucks anyway........
Mkuu wangu umevizia mjadala na kufunga goli sio halali.... Nadhani hapa tunatazama maslahi yetu wnaanchi na sii ya Chadema wala CCM. Tunataka kujua kwa nuini wabunge wetu walishindwa kuweka pingamizi ktk muswada ambao wengi wao wanafahamu vizuri mapungufu yake kama tulivyokuwa hapa kijiweni tukiuzungumzia ule ulokuja mara ya kwanza kwa Kiingereza. Hivyo walikuwa na muda wa kuupitia huu mpya wakagundua kilichobadilishwa ni lugha tu, lakini wabunge wote bado wakashindwa kuusimamisha usisomwe mara ya pili kwani kutoa pingamizi haikuwa kazi wala mamlaka ya Chadema peke yake..

Kwa hiyo usione mazungumzo yote hapa ukayachukulia ya kichama kwa sababu tu wanaopiga makelele wengi ni wana Chadema..hatupo kivyama ama kupendelea muswada utiwe sahihi ya Mh.rais kwa sababu za kichama. Laa hasha, tunaupinga kwa sababu ramani nzima ya ujenzi wa msingi huu unalenga kujenga katiba kama marais wanavyotaka iwe kwa kuteua tume ya mapendekezo yao... Makosa yameisha fanyika hatuna jinsi lakini kutafuta kiini cha makosa haya ni kipi nadhani tunayo haki hiyo..

Bora mara 10 (ingawa sii mapendekezo yangu) Marais wote wa pande mbili na wabunge wake washirikishwe ktk uchaguzi wa tume kisha hiyo tume ichague viongozi wake wenyewe mwenyekiti, katibu na kadhalika bila kuwekewa masharti ya sehemu zipi wasiziguse kwa sababu uamuzi wa mwisho bado watakua nao hao viongozi wetu na wanaweza kutuambia kwa nini kipengele kadhaa hakitabadilishwa..

Jamani - Baraza la Mapinduzi, Zanzibar karibu wote wamekwisha kufa na siku zote Muungano wetu ndio umejengwa kuhakikisha usalama wa mapinduzi yake sii kundi la watu, iweje bado Baraza hilo liwe na mamlaka makubwa kwa serikali ya Zanzibar wakati kuna wafuasi wa vyama vingine ambao sii wajumbe wa baraza hilo... Yaani hawa hawana mamlaka ya Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar?..Sii ndio kusema Zanzibar haitawaliki na chama chochote zaidi ya CCM!

Tunahitaji uchama na kuwalaumu Chadema hata kufikiria haya machache kwa sababu tu wabunge wa CCM au CUF hawakuona tatizo hili?
 
Kuna watu wanataka kuandamana kuunga mkono muswaada huu, na kuna watu wanataka kupinga. Mleta mada ana hoja ambayo watu wa upande fulani wanataka kutuonyesha kwamba haina nguvu kwa sababu hii nchi ni yetu wote kwa hiyo wote tupo responsible.

NOOO!!!.... Waliotaka kuupinga huu mswaada wamepoteza opportunity ya ku-showcase their points not only kwa wabunge wanaoisupport hii bill, bali hata kwa wananchi lukuki waliokuwa wakiangalia TV na mitandaoni, pia wahisani,mabalozi na wageni wengine walokuwapo. Kutoka nje sio uanamapinduzi kama mnavyofikiria, haiwavutii wahisani kama mnavyofikiria, na CDM kutaka kuoanana na rais ilishaongelewa wakati Slaa,Salim A. Salim na jaji warioba walipokutana.
Ni sarakasi tu, walijua watakachofanya ila walitaka kuonyesha wageni uanamapinduzi wao, too bad it didnt work that well.

Mkuu wangu umevizia mjadala na kufunga goli sio halali.... Nadhani hapa tunatazama maslahi yetu wnaanchi na sii ya Chadema wala CCM. Tunataka kujua kwa nuini wabunge wetu walishindwa kuweka pingamizi ktk muswada ambao wengi wao wanafahamu vizuri mapungufu yake kama tulivyokuwa hapa kijiweni tukiuzungumzia ule ulokuja mara ya kwanza kwa Kiingereza. Hivyo walikuwa na muda wa kuupitia huu mpya wakagundua kilichobadilishwa ni lugha tu, lakini wabunge wote bado wakashindwa kuusimamisha usisomwe mara ya pili kwani kutoa pingamizi haikuwa kazi wala mamlaka ya Chadema peke yake..

Kwa hiyo usione mazungumzo yote hapa ukayachukulia ya kichama kwa sababu tu wanaopiga makelele wengi ni wana Chadema..hatupo kivyama ama kupendelea muswada utiwe sahihi ya Mh.rais kwa sababu za kichama. Laa hasha, tunaupinga kwa sababu ramani nzima ya ujenzi wa msingi huu unalenga kujenga katiba kama marais wanavyotaka iwe kwa kuteua tume ya mapendekezo yao... Makosa yameisha fanyika hatuna jinsi lakini kutafuta kiini cha makosa haya ni kipi nadhani tunayo haki hiyo..

Bora mara 10 (ingawa sii mapendekezo yangu) Marais wote wa pande mbili na wabunge wake washirikishwe ktk uchaguzi wa tume kisha hiyo tume ichague viongozi wake wenyewe mwenyekiti, katibu na kadhalika bila kuwekewa masharti ya sehemu zipi wasiziguse kwa sababu uamuzi wa mwisho bado watakua nao hao viongozi wetu na wanaweza kutuambia kwa nini kipengele kadhaa hakitabadilishwa..

Jamani - Baraza la Mapinduzi, Zanzibar karibu wote wamekwisha kufa na siku zote Muungano wetu ndio umejengwa kuhakikisha usalama wa mapinduzi yake sii kundi la watu, iweje bado Baraza hilo liwe na mamlaka makubwa kwa serikali ya Zanzibar wakati kuna wafuasi wa vyama vingine ambao sii wajumbe wa baraza hilo... Yaani hawa hawana mamlaka ya Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar?..Sii ndio kusema Zanzibar haitawaliki na chama chochote zaidi ya CCM!

Tunahitaji uchama na kuwalaumu Chadema hata kufikiria haya machache kwa sababu tu wabunge wa CCM au CUF hawakuona tatizo hili?
Asante Mkuu Mkandala kwa kutanguliza maslahi ya taifa kwenye hili!.
Thanks.
 
Kuna watu wanataka kuandamana kuunga mkono muswaada huu, na kuna watu wanataka kupinga. Mleta mada ana hoja ambayo watu wa upande fulani wanataka kutuonyesha kwamba haina nguvu kwa sababu hii nchi ni yetu wote kwa hiyo wote tupo responsible.

NOOO!!!.... Waliotaka kuupinga huu mswaada wamepoteza opportunity ya ku-showcase their poits not only kwa wabunge wanaoisupport hii bill, bali hata kwa wananchi lukuki waliokuwa wakiangalia TV na mitandaoni, pia wahisani,mabalozi na wageni wengine walokuwapo. Kutoka nje sio uanamapinduzi kama mnavyofikiria, haiwavutii wahisani kama mnavyofikiria, na CDM kutaka kuoanana na rais ilishaongelewa wakati Slaa,Salim A. Salim na jaji warioba walipokutana.
Ni sarakasi tu, walijua watakachofanya ila walitaka kuonyesha wageni uanamapinduzi wao, too bad it didnt work that well.

Soby, asante sana kwa kuangalia from outside the box. Jf ni jukwaa huru, ila wengi wetu humu ni mashabiki wa vyama na tunajikuta tunalazimisha kutetea hata madhaifu ya vyama vyetu kifikia kiwango cha kuviona ndio grund party na viongozi wake ni malaika.

Enyi wapenzi wa vyama, pendeni vyama vyenu kwa mioyo yenu yote, ila pia vinapokosea, vikosoeni humo humo ndani ya vyama ila vinapokosolewa, kubalini matokeo.

CCM imechokwa, hili ni la kuvunda, halihitaji ubani. CUF bado iko kwenye fungate na Chadema ndio hii, bado haijajipanga!. 2015 tutegemee nini?.
 
Hayo maneno yako ya mwisho kusema kweli huwa najiuliza sana... Unakumbuka uchaguzi wa Igunga? tulisema nini wengine tukaonekana wachawi na matokeo yakawaje...

Hata hivyo harakati za katiba mpya hazikutakiwa kuanza leo. Tukumbuke kwamba CUF walikutana mna vishoka kama hivi vya Chadema wakaomba katiba mpya na kabla hawajiweka sawa wakamalizwa na Udini. Leo CHadema nao sijui kama wanaweza badilisha lolote kufikia 2015. Lakini kumbuka tu mkuu wangu Chadema can do nothing to change the results of 2015 ndani ya katiba hii - Haiwezekani na hakuna chmaa kinachoweza - KUJIPANGA ndani ya mfumo huu..
 
Naomba unieleze CDM kutokuwa na wabunge 220 kumetokana na ubovu wa katiba?
 
Bila shaka, mkuu wangu kama kiongozi wa NEC inachaguliwa na rais na sii taasisi huru unategemea kupata majibu gani. Siku zote ktk maisha mtumishi humtukia bwana wake, hakuna kitu uchaguliwe na rais kutumikia kwa maslahi ya Umma bali yale maslahi ya mwajiri wako sasa inategemea na rais aliyepo madarakani. Hakuna njia ya mkato ni ukweli ambao hauna maelezo mengine.

Halafu wewe umeishi majuu unajua fika jinsi Jeshi na Polisi linavyotetea na kulinda maslahi ya nchi na sii ya rais au chama kama kwetu. Rais mwenyewe ni mnyenyekevu kwa wananchi na hawezi hata siku moja kutoa hotuba ya hasira kwa wananchi. Huwezi kukuta vyama vina uadui wa namna hii kwa sababu katiba yetu imeundwa kulinda chama tawala na kila mahala ukiona kuna mtafaruku kama wetu ni kwa sababu ya katiba yao inajenga Udikteta.
 
Hayo maneno yako ya mwisho kusema kweli huwa najiuliza sana... Unakumbuka uchaguzi wa Igunga? tulisema nini wengine tukaonekana wachawi na matokeo yakawaje...

Hata hivyo harakati za katiba mpya hazikutakiwa kuanza leo. Tukumbuke kwamba CUF walikutana mna vishoka kama hivi vya Chadema wakaomba katiba mpya na kabla hawajiweka sawa wakamalizwa na Udini. Leo CHadema nao sijui kama wanaweza badilisha lolote kufikia 2015. Lakini kumbuka tu mkuu wangu Chadema can do nothing to change the results of 2015 ndani ya katiba hii - Haiwezekani na hakuna chmaa kinachoweza - KUJIPANGA ndani ya mfumo huu..
Mkandala, 2015 bado ni mbali sana!. Sasa hivi tuko buzy tukifanya mass mobilization kupitia maandamano!. Wakati wakujipanga ukifika, tutajipanga!.
 
Na CCM wanafanya makusudi sana ktk hili la Katiba, wakija shtuka 2015 hiyooo! hawana viongozi ktk halmashauri, kata, madiwani na mabunge wa kotosha....Mimi nadhani kisiasa CDM wameisha maliza kazi ya kujitangaza sasa hivi ni kueleza ofisi zao maeneo yote ya mikoa ingawa kifheda sidhani kama wataweza lakini wakiweza ku mobilize watu bila shaka wapo wa kujitolea maana hata TANU ilianza hivyo hivyo..
 
Bila shaka, mkuu wangu kama kiongozi wa NEC inachaguliwa na rais na sii taasisi huru unategemea kupata majibu gani. Siku zote ktk maisha mtumishi humtukia bwana wake, hakuna kitu uchaguliwe na rais kutumikia kwa maslahi ya Umma bali yale maslahi ya mwajiri wako sasa inategemea na rais aliyepo madarakani. Hakuna njia ya mkato ni ukweli ambao hauna maelezo mengine.

Halafu wewe umeishi majuu unajua fika jinsi Jeshi na Polisi linavyotetea na kulinda maslahi ya nchi na sii ya rais au chama kama kwetu. Rais mwenyewe ni mnyenyekevu kwa wananchi na hawezi hata siku moja kutoa hotuba ya hasira kwa wananchi. Huwezi kukuta vyama vina uadui wa namna hii kwa sababu katiba yetu imeundwa kulinda chama tawala na kila mahala ukiona kuna mtafaruku kama wetu ni kwa sababu ya katiba yao inajenga Udikteta.
Vyote ulivyovisema ni talking points, ni maneno yaliyokaa vizuri kimashairi, ila hayatoki moyoni mwako na huamini hivyo.
 
Alaaa mkuu wangu umekuwa mnajimu mara kujua yatokayo rohoni mwangu. Hata hivyo ni Reality itoke rohoni mwangu ama kwako, hakuna mtu yeyote anayeweza kuajiliwa na Boss kwa maslahi nje ya mwajiri wake...Atafuata sera na ilani za kiongozi huyo (Chama) maadam yeye mwenyewe ni mwanachama wa CCM.. hii haihitaji Phd mkuu wangu. Na ndio maana CCM wamehakikisha kila mkoa na wilaya kuna mkuu wa mkoa mtu aliyechaguliwa na rais na vyombo vyote vya usalama viko chini yao.

Kutoka moyoni mwangu ni kwamba bila katiba inayoweza kuondoa mamlaka ya moja kwa moja ya rais ktk maswala ya usalama bila kuwepo kamati ya bunge la Usalama ambayo ndio tamshauri rais kwa jambo lolote na sii rais kuwaambia la kufanya vyombo hivyo kupitia ma RC na DC.. Uhuru wa kweli hautapatikana.. Kifupi, NEC wanatakiwa kuwa huru na hilo pekee ni ushindi kwa CCM miaka yote toka enzi za NCCR, CUF na itaendelea kuwa hadi hapo NEC itakapokuwa huru.
 
Mkuu Mkandara, hilo pia linawezekana kwa kupata katiba mpya, muswada Utasainiwa by Jumatano, tuwashauri wote wasisusie kuipa ushirikiano tume ili tupate katiba bora.

Kwa kutoipa ushirikiano tume, tutabakiwa na katiba hii hii iliyopo na kupitia kwayo, CCM itatawala milele!
 
Hindi ndivyo nisemavyo kila siku, watu waacha mada muhimu na kujikita katika kuposha mada.
Hata kama kifungu 86 kilishatumika huko nyuma, Chadema walipaswa kukumilisha ili hansadi ziweke kumbukumbu na miaka 100 toka sasa wajukuu zetu wakija kutusuta waje waseme wapo waliojaribu wakazidiwa nguvu na watawala WALIOKUWEPO hivyo kutohukumiwa.
Kwa hili ni uungwana wa kawaida kusema Chadema hawakuwa makini na wamepoteza fursa ambayo kiutaratibu na kimuongozo wa bunge kifungu 86 wamechemsha.
 
mmmmmnnnh mbele kiza. Tukiwapa ushirikiano Upinzani hautashinda milele na tukiwanyima itarudi hii kukuu ilopakwa rangi mpya na tutawaliwa milele - kazi kweli kweli....
 
Faiza Fox asante kunisaidia kuelimisha hili, Mhe. Tundu hakutoa pingamizi, alitoa maoni. Ukitoa maoni bunge linasikiliza tuu, wanaweza kuamua kuyazingatia au kuyapuuza. Lakini kama angetoa pingamizi, spika hana mamlaka ya kuzuia, wala hana uamuzi asikilize au la, ni lazima asimamishe kila kitu, asikilize lile pingamizi na wabunge kulichangia na ndipo aliulize bunge kufikia uamuzi.

Naendelea kusisitiza kutowasilishwa pingamizi was a mistake, ila pia lazima niikubali hoja ya Mzee Mwanakijiji kuwa sio kosa la Chadema wala tuwatwishe huu mzingo wa lawama, kwa sababu kanuni ziko wazi, mbunge yoyote angeweza kuwasilisha pingamizi, sio lazima mpaka Lissu tuu au Chadema.
Nashangaa kwa nini hadi leo post hii hajawekwa kule juu na title ya uzi huu haijabadilishwa!
 
Jamani kila kitu chama cha magamba walishapanga, sasa unachowalaumu chadema ni nini? Na we ni gamba (snakes ;>)
 
Hindi ndivyo nisemavyo kila siku, watu waacha mada muhimu na kujikita katika kuposha mada.
Hata kama kifungu 86 kilishatumika huko nyuma, Chadema walipaswa kukumilisha ili hansadi ziweke kumbukumbu na miaka 100 toka sasa wajukuu zetu wakija kutusuta waje waseme wapo waliojaribu wakazidiwa nguvu na watawala WALIOKUWEPO hivyo kutohukumiwa.
Kwa hili ni uungwana wa kawaida kusema Chadema hawakuwa makini na wamepoteza fursa ambayo kiutaratibu na kimuongozo wa bunge kifungu 86 wamechemsha.
Chadema hawajachemsha!. Saa hizi wako lunch Ikulu!.
 
Wanabodi,
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.

Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja kuhodhi madaraka yote ya dola.

Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.

Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the bettle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.

Wasalaam
Pasco (wa jf).

Nimejaribu kuipitia hii post yangu na kulinganisha ni kinachoendelea nimekujikuta I was right somehow.

1. Kitendo cha Chadema kumuona rais Jakaya Kikwete, ni dalili ya kukubali yaishe, hili ni jambo jema!
2. Kwa mujibu wa taarifa rasmi, wataipa tume ushirikiano na tutaweza kusonga mbele, hili pia ni jambo jema.
3. Nakiri kuwa hoja yangu ya kuwaambia Chadema walikosea, imepigwa chini, hawakukosea, hivyo hawana sababu yoyote ya kuomba radhi.
Leo au kesho muswada unasainiwa kuwa sheria, this time Chadema wataalikwa kwenye signing ceremony, na kama kawaida yao watasusa sherehe lakini wataipa tume ushirikiano!.

All and all, life goes on.

Wasalaam

Pasco.
 
Kama nakuona vile ulivyo na furaha! 'Hongera sana' kwa kuyaona haya mapema!
 
Back
Top Bottom