RealMan
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 2,367
- 1,395
..........ijapokuwa maudhui ya barua ni mazuri ila kina kitu kimefichwa nyuma yake na hicho ndio intention ya barua hii ya kipuuzi. Binafsi siiungi mkono waachie wananchi wote wawakilishe mawazo yao bila ya kujali dini wala kabila lao kwani Tanzania ni kwetu sote.
Mdondoaji nimefuta amabyo nimeona hayakuwa relevant kwangu.
Ila hayo ulosema hapo juu ndio haswa tunapaswa kujikita kwayo. Mpaka sasa mswada umwemtoa mwananchi na haionekani wapi mwananchi atakuwa na nguvu ukiondoa "referendum (part iv sec 26)".
Tunabaki kutegemea pasonalities ili kufikia mabadiliko tarajiwa. Kwa mfano tutasema "Tume ikiongozwa na Prof Shivji tunaweza kupata katiba nzuri". Ni vipi akiwa mtu mwingine ambaye anahisia za upendeleo 'bara na unguja'??? Lakini bado hata akiwa Shivji anaweza asifanye lolote maana Hadidu za Rejea zinatoka Ikulu.
Nadhani tuna kumbukumbu ya kilichomtokea Jaji Kisanga pale Diamond jubilee hasira za Mkapa zilipomwangukia.
Jibu ni wananchi ku-unite tuache huu udini maana mateso tunayopata kwa katiba dikteta yanatuumiza wote.