KATIBA: Askofu Ruzoka amlima barua Waziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KATIBA: Askofu Ruzoka amlima barua Waziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Apr 5, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Editable text:

  HOFU NA MASHAKA YA WANANCHI KUHUSU
  MUSWADA WA MAPENDEKEZO YA KUTUNGWA KWA SHERIA
  YA MABADILIKO YA KATIBA YA NCHI YA MWAKA 2011

  Kwa
  Waziri wa Katiba na Sheria

  Mheshimiwa Waziri,
  Muswada wa Mabadiliko ya Katiba ya Nchi wa mwaka 2011 Namba 1 wa tarehe 11 Machi, 2011 umetangazwa katika siku chache zilizopita.

  Baada ya kuusoma muswada huu tulishangazwa kuona kwamba mchakato wote unaanzia na kuishia kwa Rais na kwamba Chombo Kikuu cha kuratibu mchakato wote ni Tume itakayoteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala.

  Tunatambua kwamba kilio cha kutaka Katiba mpya kilitokana na utashi mwema na pia hasira njema ya jamii ya Watanzania wakitaka mabadiliko yaliyo na hekima na utu.

  Tunahofia kwamba maudhui na mwelekeo wa muswada wa marekebisho ya Katiba unaopelekwa Bungeni havitakidhi mahitaji mazito ya watu na huenda ukachochea hasira ambayo imekwisha jidhihirisha katika jamii yetu.

  Tunakuomba ulisimamie zoezi la marekebisho ya katiba kwa hekima sana ukiongoza tafakari jadidi na elimu angavu itakayowezesha zoezi lote kuwa la mazungumzo ya kitaifa kweli kweli huku amani, maelewano na makubaliano vikilindwa sana katika wakati mgumu huu.

  Tafadhali lipatie taifa muda wa kufaa na chombo huru kinachoaminika kuongoza wananchi kufikia makubaliano yatakayojenga msingi imara wa taifa letu kwa wakati ujao.


  Askofu Mkuu Paulo Ruzoka
  MWENYEKITI

  TUME YA HAKI NA AMANI (TEC)

  5/4/2011
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu sijui kama umesoma vema; sijaona kipengele ambacho kasema USIENDE Bungeni ama alikosema Serikali iwe na dini.
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  ASKOFU ni raia wa TANZANIA
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  suala la kutofanya utafiti linaendelea
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Appreciable initiative, but i smell something fishy on this innocent thread.

  Watchful waiting.
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kama ni mwelewa na anasimamia haki, atafuata alyoelekezwa kwenye barua kwa manufaa ya waTZ wote!

  Mungu ibariki Tz, Mungu tubariki waTz!
   
 8. M

  MBANINO Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo yameanza sasa.

  Ni dhahiri huu mchakato unaburuzwa kwa nia ya kulinda maslahi ya baadhi ya watu na haswa watawala pasipo kujua ya kwamba Katiba ni ya Watanzania wote.

  Waliongea wadau na washiriki mbalimbali katika kongamano la kujadili mchakato wa Katiba mpya pale Chuo Kikuu sehemu ya Mlimani na kikubwa ni kwa wengi kutokuridhishwa na jinsi zoezi lenyewe linavyoendeshwa. Tunahitaji tume huru ambayo itakuwa tayari kuchukua maoni ya walio wengi na kuyafanyia kazi.

  Je, suala hili linavyoendeshwa kwa sasa tuendelee kuwa na imani nalo? Sidhani, kama serikali wanania ya dhati kabisa ya mabadiliko haya. Barua ya Askofu Ruzoka ni mwanzo mzuri wa kuonyesha kutoridhishwa na uendeshaji wa mchakato huu unaofanywa na serikali kwa sasa.
   
 9. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu invisible.

  Tunashukuru kwa viongozi wetu wa dini kwa kuliona hili. Huu ni ukweli usiojificha huo muswaada una mapungufu, kwanini viongozi wetu wana tamaa ya madaraka.

  Comrades, your time is over waachie na wengine jamani kama wewe ni mpenda amani unayoitangaza kila siku step down basi
   
 10. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mmmmmh jamani mambo ya shakuwa mambo,

  Kama serikali itaendelea kukaidi maoni ya wananchi naona watakuwa wameruhusu wenyewe Nguvu ya umma ichukue hatamu katika kujenga katiba.....
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  kanisa likishasema basi hakuna wa kupinga!muswada umeshagonga mwamba!
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwani wapi amesema usipelekwe bungeni? Halafu wapi ameongelea dini jaman? Si ifike mahali tuache ushabiki wa kidini kwny mambo ya msingi?
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wale wale wasiofanya utafiti na kufikiri kabla ya kuchangia
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  kama ni mwelewa na anacmamia haki, atafuata alyoelekezw kwnye barua kwa manufaa ya waTZ wote! Mungu ibarik Tz, Mungu 2barik waTz!
   
 15. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0

  Tatizo lako unatumia mak**** kufikiri badala ya ubongo. Kuna sehemu umeona wamesema usiende bungeni? Au kwamba serikali ina dini?
   
 16. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo utakuwa unabishana na hayawani.
   
 17. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kama sehemu ya jamii, Kama wadau wa amani na utulivu, Kama wadau wa maendeleo, na kama Watanzania, nakubaliana kuwa viongozi wa dini kwa kuwakilisha wanaowaongoza watoe maoni yao yao mama kukubali au kupinga mchakato huu.

  Naamini serikali inatakiwa ijue kuwa yenyewe bila ushiriano wa wananchi na makundi mbali mbali ya wananchi haitaweza kutengeneza katiba inayotosheleza matakwa ya watanzania wengi.
   
 18. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  piga ua ufisadi utafikia kikomo very soon.  1) wakibadili katiba na kuwapa wananchi katiba wayoitaka, kuna uwezekano mkubwa CCM ikatoka madarakani, ika vunjika na mafisadi
  kushugulikiwa.


  2) wakileta mzaha na kutengeneza katiba wanayoijua wao kwa mchakato wao , basi watakua wanatengeneza mazingira ya North Africa
  (na huko uarabuni) na mwisho wake BADO mafisadi itabidi waondolewe
   
 19. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hivi kwanini Kupeng'e unakimbilia sana U-DINI?

  Katiba mpya lazima ijumuhishe makundi yote ya JAMII - Should transcend all boundaries! BAKWATA,KKKT, & TEC all inclusive.. Tukianza kutizamana kwa jicho la udini tutakuwa tunawapa wanasiasa nafasi ya kuendelea kututawala with impunity!

  Jaribu kuwa na POSITIVE ATTITUDE angalau kwa mambo yanagusa maisha ya Watanzania wote!

  Ni hayo tu
   
 20. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kupeng'e aka malaria sugu, aka jeykey wa ukweli, aka mtoto wa jeykey, aka francis muro, aka basra rashid, aka jinomswakiwanini, aka.....; wewe ulitaka aandike yeye kama yeye kwa sababu gani wakati taasisi ipo?

  Na wewe mwandikie huyo waziri mkuu kupinga barua ya TEC.
   
Loading...