Kati ya Tanga,kibaha, mbeya, morogoro na songea MJI gani una gharama ndogo za maisha?

Kati ya Tanga,kibaha, mbeya, morogoro na songea MJI gani una gharama ndogo za maisha?

1Africa54

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2025
Posts
462
Reaction score
540
Kati ya Tanga, mbeya,kibaha , morogoro na songea MJI gani una gharama ndogo za maisha?
Haswa mzunguko wa Hela
Upatikanaji wa misosi
Utulivu
Huduma za jamii
Kwa anae jitafuta
 
Songea gharama ya maisha ni ndogo sana. Kuna maeneo kama bombambili boda bado ni jero. Ila mzunguko wa pesa ni mdogo sana hivyo ni ngumu kupata pesa. Pia umbali kufikq majiji ya Tanzania linapafanya kutokuwa sehemu nzuri ya kuweka makazi. Morogoro ni pazuri zaidi kwa vyakula,gharama za maisha na ukaribu na sehemu muhimu
 
Maisha popote mkuu
Hapo hapo ulipo wanapokujua watu wengi pana fursa kuliko huko wasikokujua

Ni wewe na akili yako na jicho lako la kuona fursa

Kama unadhani huko kuna unafuu unajidanganya

Matatizo hayakimbiwi tafuta solution hapo hapo ulipo
 
Kati ya Tanga, mbeya,kibaha , morogoro na songea MJI gani una gharama ndogo za maisha?
Haswa mzunguko wa Hela
Upatikanaji wa misosi
Utulivu
Huduma za jamii
Kwa anae jitafuta
Nenda moro mjomba hiyo ndio back up yangu Life time.
 
Kati ya Tanga, mbeya,kibaha , morogoro na songea MJI gani una gharama ndogo za maisha?
Haswa mzunguko wa Hela
Upatikanaji wa misosi
Utulivu
Huduma za jamii
Kwa anae jitafuta
Nyie hamjui tu uzuri hiyo miji yote nimeishi, Tanga ndio mji unamfaa mtu anae anza maisha, maisha cheap sana tanga jamani, kuanzia makazi, ujenzi, chakula na mambo mengine mfano
Bidhaa nyingi zinaingia toka zenji, ziko cheap, chakula karib kila kitu kinalimwa tanga usambaani huko, viwanja, aisee kule 15 km kutoka city centre unapata kwa 1mill, viwanda vya cement vimejaa pale cement bei cheap, utelezi ni cheapest, room za kupanga, room 40,000 dar ni 100,000. Ukitaka kuoa kule mke wapewa tu bure tu.

Kikubwa zaidi bado unapata vibes kama uko dar tu, mji wa mwambao ule, ukitaka kwenda mombasa safar ya masaa 3 tu.
 
Songea ruvuma HIYO back days 2019 chips yai buku nilichoka nikaogopa kuzila nika HISI Zina TATIZO. Half keki 100 alafu KUBWA balaa. Pale stendi ugali KUKU WA mchuzi buku mia Tano au buku mbili ILE SIJUI ni nchi tofauti



Kwishaaaaaa
Kama atafanyavuamuzi wa kwenda huko kwa hoja ya bei ya chipsi yai na keki basi ana safari ndefu kwenye haya maisha
 
Back
Top Bottom