Kati ya Reginald Mengi na Mbwana Samatta, nani alistahili kupewa mtaa?

KAYABOMBICHI

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
296
142
Nimemsikia mkuu wa mkoa wa Daresalaaam akiahidi kumpa mtaa mchezaji wa kimataifa Mtanzania Mbwana Ali Samatta kwa kuitangaza nchi vizuri kupitia michezo.

Sina kinyongo na hilo lakini ninachokiwaza ni kuwa Mzee Mengi amekuwa na mchango mkubwa katika taifa hili kwa ujenzi wa uchumi na kutoa ajira kwa watanzania wengi. Amesaidia kujenga hospitali, mashule, misikiti, makanisa na kadhalika.

Je, yeye hakustahili kuenziwa kwa kupewa angalau mtaa?
 
Usijali mkuu. Mengi alishapewa mtaa mzima mioyoni mwa wale wote aliowasaidia kwa namna moja ama nyingine kama walemavu na wote walioona na kuthamini kile alichokuwa akikifanya kwa jamii.
 
Mwacheni Mzee Mengi apumzike,Mtaa utamsaidia nini?Muombeeni kwa Mungu amfanyie wepesi huko aliko.Apumzike kwa Amani.
 
Mengi kapewa shule nyingi ikiwemo pale Moshi kuna Reginald Mengi primary school
Jina lake litachukua vizazi kadhaa kuja kusahaulika.
Ameacha alive legacy!
 
Kampuni yake kupewa jina la kituo cha mabasi ni moja ya heshima kubwa sana hata kama sio jina lake ila kazi yake imeheshimiwa.
Kwanini haikuwa TBC Bus Stand ikawa ITV Bus Stand?

Cc ITV Mwenge
 
Dunia haijafika mwisho anaweza kupewa siku wakikumbuka hilo ikifika
 
Nimemsikia mkuu wa mkoa wa Daresalaaam akiahidi kumpa mtaa mchezaji wa kimataifa Mtanzania Mbwana Ali Samatta kwa kuitangaza nchi vizuri kupitia michezo.

Sina kinyongo na hilo lakini ninachokiwaza ni kuwa Mzee Mengi amekuwa na mchango mkubwa katika taifa hili kwa ujenzi wa uchumi na kutoa ajira kwa watanzania wengi. Amesaidia kujenga hospitali, mashule, misikiti, makanisa na kadhalika.

Je, yeye hakustahili kuenziwa kwa kupewa angalau mtaa?
Kuna Mzee mmoja alisema kwenye msiba pale kwake(Kinondoni) yakuwa yupo tayari kutoa Kiwanja chake pembeni ya Petrol ya Bamaga ujengwe mnara wa kumbukumbu ya Mengi.. Sasa wale wazito waliokuwa wanasema wata muenzi basi wachukue changamoto hiyo.
 
Kila Mtu na nafasi yake na kila Mtu na Zama Zeke, mwacheni Mzee wa Watu apumnzike.

Leo ni siku nyingine muda mwingine na leo sio kama jana, na jana sio kama leo.

Mbwana kapewa flavor zina mstahili na Mzee wetu pia alipewa Flavor zinazo mstahili kiufupi tusambaze Love tu.
 
Kuna baharia mmja wa zamani
Anaitwa rubama,Ali force kingi mpk mtaa ukapewa Jina lke
Mwanzo walitaka kuipa Jina tofauti akawambia msinitanie andikeni Jina langu mkongwe

Ova
 
Back
Top Bottom