Mbwana Samatta apewe Shahada ya Udaktari wa Heshima

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Napendekeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimtunuku Mbwana Samatta shahada ya udaktari ya heshima (Honoris Causa) kutokana na mchango wake
mkubwa katika tasnia ya mchezo wa soka. Mchango wake unatokana na mambo yafuatayo:-

1. Amekuwa mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi ya daraja la kwanza ya Uingereza (EPL), ligi ambayo inashika namba moja kwa
umashuhuri ulimwenguni
2. Amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya mabingwa ya klabu za Ulaya na kufanikiwa kufunga goli dhidi ya klabu ya Liverpool,
moja ya timu bora sana nchini Uingereza
3. Amekuwa Mtanzania wa kwanza kucheza kwenye uwanja wa Wembley, uwanja mashuhuri sana wa mpira wa miguu jijini London

Nimependekeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuwa mpaka sasa ni chuo pekee nchini kinachotoa shahada katika tasnia ya michezo.
Haitakuwa ajabu kwa Mbwana Samatta kutunukiwa heshima hii. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Manchester kimeamua kumtunuku mchezaji kijana wa Manchester United
Marcus Rashford degree ya udaktari kutokana na mchango wake katika soka na pia kusaidia watoto maskini.

Nawasilisha
 
Hayo matope kichwani mwako sijui yatanyonywa lini yakamwagwe... Ni hatari sana ujue?
 
Mchanganuo wake uwe hivi:

Kwasababu ya magoli mengi kuyafunga kwa kichwa apewe certificate.

Kwasababu ya kucheza Genk na TP Mazembe apewe diploma.

Kwasababu ya kucheza EPL apewe bachelor

Kisha kwasababu ya kucheza UEFA na kuifunga goli Liverpool ndiyo apewe hiyo PhDkabisa maana naona mnaanza kuleta mzaha kwenye PhD
 
Degree apewe tu....sisi huku mbagala tunasubiri kushangilia...ukiwa na HELA kila kitu kinakuja..
Pesa,wanawake,elimu,mabodigadi na chawa mob!
 
Kwa nini asipewe hata Nasibu, ambaye kupitia sanaa yake basi amegusa maisha ya vijana wengi wanaoishi vizuri na kusaidia ndugu na jamaa zao? Huyo samatta zaidi ya ninyi washabiki wa mpira mnaopata burudani hiyo ana lipi la ziada ktk kuwainua vijana wenzie, utasema "role model" .
 
Mazungumzo ya kwenye baa yanafurahisha. Katina inasema kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake ila asivunje sheria
 
Kwa nini asipewe hata Nasibu, ambaye kupitia sanaa yake basi amegusa maisha ya vijana wengi wanaoishi vizuri na kusaidia ndugu na jamaa zao? Huyo samatta zaidi ya ninyi washabiki wa mpira mnaopata burudani hiyo ana lipi la ziada ktk kuwainua vijana wenzie, utasema "role model" .
Acha wivu mbona umeongea kama mtu ambaye anashindwa kuyachambua mambo kwa jicho la 3

Kama uko na akili timamu Hauwezi kubeza kabisa mchango wa samata ... Mimi sio shabiki wa samata hata kidogo but kuna wakati ukifika ukweli huwa unapaswa kuzu gumzwa hata kama huo ukweli utakuwa ni mchungu kuumeza

Kwa kupitia samata Nchi yetu inapata kupeperusha Bendera yake zaidi kimataifa na kuifanya Tanzania ijulikane zaidi kwa watu wengi ulaya nzima na dunia nzima kiujumla

kumbuka kwamba samata anacheza katika league kuu ya uingereza na kabla ya hapo awali alikuwa anacheza katika team ya Genk ambayo ipo Belgium na msimu wa league ya Belgium ulipoisha mwaka Jana samata alikuwa ni mfungaji bora wa League hiyo timu yake ikatangazwa kuwa bingwa na yeye pia akashinda tuzo nyingine ya kuwa Mchezaji bora toka Africa katika league hiyo ya Genk

Kisha akaja kusajiliwa katika league ya uingereza amecheza katika team yake hiyo mpya iliyo msajili kwa kiwango kizuri tu na ifahamike kwamba kila week alikuwa anashuka dimbani na kucheza mpira samata amewahi kuifunga Liverpool na man city ambazo ndio team giant kwa sasa pale uingereza Kupitia hiyo performance yake nzuri aliyo ionyesha kuna raia wa nchi mbali mbali duniani kote watataka kujua Huyo samata ni nani na anatokea nchi gani

wakishaijua nchi anayotokea kwa watu wanaojua kuzichangamkia fursa wata taka kujua fursa za uchumi zinazopatikana katika nchi yetu kuna wengine pia watatambua kwamba Tanzania ni nchi nzuri ambayo inavivutio vingi vya utalii kupitia samata nchi yetu itakuwa imejitangaza kimataifa itapata watalii mbali mbali toka sehemu mbali mbali duniani kote pia itapata investors toka sehemu mbali mbali duniani na taifa litapata kipato

Hao investors wakija kuwekeza huku watu wataifa hili watapata ajira kuna watakao ajiriwa na kuna ambao watapata fursa za kiuchumi kupitia hao investors ... Usisahau pia hao watalii watakapo kuja nchini watakuwa wana kuja na pesa za kigeni ambazo zitaongeza nguvu ya uchumi. .pia watu wataifa hili watapata ajira pamoja na connection toka kwa hao watalii " pia kupitia samata maskauti wa team kubwa za huko duniani wataanza kuitolea macho Tanzania na kuja kuangalia vijana wenye vipaji nchini na huwenda ikaja kuwa ni fursa nyingine ya kiuchumi kwa vijana wa taifa hili ........

Sikatai kuwa diamond amefanya vizuri Sana na anastahiki sifa
Lakini how come uanze ku-compare na mtu ambaye ana link na hiyo chain ya fursa zote nilizo ziorodhesha katika hii comment

Tunapo kuwa tuna discus vitu vya maana tuwe tunajenga desturi ya kuweka ushabiki na ujinga pembeni

Natanguliza shukrani
 
Na yule wa kenya ambaye alichukua UEfA kabisa na inter apewe uprofesa???

Acha ullimbukeni samatta!
Mimi nimempendekeza Samatta kwa sababu nilizotoa. Wala sikuona busara na kumlinganisha na huyo Mkenya wala Nasibu. Yeyote mwenye sababu anaweza kuwapendekeza. Mbona wanasiasa wanapewa hizo degree za heshima? Nimetoa mfano kwamba Rashford anatunukiwa hiyo doctorate?
 
Samatta amefeli kuonesha ubora wake pale Villa park,hatimae wanataka kumtema atimkie Uturuki huko.

Wenzake huwa wanaenda Uturuki,Qatar,Marekani kumalizia mpira lakin yeye ndo anaenda kupata maendeleo ya mpira ni kama vise versus
 
Labda unamaanisha udaktari wa kuziba pancha na kufuma mipira.

[SUB]just kidding[/SUB]
 
Back
Top Bottom